Kesi ya kupinga ubunge Igunga leo

EasyFit

JF-Expert Member
Jul 4, 2011
1,269
1,082
MAHAKAMA KUU ya Kanda ya Tabora leo itaanza kusikiliza kesi ya kupinga matokeo yaliyompa ushindi Dk Peter Kafumu Mbunge wa Igunga kupitia Tiketi ya CCM katika uchaguzi mdogo uliofanyika mwishoni mwa mwaka jana.

Shauri hilo lilifunguliwa na mlalamikaji Joseph Kashindye aliyekuwa mgombea ubunge kupitia Tiketi ya Chadema dhidi ya Peter Kafumu, Mwanasheria Mkuu wa Serikali pamoja na msimamizi wa uchaguzi wa jimbo hilo.

Mahakama hiyo itaanza kusikiliza hoja za msingi zilizowasilishwa na pande zote ili kupata ufumbuzi wa uamuzi sahihi katika mahakama hiyo.

Hoja 15 ziliwasilishwa na wakili wa upande wa mlalamikaji Profesa Abdalla Safari ikiwamo anayopdai kwamba Waziri wa Ujenzi John Magufuli alifanya mkutano wa kampeni Kata ya Igulubi wilayani Igunga kutumia madaraka yake kuahidi ujenzi wa Daraja la Mbutu kama wananchi hao watampigia kura mgombea wa chama mapinduzi.

Pia Safari anadai waziri huyo aliwatisha wananchi wa kata hiyo kwamba wasipo ichagua CCM daraja hilo halitajengwa na kwamba pia aliwatisha wananchi hao kuwa wasipomchagua Dk Kafumu watashughulikiwa.

Profesa Safari alidai Baraza la Waislamu(Bakwata) Wilaya ya Igunga liliwakataza wasikipigie waumini wasiipigie kura Chadema na kwamba naye Rais mstaafu Benjamini Mkapa alitoa ahadi ya kugawa mahindi kwa wananchi wa Igunga siku mmoja kabla uchaguzi ili waichague CCM.

Jaji Mary Shangali anatarajia kusikiliza kesi hiyo na kwamba tayari mashahadi 80 wanatarajiwa kutoa ushahidi wao kwenye shauri hili.

Shangali alibainisha kuwa upande wa walalamikaji watakuwa na mashahidi wasiopungua 50 huku upande wa wajibu madai chini ya wakili Kamaliza Kayaga watakuwa na mashahidi 20 .

Miongoni mwa mashahidi ni mawaziri, baadhi ya wabunge na kwamba upande wa Serikali utakuwa na mashahidi 10.

Source: Mwananchi
 
Kazi ya tume ni kutangaza matokeo na suala na nani kahongwa nini na wakati gani hiyo ni kazi ya PCCB Na polisi kuzifanyia kazi wakati wa kampeni,na mfano ni Arumeru tuliona matukio yalivyokuwa na vyombo husika vilivyofanya kazi zake.
 
Hoja 15 ziliwasilishwa na wakili wa upande wa mlalamikaji Profesa Abdalla Safari ikiwamo anayopdai kwamba Waziri wa Ujenzi John Magufuli alifanya mkutano wa kampeni Kata ya Igulubi wilayani Igunga kutumia madaraka yake kuahidi ujenzi wa Daraja la Mbutu kama wananchi hao watampigia kura mgombea wa chama mapinduzi.

Pia Safari anadai waziri huyo aliwatisha wananchi wa kata hiyo kwamba wasipo ichagua CCM daraja hilo halitajengwa na kwamba pia aliwatisha wananchi hao kuwa wasipomchagua Dk Kafumu watashughulikiwa.

Profesa Safari alidai Baraza la Waislamu(Bakwata) Wilaya ya Igunga liliwakataza wasikipigie waumini wasiipigie kura Chadema na kwamba naye Rais mstaafu Benjamini Mkapa alitoa ahadi ya kugawa mahindi kwa wananchi wa Igunga siku mmoja kabla uchaguzi ili waichague CCM.

Source: Mwananchi

kama ni kweli wananchi waliambiwa kua hawatapata maendeleo kama hawatachagua ccm then tuko mahali pabaya...jamani maendeleo ya wananchi ni muhimu na haijali uko chama gani...huku tunakoelekea mh sina imani nako kabisaa:disapointed:
 
Mzee Mwanakijiji na Wana JF,
Naunga Hoja kuwa tuna Mfumo Mbovu wa Uchaguzi, ungetuambia mawazo na maoni yako nini kifanyike kwa hili suala maana linajirudia rudia kila mara, maana kuna wadau na viongozi wa Uchaguzi wanapitia humu.
Nawakilisha

Tuna mfumo mbovu sana wa uchaguzi! we really do!
 
kafumu nilishamuambia ubadhirifu walioufanya akiwa madini. yeye akasema ni mlokole namhukumu pasi nongwa nina uchungu kwa asiyehusika lakini leo anapelekwa mahakama aniambia, je yeye bado ni mlokole na uchuro wote wa ccm kwenye uchaguzi mdogo wa Igunga?
 
Tuna mfumo mbovu sana wa uchaguzi! we really do!

hivi mwanakijiji, uzi wako wa rais kuvunja sheria ya mapitio ya katiba ulimalizika vipi? jana niliona kwenye taarifa ya habari wakirudia picha za kuwaapisha wajumbe, nilipomwona mzungu, nikakumbuka uzi wako
 
Mzee Mwanakijiji na Wana JF,
Naunga Hoja kuwa tuna Mfumo Mbovu wa Uchaguzi, ungetuambia mawazo na maoni yako nini kifanyike kwa hili suala maana linajirudia rudia kila mara, maana kuna wadau na viongozi wa Uchaguzi wanapitia humu.
Nawakilisha

hii ya mfumo ni thread mkuu. Atahama mada
 
Kwa mfumo wa uchaguzi wa 'ki-ccm', kesi za namna hii hazitakaa kuisha.
Kuna hila, gilba na dhuruma nyingi sana zinafanyika wakati wa uchaguzi. Haya mambo yangetakiwa kushughulikiwa outright before uchaguzi na mgombea anakua disqualified. Lkn tatizo vyombo vya kuyashughulikia haya, e.g. Tume ya uchaguzi, PCCB, msimamizi wa uchaguzi au msajili wa vyama vya siasa, wote hawa wameweka mbele 'u-ccm'. Yani ni matatizo tu.
 
Rushwa ni kigezo cha kutengua matokeo. Sumbawanga ni mfano.

Kazi ya tume ni
kutangaza matokeo na suala na nani kahongwa nini na wakati gani hiyo ni
kazi ya PCCB Na polisi kuzifanyia kazi wakati wa kampeni,na mfano ni
Arumeru tuliona matukio yalivyokuwa na vyombo husika vilivyofanya kazi
zake.
 
Nimestuka kusoma kwamba kuna Mawaziri watasimama Kama watetezi/Mashahidi. Hii inaweza kuichafua serikali Kama utetezi wao utatupiliwa mbali katika maamuzi ya hukumu.
 
hii kesi nayo ni nzuri kwa upande wetu. Tuongeze na maombi tu ili dalali apotezwe leo
 
Ngoja nijitahidi kuwaletea updates kama ratiba zitakaa, Nataka pia nimsikie Prof.Safari kama mwanasheria makini, na Ustaadh aliyefunga vilimi-limi vyao juu ya Ukatoliki wa CHADEMA
 
Tuna mfumo mbovu sana wa uchaguzi! we really do!

sio mfumo wa uchaguzi tu mbovu nchi yetu kila mfumo mbovu ukianzia mfumo wa serikali na wizara zake mbovu, bunge mbovu, mahakama mbovu, polisi mbovu, muungano mbovu kila kitu cha hovyohovyo tu tunahitaji kujenga mfumo mpya kabisa chini ya chama kipya na sera mpya kabisa!!the sooner the better!!
 
MAHAKAMA KUU ya Kanda ya Tabora leo itaanza kusikiliza kesi ya kupinga matokeo yaliyompa ushindi Dk Peter Kafumu Mbunge wa Igunga kupitia Tiketi ya CCM katika uchaguzi mdogo uliofanyika mwishoni mwa mwaka jana.

Shauri hilo lilifunguliwa na mlalamikaji Joseph Kashindye aliyekuwa mgombea ubunge kupitia Tiketi ya Chadema dhidi ya Peter Kafumu, Mwanasheria Mkuu wa Serikali pamoja na msimamizi wa uchaguzi wa jimbo hilo.

Mahakama hiyo itaanza kusikiliza hoja za msingi zilizowasilishwa na pande zote ili kupata ufumbuzi wa uamuzi sahihi katika mahakama hiyo.

Hoja 15 ziliwasilishwa na wakili wa upande wa mlalamikaji Profesa Abdalla Safari ikiwamo anayopdai kwamba Waziri wa Ujenzi John Magufuli alifanya mkutano wa kampeni Kata ya Igulubi wilayani Igunga kutumia madaraka yake kuahidi ujenzi wa Daraja la Mbutu kama wananchi hao watampigia kura mgombea wa chama mapinduzi.

Pia Safari anadai waziri huyo aliwatisha wananchi wa kata hiyo kwamba wasipo ichagua CCM daraja hilo halitajengwa na kwamba pia aliwatisha wananchi hao kuwa wasipomchagua Dk Kafumu watashughulikiwa.

Profesa Safari alidai Baraza la Waislamu(Bakwata) Wilaya ya Igunga liliwakataza wasikipigie waumini wasiipigie kura Chadema na kwamba naye Rais mstaafu Benjamini Mkapa alitoa ahadi ya kugawa mahindi kwa wananchi wa Igunga siku mmoja kabla uchaguzi ili waichague CCM.

Jaji Mary Shangali anatarajia kusikiliza kesi hiyo na kwamba tayari mashahadi 80 wanatarajiwa kutoa ushahidi wao kwenye shauri hili.

Shangali alibainisha kuwa upande wa walalamikaji watakuwa na mashahidi wasiopungua 50 huku upande wa wajibu madai chini ya wakili Kamaliza Kayaga watakuwa na mashahidi 20 .

Miongoni mwa mashahidi ni mawaziri, baadhi ya wabunge na kwamba upande wa Serikali utakuwa na mashahidi 10.

Source: Mwananchi

Huu ni Ushahidi wa Viongozi wa dini kutumiwa kisiasa kwenye kampeni. Ushahidi huu una uzito sana katika sheria ya uchaguzi.
 
Last edited by a moderator:
Back
Top Bottom