Kesi ya Jerry Muro

Tumsifu Samwel

JF-Expert Member
Jul 30, 2007
1,407
159
Ile kesi inayo mkabili mtangazaji wa shirika la utangazaji tanzania (TBC) Jerry Muro
upelelezi wake umekamilika na alitarajiwa kupandishwa kizimbani leo.

Kwa mdau yoyote aliye na habari za kilichojiri uko mahakamani atujuze tafadhali.
 
mkuu kumbe bado upo JF?
Nilifkiri lile ombi lako la kuondolewa humu JF ulikuwa unamaanisha.!
 
hao ndo wale wa kujilipua, alitaka kujilipua bahati yake bom likakataa kulipuka...sasa bado yupo na kibajaji chake tunamwona anafurahia maisha jf...hahaha.
 
Jamani Ndibalema na Ubungoubungo mbona hamna majibu CarthbertL kauliza swali nyi mnaleta mzaha ...
 
Hahaha hata mimi nilimuuliza hilo swali sijui alisepa au? ila siyo kitu tunafurahi kuwa naye tuendelee kuchanja mbuga.
 
CarthbertL anaandika, pamoja na mengineyo:
"Ile kesi inayo mkabili mtangazaji wa shirika la utangazaji tanzania (TBC) Jerry Muro
upelelezi wake umekamilika na alitarajiwa kupandishwa kizimbani leo..."

mahakama ni hekalu la haki; haki itatendeka tu utaarifiwe au la kuhusu kesi hiyo, haibadilishi kitu.

kosa moja lisimuhukumu mtu! tumkaribishe jamani na mada yake tuchangie kama inavyostahili badala ya kuanza kumnanga!
 
Hii imekaeje wadau? Kelele nyingiii hatimaye kesi imefutwa tu kiaina (eti aliyemshitaki kaamua kumsamehe). Lakini nilijua ingefutwa kwa kuwa kulikuwa kuna dalili nyingi za kwamba ile kesi ilikuwa imetengenezwa ili kumchafua Muro. Hata hivyo inaonekana Muro ni mtu wa system (hisia zangu tu). Inaonekana polisi walikurupuka, wamefika mahali yamewashinda. Sijui na kesi ya kumilikii pingu nayo atasamehewa?
 
ambao hawana title kama za muro wanafia gerezani!! jamani!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!
 
All people under the law are equal, but others are more equal, tatizo letu unataka kufananinisha kifo cha kenyata na uhai wako.
 
Mi sijaelewa.. Kesi ipi imefutwa??? Maana ukisoma hiii habari kutoka katika gaezti la mwananchi inaonyesha kuwa jamaa kafutiwa kesi ya kukopa million 1.5.. Ila kuna ile kesi ya kutaka kutapeli millioni 10... Hebu niwekeni sawa hapa, ina maana jamaa alikuwa na kesi mbili????????
 
hiyo ya 1.5M ambayo alikuwa anadaiwa laki 5 (TZS500,000).
 
mkanganyiko wa taarifa, alie na taarifa wa kesi ipi imefutwa kati ya zilizokua zinamkabili Muro aje atujuze kiufasaha.
 
Hii imekaeje wadau? Kelele nyingiii hatimaye kesi imefutwa tu kiaina (eti aliyemshitaki kaamua kumsamehe). Lakini nilijua ingefutwa kwa kuwa kulikuwa kuna dalili nyingi za kwamba ile kesi ilikuwa imetengenezwa ili kumchafua Muro. Hata hivyo inaonekana Muro ni mtu wa system (hisia zangu tu). Inaonekana polisi walikurupuka, wamefika mahali yamewashinda. Sijui na kesi ya kumilikii pingu nayo atasamehewa?

MSOME VIZURI..

Saturday, July 10, 2010

HATIMAYE JERRY MURO AFUTIWA MASHTAKA YAKE...

Ile kesi ya Utapeli anayotuhumiwa Mtangazaji wa zamani wa ITV ambaye kwasasa anapiga mzigo na TBC1 bwana JERRY MURO hatimaye imefutwa baada ya Mlalamikaji bwana EDUARDO CHAMUHENE ambaye ni mkurugenzi mtendaji wa Boneste General Enterprises ya jijini kuamua KUMSAMEHE! Inadaiwa apo awali Jerry alimkopa uyo bwana sh Milioni 1.5 kwa ajili ya kwenda kutoa gari yake Bandarini na baada ya miezi 2 Jerry alipunguza deni kwa kumlipa m1 na kubaki laki 5 iliyomfikisha Mahakamani Hapo jana!

KINYAIYA'S ENTERTAINMENT:: HATIMAYE JERRY MURO AFUTIWA MASHTAKA YAKE...
 
Kumbe ile Kesi ya Kova ya utapeli/rushwa ya 10m/- pamoja na mambo ya kumiliki pingu bado iko palepale?
 
I got to know, kwa hiyo jamaa alikuwa ana kesi mbili??!! Na mwananchi nao, wameiandikaje hii habari wakati wanajua sisi hatuijui hiyo kesi nyingine?
 
Back
Top Bottom