Kesi ya Jerry Muro

I got to know, kwa hiyo jamaa alikuwa ana kesi mbili??!! Na mwananchi nao, wameiandikaje hii habari wakati wanajua sisi hatuijui hiyo kesi nyingine?

Wanataka kuuza magazeti, si unajua tena njaa kitu kibaya?
 
kumbe mshikaji utapeli ni fani yake..................

Ha ha ha ha, hata mimi nashangaa. Sikujua kabisa kama alikuwa ana kesi mbili mahakamani. Napata shaka kwamba huyu bwana si mwaminifu kama ambavyo wengi wetu tumekuwa tukimdhania.
 
Ndio tatizo la magazeti, yaani hawana mbinu nyingine ya kuuza magazeti yao zaidi ya hii ya kuwazuga watu kwa kichwa cha habari kingine.
njaa kwake tumboni ikishavamia kichwani ni hatali tupu, mwanaume anaweza kuwa shoga, mwandishi akawa mwongo, nk
 
Ha ha ha ha, hata mimi nashangaa. Sikujua kabisa kama alikuwa ana kesi mbili mahakamani. Napata shaka kwamba huyu bwana si mwaminifu kama ambavyo wengi wetu tumekuwa tukimdhania.

tusimhukumu kwa maneno ya magazeti. tuna uhakika gani kama gazeti hilo limeandika habari sahihi. time will tell. lets just wait and see!
 
Kumbe ile Kesi ya Kova ya utapeli/rushwa ya 10m/- pamoja na mambo ya kumiliki pingu bado iko palepale?

Toto confusion, toto distruction. Waandishi wetu bana!! hata hiyo habari yenyewe kwenye Mwananchi haieleweki vizuri iwapo hiyo kesi ya Utapeli imefutwa au imeairishwa...haieleweki iwapo mwandishi amechanganya madesa katika kuripoti au lah hitimisho lakie lina utata....Hawa watu waandishi tabu tupu!
..........................
Mahakama yamfutia Muro kesi ya utapeli

Send to a friend Friday, 09 July 2010 20:58 0diggsdigg

Ummy Muya

jerrymurro.jpg

Jerry Muro

KESI inayomkabili mtangazaji wa Shirika la Utangazaji Tanzania (TBC1), Jerry Muro jana imefutwa na Mahakama ya Hakimu Mkazi Kinodoni baada ya mlalamikaji kuamua kumsamehe.

Mlalamikaji katika shauri hilo, alikuwa Mkurugenzi Mtendaji wa Kampuni ya Boneste General Enterprisess Ltd, Eduado Chamuhene ambaye alimshtaki katika mahakama hiyo, baada ya kutomalizia kumlipa fedha alizomkopa.

Wakati hakimu akijianda kuendelea na kesi hiyo, mlalamikaji alinyoosha mkono na kuomba kuliondoa shauri hilo, mahakamani hapo.

“Mheshimiwa huyu kijana ni kama mtoto wangu ninamuonea huruma nimeamua kumsamehe, naomba uridhie uamuzi wangu,”alisema Chamuhene. Hakimu Fimbo aliridhia ombo hilo, na kulifuta shauri hilo.

Katika shauri hilo, ilidaiwa na mlalamikaji mbele ya Hakimu Sundi Fimbo kuwa Februari 26 mwaka 2008, Jerry akiwa mfanyakazi wa ITV alifika nyumbani kwake eneo la Mabibo sahara akiwa na msichana mmoja aliyemtambulisha kama mke wake akimuomba amkopeshe Sh 1.5 milioni akatoe gari lake bandarini.

Chamuhene alisema alimpatia Jerry hundi ya Sh 1.5 milioni na kukubaliana kurudisha fedha hizo baada ya siku 60, lakini Jerry badala ya kukamilisha deni hilo, alilipa Sh milioni moja na kiasi kilichobaki hakukilipa.

Aliieleza mahakama kuwa baada ya muda kupita aliamua kumuandikia barua na kumpelekea ofisini kwake wakati huo,akiwa ITV na ilisainiwa katika kitabu maalum cha kupokeea barua, lakini hakutoa sababu yeyote na hakufanya mawasiliano ya aina yeyote.

Kabla Hakimu hajaahirisha shauri hilo, mshtakiwa ambaye aliwasili mahakamani hapo na kumuomba Hakimu ampatie muongozo wa kesi kutokana na yeye kutofahamu taratibu za mahakama ili mpatie wakili wake.

Mahakama yamfutia Muro kesi ya utapeli
 
sasa hapo nini hakieleweki?na sisi wasomaji tuwe makini taarifa inaeleweka sema wengi wetu tunasoma vichwa vya habari tu.
 
Toto confusion, toto distruction. Waandishi wetu bana!! hata hiyo habari yenyewe kwenye Mwananchi haieleweki vizuri iwapo hiyo kesi ya Utapeli imefutwa au imeairishwa...haieleweki iwapo mwandishi amechanganya madesa katika kuripoti au lah hitimisho lakie lina utata....Hawa watu waandishi tabu tupu!
..........................
Mahakama yamfutia Muro kesi ya utapeli

Send to a friend Friday, 09 July 2010 20:58 0diggsdigg

Ummy Muya

jerrymurro.jpg

Jerry Muro

KESI inayomkabili mtangazaji wa Shirika la Utangazaji Tanzania (TBC1), Jerry Muro jana imefutwa na Mahakama ya Hakimu Mkazi Kinodoni baada ya mlalamikaji kuamua kumsamehe.

Mlalamikaji katika shauri hilo, alikuwa Mkurugenzi Mtendaji wa Kampuni ya Boneste General Enterprisess Ltd, Eduado Chamuhene ambaye alimshtaki katika mahakama hiyo, baada ya kutomalizia kumlipa fedha alizomkopa.

Wakati hakimu akijianda kuendelea na kesi hiyo, mlalamikaji alinyoosha mkono na kuomba kuliondoa shauri hilo, mahakamani hapo.

“Mheshimiwa huyu kijana ni kama mtoto wangu ninamuonea huruma nimeamua kumsamehe, naomba uridhie uamuzi wangu,”alisema Chamuhene. Hakimu Fimbo aliridhia ombo hilo, na kulifuta shauri hilo.

Katika shauri hilo, ilidaiwa na mlalamikaji mbele ya Hakimu Sundi Fimbo kuwa Februari 26 mwaka 2008, Jerry akiwa mfanyakazi wa ITV alifika nyumbani kwake eneo la Mabibo sahara akiwa na msichana mmoja aliyemtambulisha kama mke wake akimuomba amkopeshe Sh 1.5 milioni akatoe gari lake bandarini.

Chamuhene alisema alimpatia Jerry hundi ya Sh 1.5 milioni na kukubaliana kurudisha fedha hizo baada ya siku 60, lakini Jerry badala ya kukamilisha deni hilo, alilipa Sh milioni moja na kiasi kilichobaki hakukilipa.

Aliieleza mahakama kuwa baada ya muda kupita aliamua kumuandikia barua na kumpelekea ofisini kwake wakati huo,akiwa ITV na ilisainiwa katika kitabu maalum cha kupokeea barua, lakini hakutoa sababu yeyote na hakufanya mawasiliano ya aina yeyote.

Kabla Hakimu hajaahirisha shauri hilo, mshtakiwa ambaye aliwasili mahakamani hapo na kumuomba Hakimu ampatie muongozo wa kesi kutokana na yeye kutofahamu taratibu za mahakama ili mpatie wakili wake.

Mahakama yamfutia Muro kesi ya utapeli

mie macho yake tu... :A S tongue:
 
Jambo usilolijua ni sawa na usiku wa giza.

Mna uhuru wa kusema, kuandika mnayoyataka, lakini kaeni kwanza mtafakari kwa kina... someni katikati ya mistari, mtaujua ukweli.

Siwezi kusema mengi kwa kuwa Jerry ninamfahamu; ni swahiba yangu na pia ni mwanataaluma mwenzangu.

Wewe unayedai kwamba Jerry ni "mtu wa system", una ushahidi wowote? Au unasema tu kwa kujifurahisha? Kama ni kujifurahisha, sawa, lakini ukitakiwa kuthibitisha usianze kujiuma-uma ulimi na kuwa na kigu-gu-mi-zi!

./Mwana wa Haki
 
Kesi ya Pingu/Utapeli haijafutwa. Leo ilitajwa mahakamani na ikaahirishwa kwa sababu mmoja wa washitakiwa hakuwepo mahakamani kutokana na msiba wa Bibi yake, kwa mujibu wa taarifa ya habari ya TBC saa 2 usiku. Iliyofutwa ilikuwa nyingine.
 
Kuwa na kesi mbili mahakamani tayari inaonyesha J murro ana usanii fulani. Naamni wamemuhurumia kwenye hii kesi ili wamtaight kwenye ile nyingine.

Naamin kabisa J Muro alijisahau akaanza usanii. Ajiandae tu kula mvua. yeye alijua habari zake zinafuatilia maisha ya watu halafu hauwi makini katika mambo yako.
 
Wage akiri kumpa rushwa Jerry Murro


na Happiness Katabazi


amka2.gif
SHAHIDI wa pili upande wa Jamhuri katika kesi ya kuomba rushwa ya sh milioni 10 inayomkabili aliyekuwa Mtangazaji wa Shirika la Utangazaji la (TBC1) Jerry Murro, na wenzake Michael Wage amekiri kutoa rushwa ya sh milioni moja baada ya kutishiwa bastola na pingu.
Wage alitoa maelezo hayo jana katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu mbele ya Hakimu Mkazi Gabriel Mirumbe wakati akiongozwa na Naibu Mkurugenzi wa Mashtaka nchini Boniface Stanslaus.
Alidai kuwa alilazimika kutoa rushwa hiyo kwa sababu alitishwa na Murro na mshtakiwa wa pili Kapama aliyejitambulisha kuwa ni Kaimu Mkurugenzi wa PCCB na mshtakiwa wa tatu Deo Mgassa alijitambulisha kuwa ni msaidizi wa mkurugenzi huyo.
Shahidi huyo ambaye alikuwa mhasibu wa Halmashauri ya Wilaya ya Bagamoyo kabla ya hajasimamishwa kazi na Waziri Mkuu Mizengo Pinda, Januari mwaka jana, alidai kuwa washtakiwa hao wote watatu Januari 31 mwaka jana, katika Hoteli ya Sea Cliff walimtaka awapatie sh milioni 10 ama sivyo wangembambikia kesi kama alivyobambikiwa aliyekuwa Mkurugenzi wa Utumishi na Utawala wa Benki Kuu, Amatus Liyumba, kwa kumwambukiza maradhi mpenzi wa rafiki wa Kapama ndiyo maana akabambikiziwa kesi iliyomfanya ahukumiwe kwenda jela miaka miwili.
Wage aliieleza Mahakama kuwa Januari 28 mwaka jana akiwa nyumbani kwake Bagamoyo alipokea simu kutoka kwa mtu aliyejitambulisha kuwa mtangazaji wa TBC1 na hakuwa hakimfahamu, akimtaka kesho yake aje Dar es Salaam kwa ajili ya mahojiano kwani amepata taarifa kuwa anakabiliwa na tuhuma za ufisadi katika Halmashauri ya Bagamoyo.
Katika hilo Wage alieleza kuwa alikubaliana na ombi hilo na Januari 29 mwaka jana, saa tano asubuhi alifikia katika mgahawa wa Califonia ulioko jijini hapa akiwa na dereva wake.
Alisema akiwa njiani alimpigia simu Murro ili aje aungane naye na baada ya dakika chache Murro aliwasili katika mgahawa huo akiwa na gari ndogo na akamweleza watafute meza nyingine ili wakae mbali na dereva wake na walipohamia kwenye meza nyingine ndipo Murro alipoanza kumueleza tuhuma za ufisadi zinazomkabili na kwamba anataka kuzitangaza kwenye kipindi cha Usiku wa Habari kinachorushwa na TBC1.
“Baada ya Murro kunieleza tuhuma hizo akaniambia mahojiano kamili yangefanyika katika Hoteli ya Sea Cliff kwani huko ndiko walikokuwa mabosi wake na kunitaka nimwache dereva wangu kwenye mgahawa huo nikapande gari lake twende nae Sea Cliff na nilifanya kama alivyonielekeza nikapanda na tulipokuwa njiani akampigia simu mtu akawa anazungumza naye na akanitaja jina langu… alivyokata simu nikamuuliza ni kwa nini alikuwa akitaja jina langu akasema alikuwa akizungumza na Kaimu Mkurugenzi wa PCCB (Kapama) naye pia atanihoji.
“Kitu kingine wakati nilipokuwa ndani ya gari hilo tukielekea Sea Cliff, Murro aliniambia yeye ni ofisa wa jeshi na ana nyota tatu na amechukua mafunzo nchini Marekani na Afrika Kusini na ana madaraka ya kunikamata… na baada ya hapo alifungua dashibodi ya gari lake akatoa pingu akaniambia nikimletea vurugu atanifunga na pingu na kisha akanionyeshea bastola pia akaniambia nikifanya vurugu atanifyatulia risasi ili kunidhibiti,” alieleza.
Wage aliendelea kueleza kuwa walipofika tu Hoteli ya Sea Cliff walipokelewa na mtu aliyejitambulisha kuwa ni Kaimu Mkurugenzi wa PCCB, anaitwa Mussa ambapo hata hivyo Wage alimtambua mtu huyo mahakamani kuwa ni Mugassa na akaongeza mtu mwingine aliyejitambulisha kwa jina la Dokta ambaye Wage jana alimtambua mahakamani kuwa ni Kapama na kuongeza kuwa baada ya hapo mahojiano yakaanza na Dokta akaanza kumueleza kuwa yeye ni fisadi mkubwa na kwamba kama alihitaji msaada wao angesema mapema ili mahojiano yao yasiweze kurushwa kwenye kipindi cha Usiku wa Habari cha TBC1.
“Niliwajibu mimi siyo fisadi; ndipo yule Dokta (mshtakiwa wa pili) akaniambia kuwa hata Liyumba alifungwa jela kwa kuonewa kwani ile kesi ya matumuzi mabaya ya ofisi ya umma, alibambikiziwa kwa kuwa alikuwa akitembea na mpenzi wa rafiki yake anayefanya kazi BoT akamwambukiza maradhi… nilipokea taarifa hiyo kwa mshtuko mkubwa na nikaona wanaweza kunibambika kesi watu hao na siku hiyo nilikuwa na sh milioni moja mfukoni ikabidi nimpatie kiasi hicho cha fedha Kaimu Mkurugenzi wa PCCB (Kapama), mshtakiwa wa pili, ndani ya gari na Murro alikuwa nje ya gari na kuwaahidi kesho yake Januari 31 mwaka jana ningewaletea sh milioni tisa zilizokuwa zimebaki.
“Baada ya kumaliza kuwapatia sh milioni moja, niliingia kwenye gari la Murro akaenda kunishusha mgahawa wa Best Bite na tutakubaliana kesho yake tukutane kwenye mgahawa wa City Garden ulioko mtaa wa Mkwepu… Nikapanda kwenye gari langu nikaenda nyumbani kwangu Bagamoyo nikawaeleza ndugu zangu kuhusu tukio la mimi kutishiwa bastora na kuombwa rushwa; wakaniambia nikatoe taarifa polisi….na kweli Januari 31 mwaka jana, nilivyokuja Dar es Salaam nilifikia moja kwa moja kituo kikuu cha Polisi Kati huku mfukoni nikiwa na sh milioni tisa,” alidai Wage.
Alisema mara baada ya kutoa taarifa hizo polisi wakamtaka ampigie simu Murro na amweleze kuwa tayari ameishafika kwenye mgahawa wa City Garden.
Wage alieleza kuwa alifanya hivyo na baada ya dakika chache Murro aliwasili kwenye mgahawa huo lakini alivyomuona Wage ameambatana na watu wengine watatu alishtuka na polisi waliwahi kuzuia gari lake lisitoke katika viwanja vya mgahawa huo na askari kanzu hao walimwamuru aendeshe gari lake na kulipeleka kituo cha polisi Kati na Murro alitii amri hiyo na wote walifika kituoni hapo.
Alisema Murro alipoulizwa kama alikuwa akimfahamu Wage alikana kumfahamu na polisi hao walipopekuwa gari la Murro walikuta bastola, pingu na miwani ya kusomea ambayo Wage alidai ni yake na aliisahau jana yake wakati alipopanda katika gari hilo wakati anapelekwa Sea Cliff.
Vitu hivyo vyote pingu, bastola na miwani ilipokelewa mahakamani hapo kama utambulisho. Kwa upande wake wakili wa Murro, Richard Rweyongeza, na Majura Magafu, anayemtetea Kapama na Muggasa akimhoji shahidi huyo alidai kuwa shahidi huyo haoni kwamba Murro alikuwa akitangaza habari za hatari hatari za kuligusa jeshi la polisi na alikuwa akitaka kurusha tuhuma za ufisadi zinazomkabili Wage ndiyo maana alishirikiana na polisi kumbambikizia kesi mteja wake, hoja hiyo ilipingwa vikali na shahidi huyo. Leo shahidi wa tatu atahojiwa.
 
Shahidi aeleza Muro alivyomuomba rushwa


Na Zamzam Abdul

SHAHIDI wa tatu upande wa mashitaka Bw. Michael Wage ametoa ushahidi wake katika kesi ya kudai rushwa ya sh. milioni kumi kinayomkabili
mtangazaji wa TBC, Bw. Jerry Muro.

Akitoa ushahidi wake Bw. Wage alisema Januari 28 mwaka 2010 jioni akiwa nyumbani kwake alipigiwa simu na mtu ambaya alijitambulisha kuwa yeye ni Jerry Muro, mtangazaji wa TBC.

Alinitaka Januari 29 mwaka 2010 nifike Dar es Salaam kwa ajili ya mahojiano ili aweke sawa taarifa alizonazo kuhusu mimi, za ufisadi na ubadhilifu wa mali za serikali.

"Siku hiyo nilitoka Bagamoyo kuja Dar es Salaam ambapo aliniambia tukutane Calfonia Restaurant saa 5:00," alisema Bw. Wage.

Alisema alimpigia simu Bw. Muro kumjulisha kwamba tayari ameshafika kwenye eneo hilo, naye akaja akiwa na gari yake ndogo aina ya saloon.

Alikuja mpaka nilipokuwa nimekaa mimi pamoja na dereva wangu ambapo alinitaka tuongee pembeni katika meza iliyofuata ili dereva wangu asijue nini anataka tuongee.

"Tulihama na kuingia ndani, na ndipo aliniambia kuwa nakabiliwa na tuhuma za ufisadi na ubadhilifu wa fedha na anaandaa kipindi cha kueleza tuhuma na biashara zangu katika kipindi cha usiku wa habari," alisema Bw. Wage.

Alinieleza mahojiano hayo yatafanyika katika Hotel ya Sea Cliff ambako yuko bosi wake wanamsubiri na kutaka nimuache dereva wangu ili tupande gari lake kuelekea huko.

"Tukiwa njiani alimpigia mtu simu katika maongezi yao alinitaja jina langu na nikamuuliza huyo ni nani akanijibu Mkurugenzi wa PCCB, naye anataka kuonana na mimi kabla sijapelekwa mahakamani," alisema.

Bw. Wage anaeleza kuwa wakiwa wanaendelea na safari, Bw. Murro alimwambia yeye ni Ofisa wa Jeshi na ana nyota tatu amesoma Uingeraza na Marekani na ana uwezo wa kumkamata.

"Akafungua 'dash board' akatoa pingu akaniambia nikileta mchezo atanifunga na hizo pingu baada ya hapo akatoa tena bastola na kuniambia kama pingu zitashindikana angenipiga risasi.

"Baada ya hapo tulifika Sea Cliff tulipokewa na mwanaume aliyejitambulisha kwa jina la Mgassa, kuwa yeye ni Mkurugenzi wa PCCB kwa hiyo jumla tukawa watatu tukaingia hotelini hapo.

Baada ya muda mfupi akaingia mtu mwingine alijitambulisha kama Kaimu Mkurugenzi wa PCCB, anaitwa Edmund Kapama.

"Ndipo Bw. Muro aliniambia kuwa mimi ni fisadi, hivyo anaandaa kipindi kwa ajili yangu na kama nahitaji msaada niseme. Niliwajibu mimi sio fisadi na sijawahi kuiba fedha yeyote kutoka serikalini.

"Msaada wenyewe waliniambia nitoe sh. milioni 10 niliwajibu pale sikuwa nayo, hivyo nikaomba niwapatie kesho yake ndipo waliniambia nionane na mmoja wapo akiwemo Muro," alisema.

Vitu alivyokamatwa navyo mshtakiwa huyo, bastola na pingu, vilifikishwa mahakamani hapo kama utambulisho.

Katika kesi hiyo inadaiwa kuwa Januari 29, mwaka jana jijini Dar es Salaam, Bw. Murro na wenzake walikula njama ya kuomba rushwa ya sh milioni 10 kutoka kwa Bw. Wage ambapo Bw. Kapama na Mgassa walijifanya ni maofisa wa Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (TAKUKURU).
 
Hii kesi ni ya kubambikiziwa na huyu shahidi ushahidi wake unagongana......................Haiwezekani Murro ajitambulishe ni afisa wa TBC1 halafu tena ajigeuke utambulisho huo awe afisa wa Takukuru......................
Katika hilo Wage alieleza kuwa alikubaliana na ombi hilo na Januari 29 mwaka jana, saa tano asubuhi alifikia katika mgahawa wa Califonia ulioko jijini hapa akiwa na dereva wake.
Alisema akiwa njiani alimpigia simu Murro ili aje aungane naye na baada ya dakika chache Murro aliwasili katika mgahawa huo akiwa na gari ndogo na akamweleza watafute meza nyingine ili wakae mbali na dereva wake na walipohamia kwenye meza nyingine ndipo Murro alipoanza kumueleza tuhuma za ufisadi zinazomkabili na kwamba anataka kuzitangaza kwenye kipindi cha Usiku wa Habari kinachorushwa na TBC1.
"Baada ya Murro kunieleza tuhuma hizo akaniambia mahojiano kamili yangefanyika katika Hoteli ya Sea Cliff kwani huko ndiko walikokuwa mabosi wake na kunitaka nimwache dereva wangu kwenye mgahawa huo nikapande gari lake twende nae Sea Cliff na nilifanya kama alivyonielekeza nikapanda na tulipokuwa njiani akampigia simu mtu akawa anazungumza naye na akanitaja jina langu… alivyokata simu nikamuuliza ni kwa nini alikuwa akitaja jina langu akasema alikuwa akizungumza na Kaimu Mkurugenzi wa PCCB (Kapama) naye pia atanihoji.
"Kitu kingine wakati nilipokuwa ndani ya gari hilo tukielekea Sea Cliff, Murro aliniambia yeye ni ofisa wa jeshi na ana nyota tatu na amechukua mafunzo nchini Marekani na Afrika Kusini na ana madaraka ya kunikamata… na baada ya hapo alifungua dashibodi ya gari lake akatoa pingu akaniambia nikimletea vurugu atanifunga na pingu na kisha akanionyeshea bastola pia akaniambia nikifanya vurugu atanifyatulia risasi ili kunidhibiti," alieleza.
 
Tatizo kwa Murro ni kujitoa kwenye hisia ya kuwa kushirikiana na watu wasiokuwa wafanyakazi wa TBC1 katika kufanya shughuli ya TBC1 kunaashiria nia ya kudai rushwa........................ni hoja ambayo Murro itamsumbua sana na asipokuwa makini ndiyo itakayomtia hatiani na kumsababishia maumivu ya kifungo kirefu................
 
Polisi waliingilia kazi za Takukuru za kuchunguza rushwa na hili laweza kuwa la msaada mkubwa kwa Murro kama atalijengea hoja vizuri.....polisi walipaswa kuliwakilisha suala hili Takukuru na kwa kutofanya hivyo..............dai la Murro kuwa polisi wamemtumia mtuhumu ili kumkomoa kutokana na kuitekeleza kazi yake vyema ambako kunawakwaruza polisi na hivyo kunuia kumbambikizia kesi linaweza kuwa hoja ya kisheria ya kumtoa kwenye hili sakata....................

It all boils down to whom will the Hon. Magistrate believe..........................It is a criminal case of one man against three...........Who is more credible between the two sides?............
 

Jerry Muro adaiwa kutishia kuua


Imeandikwa na Mwandishi Wetu; Tarehe: 25th January 2011 @ 08:27
ALIYEKUWA Mtunza Hazina wa Halmashauri ya Wilaya ya Bagamoyo mkoa wa Pwani, Michael Wage ameeleza mahakamani alivyotishwa na kutakiwa kutoa rushwa ya Sh milioni 10 na aliyekuwa mtangazaji wa Shirika la Utangazaji Tanzania (TBC), Jerry Muro na wenzake.

Wage ambaye ni shahidi wa tatu katika kesi ya kuomba na kutaka kupokea rushwa inayowakabili kina Muro katika Mahaka ya Hakimu Mkazi Kisutu, akitoa ushahidi wake jana alidai kuwa alipigiwa simu na Muro aliyemweleza kuwa ana tuhuma nzito dhidi yake.

Alidai kuwa alipokea simu hiyo akiwa Bagamoyo Januari 28 mwaka jana na Muro alijitambulisha kwake na kumueleza kuwa anamuhitaji kwa mahojiano kuhusu tuhuma hizo.

Kwa mujibu wa madai hayo, walikubaliana kukutana kesho yake katika hoteli ya Califonia saa tano asubuhi ambako Muro alimwambia Wage ni vyema wakazungumzie tuhuma hizo katika hoteli ya Sea Cliff.

Wage alidai Muro alimwambia kuwa katika hoteli hiyo ndiko aliko bosi wake na wakakubaliana na kwenda Sea Cliff kwa kutumia gari ya Muro na kuiacha gari yake pale pamoja na dereva wake.

"Muro alinieleza kuwa nakabiliwa na tuhuma za ubadhilifu wa fedha za na ufisadi na kwamba anaandaa kipindi cha kueleza tuhuma hizo na biashara zangu katika kipindi cha Usiku wa Habari cha TBC1," alidai Wage.

Wakiwa njiani, Wage alidai mbele ya mahakama hiyo akiongozwa na Wakili Mkuu wa Serikali Stanslaus Boniface, kwamba Muro alipiga simu kwa mtu ambaye hakumfahamu lakini katika maongezi yao alimtaja Wage Alidai baada ya kukata simu hiyo, alitaka Muro amtaje aliyekuwa akiongea na Muro alimjibu alikua akiongea na Kaimu Mkurugenzi wa Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (TAKUKURU) ambaye anahitaji kufanya naye mahojiano kabla hajafikishwa mahakamani.

"Muro alinitishia kuwa yeye ni afisa wa jeshi na ana nyota tatu amesomea Uingereza na Marekani, alifungua dashboard ya gari na kutoa pingu, akaniambia nikileta fujo atanifunga, alinitolea na bastola na kuniambia pia ikishindikana kunidhibiti ananipiga risasi kwa kutumia bastola hiyo," alidai.

Kwa mujibu wa madai hayo, walipofika Sea cliff walipokewa na mtu aliyetambulishwa kwake kuwa ni Naibu Mkurugenzi wa Takukuru na jina lake moja ni Musa na wakaingia hotelini na baadaye aliingia mtu mwingine Muro akamtambulisha kuwa ni Kaimu Mkurugenzi wa taasisi hiyo.

Muro anadaiwa kuwaeleza wale watu kuwa Wage ni mla rushwa mkubwa wa Bagamoyo na kwamba habari zake zitatangazwa kituo cha TBC1 na kwamba ni lazima ashitakiwe kwa kosa hilo.

"Walinitisha kwa kuniambia kuwa sio watu wote wanaopelekwa mahakamani wana hatia, walisema Amatus Liyumba alibambikiwa kesi na rafiki yake wa BoT,"alidai.

Alidai walimwambia atoe Sh milioni 10 ili asaidiwe ambapo alikubali na kuwaomba awapatie Sh milioni moja kwanza ambazo anazo na nyingine angewapa kesho yake na baada ya hapo aliondoka katika hoteli hiyo.

Wage alidai alikwenda kituo cha kati cha Polisi kutoa taarifa, ambapo maofisa wa Polisi waliambatana na Karoli kwenye mgahawa wa City Gargen Januari 31 mwaka jana na kumpigia Muro aende kuchukua fedha hizo ambapo Muro anadaiwa alipofika pale na kuwaona askari alijaribu kutoroka lakini alikamatwa na kupelekwa Polisi.

Ilidaiwa gari la Muro lilipopekuliwa lilikutwa na miwani ya Karoli, na pingu, baadaye Muro alitoa bastola aliyokuwa nayo kiunoni. Kesi hiyo inaendelea leo mahakamani hapo.


 
Back
Top Bottom