Ndallo
JF-Expert Member
- Oct 1, 2010
- 7,619
- 4,292
Kuna tetesi zilizojitokeza kua kuna mikakati inayoandaliwa na jeshi la polisi mkoani Arusha kua ile kesi iliyokua inawakabili viongozi wa Chadema pamoja na wafuasi wao kua ifikapo tarehe 21 ya mwezi huu wa January siku watakapo kua pale mahakamani jeshi limeweka mikakati ya kupambana tena na wafuasi wa Chadema ili wasihuzurie mahamani kuwasindikiza viongozi wao, habari hizi nilizozipata kutoka ndani ya jeshi hili ni kua polisi wakisaidiana na wanajeshi wa kikosi cha kutuliza ghasia wamedai watapambana kufa na kupona na yoyote yule atakayesogelea uzio wa mahakama. Hofu yangu mimi ni kua kuna uwezekano mkubwa wa kutokea fujo kama zile zilizojitokeza hapo nyuma. Wana JF hizi ni tetesi nilizozipata kutoka ndani ya jeshi la polisi. Nawasilisha hoja hii mbele yenu kama kuna mtu mwenye hizi taarifa kwaua mimi pia ni mmoja wa wanaharakati ninayetaka niwepo pale mahakamani tarehe 21 January.