Nimegundua migogoro mingi inayopelekea watu kujazana mahakamani au mamlaka nyingine za kutoa maamuzi inaepukika

Mzee wa old school

JF-Expert Member
May 16, 2021
508
834
Wana jamvi, ni siku nyingine tena natumai muwazima kama nilivyo mimi leo, na kama ni hivyo.. basi Mungu ashukuriwe.

Kitaaluma ni mwanasheria.. kwa mujibu wa utafiti wangu usio rasmi, kwa kipindi cha "miaka 11" yaani toka 2013 hadi leo hii 2024, nilioufanya kwa kipindi ambacho nilikuwa mafunzo ya vitendo (field) wakati nipo masomoni, kufanya kazi za kujitolea (internship) mahakamani, taasisi mbali mbali za umma, na binafsi, mashirika ya kimataifa ya msaada wa kisheria. Nimegundua kwamba migogoro mingi, matatizo na dhulma ambayo ina pelekea watu kwenda kujazana mahakamani au mamlaka yeyoye ya kitoa maamuzi inaweza kuepukika na hata kama ikitokea haitochukua muda mrefu kuisha endapo tu jamii ikajua baadhi ya mambo muhimu na sio magumu sana kuyatekeleza ili kuepuka migogoro na hata ikitokea, basi muhisika kuwa salama.

*Sababu zinazopelekea migogoro,
1. Jamii kutokuwa na elimu sahihi juu ya maamuzi mbambali ambayo inayafanya. mfano; kununua ardhi, mambo ya ndoa, mirathi, kukopa na kukopesha, kazi n.k

2. Wataalamu wa masuala ya kisheria kutumia luga ngumu ambayo inafanya jamii kutoelewa kinacho endelea na pia inaleta ugumu kujifunza na kuelewa na hata siku nyingine mhanga kuongeza umakini. Mfano; nimeshuhudia wakili eti anamuelimisha mteja kwa kumwambia etiii "huna locus standae", mwengine nae anamwambia mteja eti issue yako ni re-judicata. Duuh! Nikajiuliza hivi kuna haja gani ya kutumia maneno magumu hivyo? Maana hapo hata mzungu mwenyewe kama sio mwanasheria au wakili hawezi elewa.

3. Ughari wa huduma za kisheria.. hivyo inapelekea raia kuogopa kabisa kuuliza jambo lolote linalotokana na masuala ya kisheria...

Sisi wa Tanzania ni ndugu, na ndoyo maana neno ndugu lilikuwa la kwanza kabisa kutamkwa katika mazungumzo ya aina yeyoye yale enzi hizo za Nyerenyere.

Hivyo basi, kwa akili zangu mwenyewe, bila kulazimishwa na mtu nimeamua kujitoa kuwasaidia wa Tanzania wenzangu kwa kuwapa elimu ya awali ambayo itawasaidia kuepuka migogoro isiyo na lazima....

Elimu hiyo nitakuwa naitoa humuhumu jukwa la habari na hoja mchanganyiko. Kwa sababu lengo ni kufikia jamii yote kwa ujumla wake.

Basi, Mungu awabariki.
 
Back
Top Bottom