Khah, First Date iliyonitoa jasho. . .

mmmh, uje na helmet ya tindikali
au uje na tester ya sumu kwenye pilau.
si unajua nilivyo na roho mbaya kwenye milki zangu??

Kama una roho ngumu karibu.

Wala haina shida nataka nikuletee boxi la misumari ya kupamba mezani.. Na shoka incase mifupa ya kuku ikiwa migumu.
 
Kuna bidada nilimpenda tangu siku ya kwanza nilipomuona.. Nikaona nijenge naye mazoea kwanza..

Mazoea yakaendelea weee... Mi nikafurahia hiyo hali...

Alikuwa na mvuto wa aina yake kwa kweli..kila jinsia ilikuwa inamkubali kuwa yeye ni kifaa.. Yaani ilikuwa naona sifa sana nikimwita mbele ya watu ili wajue mi ndiye mmiliki na yeye alishanizoea..

Watu walikuwa wananionea wivu na gere,kwa walau kuwa na uwezo wa kumwita akaitika. Wengine wanamgwaya..

Nilipoona inatosha,nikasema ngoja "nimtokee"... Nikamwambia achague kati ya lunch na dinner... Kimapepe akajibu "vyote viwili".. Mi nikatoa 5,000 mbili nikampatia.. Nikamwambia dinner itakuwa saa 1 mahali fulani,lunch sitaweza..

Mzee mi saa 12 nikawa lile eneo la tukio.. Natafuna karanga,bisi,korosho,na juice pembeni..

2 na nusu akatia timu.. Baada ya msosi.. Nikaamua kuanza kumwaga sera.... Huwezi amini.. Alinishangaaje!
Akasema anasikitika sana kunipoteza rafiki kama mimi..

Nikamwambia ndiyo tunakuwa karibu tukiwa na mahusiano ya kimapenzi.. Akanijibu kuwa sijamwelewa..
Akasema alinichukulia kama rafiki,alinithamini kama rafiki tu.. Akinitembelea anakaa hadi kitandani(enzi hizo nina room moja). Na aliamini haingeweza kutokea mimi kumwambia masuala yale...

Kilinishukaje!
Nikambembeleza(ye hapo ashachukua pochi yake),kuwa basi nafuta kauli yangu.. Akajibu,haitafutika akilini mwake.. Na akasema nimemsaidia kwa kumpa fundisho hilo kwani wanaume wengine wakija kwa dizaini hiyo atastuka mapema..

Nilisikitika na kuona aibu sana.. Akaniaga,na kutokomea!

Date hiyo umeionaje Konnie(mleta uzi)?

mara nyingi ukilianzisha kama marafiki ujue ndio imekula kwako.
ni vigumu huko mbele ya safari kubadilisha muelekeo.lol.
 
Kongosho! Unanichanganya sana mpaka nashindwa kukuelewa, Mara ulete thread kwamba wamkumbuka sofia wako na kujutia kisha leo eti first date yako ukiwa msichana! Kweli ndo maana hapa JF wakakubandika jina la 'shemale' Leo unalikubali hilo jina au unalikataa?
 
Hiyo kali sana...ila mi first date ile nakutana na girl wa watu polisi wakanikamata hapo hapo mbele yake
 
Hahahahaha!uwiiii!x-mke mwenza una den huku hahahaha!umevunja mbavu zangu mie lol!naimajin wakati mali zinatolewa ulivokua umetoa jicho na moyo kwenda mbio hahahaha!
 
Back
Top Bottom