Kesi ya kupinga matokeo ya Godless Lema

kifungu namba 108 kimeorodhesha ni madai yapi yana weza kufanya matokeo yaka batilishwa lakini si kashiwa..
 
nimechelewa kufika lakini kinachobishaniwa sasa ni juu ya maneno aliyoyatumia lema kwenye kampeni kuwa yalikuwa yana mkashifu mgombea wa ccm..wanaulizwa yaliwaathiri vipi waliofungua kesi

Maneno yepi hayo, unaweza kutukumbusha?
 
Ile kesi ya kupinga matokea ya ubunge wa Arusha mjini iliyofunguliwa na Musa mkangaa na wenzanke zidi ya kamanda Godbless Lema, mkurungezi wa manispaa ya Arusha na mwanasheria itaanza kuunguruma leo...Katika matokeo ya uchaguzi mkuu uliofanyika Oktoba, mwaka jana, Lema, alimbwaga kwa kura nyingi aliyekuwa Waziri wa Nchi, Ofisi ya Makamu wa Rais (Mazingira), Dk. Batilda Burian. Lema alipata kura 56,196 na Dk. Burian aliambulia kura 37.460......nitawajuza zaidi kinachoendelea
huyu mama kwanza alimdharau Mh. Zitto!! Ningekuwa Zitto ningeweza kumkumbusha!!
 
mwanasheria wa upande wa utetezi anasema madai ya washitaki hayajaonyeshwa bayana madai yao na ni swala ambalo siyo la kiufundi walipaswa kuaanisha bayana ili aweze kujiandaa tofauti na ilivyo sasa dr kuwa ni muislam..
 
kesi imehailishwa mpaka kesho lakini kwa upeo wangu mdogo wadai walikuwa wamebanwa sana..
 
Mimi si kama Crashwise hana shughuli nyingine zaidi ya CDM na Lema.

Kitakachojadiliwa mahakamani hakika nitakijua muda huu jamaa zangu wapo ndani nadhani unajua taratibu za kimahakama lazima simu zote zizimwe.Habari atakazoleta Crashwise lazima niziverify upo mwita.
Mnafiki Ngongo nina kazi ninayoitegemea tofauti na hiyo uliyo niajiri juzi ya ukatibu wa lema ndiyo maana nikakwambia ulete familia yako nikulelee hahahahahahahaha.....kuhusu kuzima simu siyo lazima uzime mbona mimi huripoti kutumia simu yangu huku nikiwa mahakamani.....
halafu ngongo hawa jamaa zenu waliofungua kesi hamkukaa nao na kuwashauri maana hiyo kesi hata ningekuwa mimi sijui sheria ningeshinda...
 
Mkuu wangu umeshasahau kesi ya madiwani ulivyowahukumu kabla ya mahakama haijatoa hukumu.Kwanza ulishawabatiza wasaliti ebu jiweke wewe ndiyo hakimu madiwani wangetendewa haki ?.
kukudokeza tu baadhi ya madiwa waliofukuzwa CHADEMA na wafahamu vizuri sana hata nikitaka kujua jana wamekulala nini naweza ndiyo maana sikukurupuka kuwaandama baada ya hili sekeseke kwasababu nilikuwa sijapata ukweli na huwa si mtu wa kumtuhumu mtu bila ushahidi lakini kwataarifa yako tu Malla na Bayo wamenunuliwa na CCM hata hiyo kesi iliyofunguliwa ni kwa matakwa ya CCM na kuna mengi yana sukwa juu ya Godbless Lema...sasa ulitaka niwaitaje hebu nipe jina zuri la kuwaita...
 
Ile kesi ya kupinga matokea ya ubunge wa Arusha mjini iliyofunguliwa na Musa mkangaa na wenzanke zidi ya kamanda Godbless Lema, mkurungezi wa manispaa ya Arusha na mwanasheria itaanza kuunguruma leo...Katika matokeo ya uchaguzi mkuu uliofanyika Oktoba, mwaka jana, Lema, alimbwaga kwa kura nyingi aliyekuwa Waziri wa Nchi, Ofisi ya Makamu wa Rais (Mazingira), Dk. Batilda Burian. Lema alipata kura 56,196 na Dk. Burian aliambulia kura 37.460......nitawajuza zaidi kinachoendelea
<br /> <br /
 
Ile kesi ya kupinga matokea ya ubunge wa Arusha mjini iliyofunguliwa na Musa mkangaa na wenzanke zidi ya kamanda Godbless Lema, mkurungezi wa manispaa ya Arusha na mwanasheria itaanza kuunguruma leo...Katika matokeo ya uchaguzi mkuu uliofanyika Oktoba, mwaka jana, Lema, alimbwaga kwa kura nyingi aliyekuwa Waziri wa Nchi, Ofisi ya Makamu wa Rais (Mazingira), Dk. Batilda Burian. Lema alipata kura 56,196 na Dk. Burian aliambulia kura 37.460......nitawajuza zaidi kinachoendelea
<br /> <br / ¥ br+sidhani kama watashinda kwa maana cha msingi wanachodai katika hii kesi ni maneno yaliyotumika kwenye kampeni.
 
bot_tabimg.gif




KESI ya kupinga ushindi wa Mbunge wa Arusha Mjini kupitia tiketi ya Chadema, Godbless Lema, jana ilianza
kunguruma katika Mahakama Kuu ya Tanzania, Kanda ya Arusha kwa mawakili wa utetezi kuomba
ifutiliwe mbali kwa madai kuwa walalamikaji hawana haki kisheria kupinga matokeo hayo.

Kesi hiyo namba 13 ya mwaka 2010, imefunguliwa na wanachama watatu wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) wanaodai kuwa Lema alitoa lugha za kashfa na ubaguzi wa kidini na kijinsia dhidi ya aliyekuwa mgombea wa chama chao, Dk Batilda Burian.

Walalamikaji hao wanadai kuwa lugha hizo ziliathiri matokeo ya uchaguzi katika Jimbo la Arusha Mjini.Wanaompinga Lema katika kesi hiyo ni, Mussa Mkanga, Agnes Mollel na Happy Kivuyo ambao kwa pamoja wanawakilishwa na mawakili Alute Mughwai na Modest Akida.

Wanadai kuwa katika siku na
sehemu mbalimbali, Lema alidai kuwa Dk Burian, ameolewa Zanzibar na kwamba yeye na mumewe angekwenda kuishi visiwani humo baada ya uchaguzi.

Wanadai kuwa Lema pia alitoa madai kuwa mgombe huyo wa CCM hakuwa mwaminifu na kwamba hiyo inadhihirishwa na kitendo cha kazaa na mwanamume mwingine.

Mawakili wa utetezi Method Kimomogoro, anayemwakilisha Lema,ameweka pingamizi tatu na kumuomba Jaji Aloyce Mujuluzi kulitupilia mbali kesi hiyo kwa madai kuwa walalamikaji wameshindwa kubainisha wanavyohusika na maneno yanayodaiwa kutamkwa na mteja wake dhidi ya Dk Burian.

“Wadai hawana sababu za kisheria za kulalamika kwa sababu maneno wanayodai kutolewa kwenye mikutano ya hadhara (kama yalitolewa),yalilengwa kwa Dk Burian binafsi na si wao. Hawajaeleza madhara waliyopata wao kama wapiga kura,” alisema wakili Kimomogoro.

Hoja hiyo ilimfanya Jaji Mujuluzi kumuuliza wakili huyo, “ina maana unalenga kusema pilipili usizokula zakuwashia nini,”

Kwa upande wake wakili Kimomogoro alijibu kuwa ndiyo alikuwa na maana hiyo.Alitaja kifungu cha 111 (1) ya sheria ya uchaguzi inayoelekeza mdai au mlalamikaji katika kesi ya kupinga matokeo ya uchaguzi, kubainisha wazi makosa ya kisheria yaliyotendeka na madhara aliyopata, jambo ambalo alidai kuwa
walalamikaji wameshindwa kufanya kupitia katika hati yao ya madai.

Wakili huyo alisema kisheria wadai hawana haki kulamikia taratibu za kampeni kulingana na sheria ya maadili ya uchaguzi iliyosainiwa na vyama vyote vilivyoshiriki uchaguzi mkuu wa Oktoba 31 mwaka jana.

Alidai kuwa sheria hiyo inatoa nafasi kwa chama au mgombea pekee kuwasilisha malalamiko katika
kamati ya uchaguzi ngazi husika ndani ya saa 48 tangu tukio lilipotokea.

Kwa upande wao, mawakili wa serikali wanaomwakilisha Mwanasheria Mkuu wa Serikali ambaye ni mdaiwa wa pili katika shauri hilo, Timon Vitalis na Juma Masanja, waliunga mkono hoja za Kimomogoro na kwamba ushindi wa
Lema, ulionyesha matakwa na maslahi ya umma hivyo wadai lazima waonyeshe yamewaathiri vipi.

“Matokeo ya uchaguzi huonyesha matakwa ya walio wengi. Ili matokeo ya uchaguzi yatenguliwe, lazima wadai waonyeshe wameathirika vipi na hayo
matokeo ambayo ni maslahi ya umma. Hati ya madai inaonyesha maneno yalitamkwa dhidi ya Dk Burian na si wao,” alisema wakili Vitalis akiomba shauri hilo litupwe.

Alisema kifungu cha 111 cha sheria ya uchaguzi kinatoa haki kwa mpiga kura kupinga matokeo, lakini lazima azingatie sababu zinazoweza kusababisha matokeo kutenguliwa zilizoanishwa katika kifungu cha 108 cha sheria na kwamba hoja ya Dk Burian kuzaa na mwanamume mwingine haiangukii katika kifungu hicho bali inastahili kushughulikiwa kama kashfa binafsi.

Baada ya upende wa utetezi kuwasilisha hoja za pingamizi, wakili wa wadai, Mugwai aliomba mahakama iwape muda wa kupitia na kujibu hoja, ombi ambalo lilikubaliwa na Jaji Mujuluzi.

Baadaye, jaji huyo aliahirisha kesi hiyo hadi leo atakapoendela.

soure mwananchi
 
mussa mkangaa na wenzake wana wasilisha kadi ya kupigia kura kuzibitisha kuwa ni wapiga kura kweli
 
wakili wa ccm anajibu hoja ya kwamba kesi hii ni binafsi..
 
jaji anasema sheria zetu zimejichongo kwenye baadhi ya mambo ambayo mpiga kura na si kwa ujumla vinginevyo itakuwa vurugu, wakili wa ccm alikuwa anajaribu kumshawishi jaji atumie sheria za india ambayo mpiga kura ana haki ya kufungua kesi juu ya mgombea kwa ujumla tofauti na ilivyo kwa sheria yetu..
 
wakili wa ccm anasema kunakipengele hakijui baada ya kuambiwa afafnue kipengele alichokuwa anajaribu kukijengea hoja ni juu ya kupinga kuitwa kesi hii ni ya binafsi..
 
Back
Top Bottom