Petro E. Mselewa
JF-Expert Member
- Dec 27, 2012
- 10,199
- 25,520
Mwenyekiti wa Taifa wa NCCR-Mageuzi, James Mbatia ametinga Mahakama Kuu ya Tanzania na ameshafungua kesi ya kikatiba kuhusu kujiuzulu kwa Spika Job Yustino Ndugai. Kwa taarifa nilizonazo binafsi, tayari kesi husika imeshasajiliwa na imepangiwa jopo la Majaji watatu la kuisikiliza kesi hiyo. Wakati kesi hiyo ikiwepo mahakamani, tayari CCM na ADC wameshawapitisha wagombea wao wa nafasi ya Spika wa Bunge.
Nimekuwa nikifuatilia maoni ya watanzania na wasio watanzania kwenye mitandao ya kijamii, mitaani, runingani na redioni kuhusu kesi iliyofunguliwa na Mbatia. Wengine wanamuona Mbatia akitaka Ndugai abaki kuwa Spika wa Bunge kwa njia ya Mahakama. Wapo wanaomuona Mbatia kama anayepoteza muda na 'fedha' zake kwa jambo lisilo na maana na kuwa jambo hilo limeshapitwa na wakati. Wapo wanaompongeza. Lakini, wengi wanambeza.
Suala la utetezi wa Katiba ni suala kubwa na la muhimu kwa kila mmoja wetu. Kila Mtanzania, kwakuwa Katiba ni sheria yetu mama, anapaswa kuilinda na kuitetea katiba yetu. Katiba inapotoa masharti ya kufuatwa, lazima yafuatwe. Katiba imetoa masharti ya kufuatwa na Spika anayetaka kujiuzulu. Ni lazima yafuatwe. Mbatia ameona hayakufuatwa. Amekwenda mahakamani kuitetea na kuilinda Katiba yetu iliyotoa masharti ambayo ameona yamekiukwa. Ni haki yake na anafanya jambo jema.
Viongozi wetu, wanapoapishwa, huapa kuilinda na kuitetea Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania. Sheria zote nyinginezo (zinazotungwa na Bunge na zile Ndogondogo) hazipaswi kukinzana na Katiba. Pale zinapokuwa kimya, Katiba hutumika. Haipendezi kushabikia viongozi ambao hawaifuati Katiba yetu kwa minajili ya kuilinda na kuitetea kama walivyoapa. Tena, viongozi wenyewe ni wale wanaotokea kwenye Bunge ambalo ndilo linalotunga sheria.
Si sawa Athumani, aliyedhaminiwa na Musa kupata kazi kwa Ally, kuandika barua yake ya kuacha kazi akiielekeza kwa Musa huku akitoa nakala tu kwa Ally-mwajiri wake. Hapo, aliyepaswa kuandikiwa barua husika ni mwajiri ambaye ni Ally na nakala inaweza kuelekezwa kwa Musa ikimpendeza Athumani. Kimsingi, Mbatia ana haki na hoja za kufungua shauri lake Mahakama Kuu ya Tanzania kupata tafsiri ya kikatiba juu ya suala hilo. Atabezwa lakini atabaki na hoja yake.