Kesi ya Jerry Muro

uyu jamaa akienda jela miaka kama kumi hivi itakuwa safi, ili kiburi chake kikaishie hukohuko, watu wasio na maadili kama jeri muro hatuwataki hapa tz...alikuwa anawang'ang'ania wenzie kumbe yeye naye ni mbaya..unafiki huu. haponi huyu lazima akashike debe.

Mchaga na pesa baba
 
Msiba wakwamisha utetezi wa Murro


na Happiness Katabazi


amka2.gif
ALIYEKUWA Mtangazaji wa Shirika la Utangazaji la Taifa (TBC1) Jerry Murro anayekabiliwa na kesi ya kula njama, kushawishi na kuomba rushwa ya sh milioni 10, jana alishindwa kuanza kujitetea kutokana na kupata msiba.
Kesi hiyo ambayo jana ilikuja kwa ajili ya Murro na wenzake kuanza kujitetea lakini kutokana na Murro kupata msiba wa baba yake mdogo na kuomba udhuru huo mahakamani kesi hiyo ililazimika kuahirishwa hadi Mei 2 na 3.
Mbele ya Hakimu Mkazi wa Mahakama ya Hakimu Mkasi Kisutu, Gabriel Mirumbe, wakili wa kujitegemea Richard Rweyongeza, ndiye aliyewasilisha ombi la kesi hiyo kuahirishwa kutokana na mteja wake kupata msiba.
Mbali na Murro, washtakiwa wengine katika kesi hiyo ni Edmund Kapama na Deogratius Mugasa ambao wanadaiwa kula njama, kushawishi na kuomba rushwa ya sh milioni 10 kutoka kwa aliyekuwa Mhasibu wa Halmashauri ya Wilaya ya Bagamoyo, Michael Karoli Wage.
Kati ya mashtaka hayo matatu yaliyofunguliwa Februari mwaka jana dhidi yao, Murro anakabiliwa na mashtaka mawili.
 
Kutokana na nilivyopitia maelezo ya awali na nadhani ndo'yamwisho kwa jamuhuri. Jamaa wakisimama vzuri wanapangua ngoma kiulaini ka mshikaji zombe. ....ts just a mater of technicality! Na hii ipo wazi anaebisha akaandamane au akapange foleni loliondo.
 
Jerry Muro amlipua Masha Send to a friend
Thursday, 18 August 2011 22:24
0digg

Nora Damian
ALIYEKUWA Mtangazaji wa Shirika la Utangazaji Tanzania (TBC), Jerry Muro, anayekabiliwa na kesi ya kuomba rushwa ya Sh10 milioni, ameieleza mahakama kuwa aliyekuwa Waziri wa Mambo ya Ndani, Lawrence Masha, alimtisha kuwa hatochomoka katika sakata hilo.

Muro alieleza hayo jana katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu alipoanza kujitetea kwa mara ya kwanza dhidi ya tuhuma zinazomkabili.Katika utetezi wake uliodumu kwa saa tatu akiongozwa na mawakili wake, Majura Magafu na Richard Rweyongeza, Muro alidai kwamba Masha alisema mwisho wa kesi hiyo unampeleka yeye (Muro) kaburini.
Alisema siku chache baada ya yeye kukamatwa, Masha akiwa waziri alimfuata ofisini kwake TBC Mikocheni na kumtupia bahasha ikiwa na maneno ya vitisho."Masha alinifuata ofisini, nikaenda kuongea naye lakini ghafla nilipoingia tu kwenye chumba cha mkutano alinitupia bahasha ya rangi ya kaki," alizidi kutoa madai yake Muro na kuongeza:

"Nilizifungua bahasha hizo na kukuta picha tatu za CCTV ambazo Masha aliniambia ni za kwangu, aliniambia kaka umekwisha, mimi naondoka na wewe lazima utaondoka."Hata hivyo, picha hizo ambazo zilitolewa na upande wa mashitaka kama kielelezo katika kesi hiyo, Muro alizipinga akisema hakuna sura yake na kinachoonekana ni maumbo tu ya watu watatu ambao hata sura zao hazifahamiki.

Alidai mahakamani hapo kwamba, Masha alimwambia (Muro) aitishe mkutano wa waandishi wa habari na kusema Jeshi la Polisi halijamuonea, ila wamegongana tu kwenye utendaji wa kazi, lakini yeye hakufanya hivyo.

Muro ambaye kesi yake imekuwa ikivuta hisia za watu, alidai kuwa baada ya kuanza kuripoti habari za uchunguzi amekumbana na zaidi ya matukio 15 yanayohatarisha usalama wake na kwamba, licha ya kuyaripoti polisi hakuna hata moja lililofanyiwa kazi.
Alidai kutokana na matukio hayo, bosi wake wa awali Mwenyekiti Mtendaji wa Kampuni za IPP Reginald Mengi aliamua kumnunulia bastola ili imsaidie katika usalama wake na kwamba, aliwahi kuitumia."Hata pingu niliamua kununua ili inisaidie pale ninapoona nimebanwa, nimkamate mwenyewe mhalifu, kwa sababu nilisharipoti matukio mengi polisi, lakini hakuna lililozaa matunda," alidai Muro.

Mtangazaji huyo alidai watuhumiwa anaoshtakiwa nao hawafahamu na kwamba, hajawahi kuwaona na hata Wage anayetajwa kwenye hati ya mashitaka kuwa alimuomba rushwa hamfahamu.

Alidai kuwa habari zilizomletea matatizo ni zile zinazohusu askari polisi wa Kikosi cha Usalama Barabarani kufanya ufisadi katika Uwanja wa Ndege wa Mwalimu Nyerere, biashara ya uchangudoa, rushwa kwenye rumbesa Njombe na uchunguzi wa raia wa Korea aliyekuwa amemilikishwa eneo kubwa la ardhi huko Bagamoyo, mkoani Pwani.

Aliendelea kudai mahakamani hapo kwamba, baada ya uchunguzi kuhusiana na suala la raia huyo wa Korea baadhi ya watu walimpigia simu na kumfuata ofisini na kumshawishi achukue rushwa ya Sh60 milioni, ili aachane na habari hiyo, lakini alikataa na kuirusha habari hiyo hewani.

Muro alisema hakuwahi kumuomba Wage rushwa ili asirushe habari zake za ufisadi, kwa sababu mtu huyo tayari alishavuliwa madaraka na Waziri Mkuu Mizengo Pinda, hivyo kwake (Muro) hakuwa habari.
Aliongeza kwamba, hata baada ya kufikishwa mahakamani na kushtakiwa bado ameendelea kupata majanga mengi yakiwemo kuachishwa kazi, kukosa zawadi yake ya Dola za Marekani 4,000 zilizotokana na kupewa Tuzo ya Mwandishi bora na Baraza la Habari (MCT), kukosa nafasi ya kwenda kusoma katika Chuo Kikuu cha Tumaini na kufukuzwa kwenye nyumba aliyokuwa amepanga.

"Kabla ya kuachishwa kazi nilikuwa nalipwa pesa kidogo, lakini walipomuondoa Tido hata kile kidogo nikawa sipati na hata zawadi yangu ya MCT hadi leo sijapewa," alidai Muro.

Aliendelea kudai kuwa, ndani ya Jeshi la Polisi wako wanaomkandamiza na wanaoendelea kumuandama na kwamba, mwisho wa kesi hiyo unampeleka yeye kaburini.
Muro aliiomba mahakama imuachie huru kwa sababu hakutenda kosa lolote na kudai kuwa ni njama watu wachache wenye lengo la kutaka kumwangamiza.Hakimu Frank Moshi anayesikiliza kesi hiyo aliiahirisha hadi Septemba 27. mwaka huu washtakiwa wengine watakapoendelea kujitetea.
Mbali ya Muro washtakiwa wengine katika kesi hiyo ni Edmund Kapama na Deogratias Mgasa ambao kwa pamoja wanadaiwa kumuomba rushwa Wage aliyekuwa Mhasibu wa Halmashauri hiyo ya Bagamoyo.Kapama na Mgasa pia wanadaiwa kujifanya maofisa wa Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (Takukuru).

 
[h=4]Comments [/h]


0 #4 vonostus 2011-08-19 06:25 Lo! pole sana bro! kumbe hata kazi walisha kutemesha, naweza kukwambia usijali maadamu una taaluma ila inauma sana kunyang'anywa ulicho nacho wakati unakitafuta kwa kutumia akili na taaluma yako.
Quote









+2 #3 Mwanasheria 2011-08-19 04:28 Wakati mwingine tuzipitie hotuba za wazee wetu wa zamani na maneno yao,Enzi hizo za wazee alitokea mzungu mmoja na akasema kuwa Tanzania imo mfukoni mwake,lakini aligonga mwamba na kupewa masaa kutoeki baada ya kukaa,Sasa bwana Muro amepata bahati mbaya ya kugongana na walioiweka Tanzania mfukoni na kuweza kutoa vibali vya watu kwenda makaburini.
Hata kama wewe utakufa wao au yeye siyo kwamba ataendelea kuwepo daima,siku yake itafika kama ilivyofika kwenye ubunge na kung'oa hadi vitasa vya ofisi,Mwamini mungu muro,Wazee walisema Rushwa ni adui wa haki,na ukipenda rushwa utamtumikia tajiri,Sasa ikiwa nchi yetu ndiyo tayari inamtumikia tajiri,wanyonge tumembakisha mungu tuu kutulinda hadi siku zetu zitakapofikia.

MUNGU TUBARIKI WANYONGE,
MUNGU WAZIDISHIE PIA WALIOITIA TANZANIA MIFUKONI MWAO,

AMEEEEN
Quote









0 #2 waukwehee 2011-08-19 02:57 muro amini mungu nawe utashinda hao jamaa siomchezo kweli ulikosea sana kutoka pale IPP ila pia nimipango ya mungu,chamsingi muachie mungu nawe atakusaidia ukweli utafundulika tu
Quote









-1 #1 ahmed00 2011-08-19 01:34 @Mwongozo!
Uwana mageuzi wako ndani ya ccm utaishia kuwa kama Muro. Muro alifanya kazi mzuri alipokuwa chani ya IPP. MAFISADI waliona jinsi ya kumuangamiza lazima atoke IPP, wakamwadaa nae akaingia mkenge. Baada ya kujiunga TBC, basi alikuwa chini yao na wakambambikia kesi na watamfunga.
Mwongozo! Elewa Mtandao wa MAFISADI ni Mkubwa na una NGUVU za PESA. Hao kwa lugha nyingine ni MAFIA, angalia kabla hawajaku maliza
Quote







Refresh comments list
 
Pole sana kaka jerry!
Napenda nikueleze mambo machache kwa manufa yako sasa na hata baadae,naamin kubwa linalokutesa ni lile ambalo umekua ukifanya ktk kaz yako maili ya usiku wa habar kwa tbc,au lipoti maalumu kwa itv,binaf sisemi ni kweli unahatia au la ispokua kutoka moyon mwako wewe ndo unajua na mungu pee?
Jerry,sitaki kuingilia iman yako ila napenda kusema mungu ndio mkombozi wako hata kama ni kweli ulifanya mwambie "mungu nimekutenda dhambi na nimejifunza kutokana na hili naomba unitoe ktk janga hili kwan ulisema hata kama tunadhambi nyekundu utazisafisha na kuwa nyekundu kama seruji"
nataka kuamin kua upo kwenye mapito kaka,ambayo unatakiwa kuyashinda kwa msaada wa mungu,uliwika sana si kwa mali,uzur,uwanaume,kabira nk ispokua kwa kazi yako nzur,.sasa ni wakati wa kubezwa,kutukanwa,kutengwa,kuzalilishwa kama ulvyo fukuzwa kwenye pango,na bado mengine mengi yatajitoke na kutokuaminika kabisa.cha msing ni kumuomba mungu mpaka tone la mwisho na kumuambia akufanyie mlango wa kutokea,kwan imeandikwa kwenye biblia kua"jarbu halikukupata ili kuacha mkiwa hatakama unamajaribu sitokuacha pekeyako,ntakufanyia mlango wa kutokea.
Kaka muombe mungu akufanyie mlango wa kutokea,acha watu waseme wawezavyo,kama wengine wanavyoandika humu,lakin chukulia kama challenge yako.kwa mtu ambaye hakuwaikupitia shida atasema awezavyo.mara tapeli na nk,lakin wamesahau kma wakinachenge,lowasa wameiba sana na laajabu hawaijui mahakama.KAKA USIFE MOYO,MUOMBE MUNGU ATAKUWA NA WEWE MPAKA USHINDI
 
CarthbertL anaandika, pamoja na mengineyo:
"Ile kesi inayo mkabili mtangazaji wa shirika la utangazaji tanzania (TBC) Jerry Muro
upelelezi wake umekamilika na alitarajiwa kupandishwa kizimbani leo..."


mahakama ni hekalu la haki; haki itatendeka tu utaarifiwe au la kuhusu kesi hiyo, haibadilishi kitu.



si kila mahakam ni hekalu la haki ila zile tu zinazofuata misingi sheria na taratibu za kipata haki
 
Back
Top Bottom