Kesi za migogoro ya ndoa zaipiku ya ardhi

Malcolm X5

JF-Expert Member
Jun 3, 2013
1,628
2,720
Wizara ya Katiba na Sheria imesema migogoro ya ndoa ni miongoni mwa mashauri yaliyoshika kasi kwa kuongoza kuripotiwa ikilinganishwa na mengine nchini.

Imesema kati ya Januari hadi Juni mwaka huu, mahakama zimepokea mashauri 4,982 huku yanayotokana na migogoro ya ndoa yakiwa 1,282, ardhi 1,074, matunzo ya watoto 523, makosa ya jinai 148, ukatili wa kijinsia 378 na migogoro ya kazi 148.

Hayo yalisemwa jana na Waziri wa Katiba na Sheria, Dk Harisson Mwakyembe alipokuwa akizungumza na waandishi wa habari kuhusu Muswada wa Sheria ya Msaada wa Kisheria uliowasilishwa bungeni hivi karibuni ambao unatarajia kuanza kujadiliwa na umma hivi karibuni.

Alisema migogoro ya ndoa ni tatizo kubwa linaloendelea kukua kwa kasi na kwamba limejitokeza katika maeneo mengi nchini.

Dk Mwakyembe alisema wanawake hasa wa vijijini ndiyo wahanga wakubwa wa migogoro ya ndoa kutokana na kukosa msaada wa kisheria jambo ambalo pia limeisukuma wizara hiyo, kuandaa mswada utakao wasaidia wasio na uwezo wa kulipia mawakili, kupata msaada wa kisheria.

“Hadi sasa mila zetu bado zinawakandamiza wanawake kwa kutowamilikisha mali, ardhi na vitu vingine. Hawa ndiyo waathirika wakubwa ambao talaka inapotolewa hujikuta wakikosa kila kitu. Muswada huu mpya utakuwa suluhisho kwa wasio na uwezo, kupata haki za kisheria,” alisema.


Chanzo:
Mwananchi
 
Tanzania ingekuwa na sheria ya ndoa ya mkataba ingekuwa mzuka sana.

Siku hiz ndoa nyingi zikibahatika kudumu miaka miwili ni ajabu sana. Yani baada ya hapo ni maigizo full.
 
Haya mambo ya haki sawa ni moja ya vichocheo vya talaka ni vigumu sana mwanaume wa kiafrika kukubali kupingwa na mke wake au kukosolewa
 
Back
Top Bottom