Kenya watoa fidia ya mamilioni kwa wahanga wa ng'ombe waliopigwa mnada na Tanzania

Synthesizer

JF-Expert Member
Feb 15, 2010
11,143
18,774
Kenya imewalipa fidia wafugaji waliopoteza ng'ombe baada ya serikali ya Tanzania kuwakamata na kuwapiga mnada kwa madai kuwa walivuka mpaka na kuingia Tanzania na hivyo kukiuka sheria za mipaka kati ya nchi. Serikali ya Kenya imetoa kiasi cha shilingi za Tanzania bilioni moja (Tshs 1.1b) kuwalipa wahanga wa mnada wa Tanzania ili kuwaepusha na kuingia umasikini baada ya mifugo yao kupigwa mnada na serikali ya Tanzania.

Wakati Tanzania ikikamata mifugo takribani 1,700 ya jamii ya Wamasai wa Kenya walioingia Tanzania, Kenya pia ilikamata mifugo takribani 3,000 ya jamii ya Wamasai Watanzania waliokuwa wameingia Kenya katika kipindi hicho hicho. Baadaye mifugo yote ya Tanzania iliachiwa kwa kile viongozi wa Kenya walichoita kwamba wao sio walipizaji kisasi.

Itakumbukwa kwamba wengi wa wafugaji walionyang'anywa mifugo na serikali ya Tanzania ni jamii ya Masai ambao kwa miaka mingi wamekuwa wakivuka mpaka na mifugo yao kati ya Kenya na Tanzania. Hili pia lilikuwa likifanyika kwa jamii ya Wamasai wa Tanzania kuvuka mpaka na kuingia Kenya na mifugo yao, na halijawahi kuonwa kuwa tatizo katika awamu zote zilizotangulia za uongozi wa Tanzania na Kenya. Jamii ya Wamasai inayoishi eneo la mpaka kati ya Kenya na Tanzania ina muingiliano wa kindugu na eneo la kuchunga mifugo (pastoralism) ambavyo havikuzingatiwa wakati wa kugawa mpaka kati ya Kenya na Tanzania, kama ambavyo mbuga za Serengeti Tanzania na Masai Mara Kenya kugawanywa na kufanya wanyama kila mwaka kuvuka mpaka kati ya hifadhi hizi mbili zinazopakana katika kile kinachoitwa the Great Wildebeest Migration.
 
Msukuma na mmasai hawaelewani kwa asili.Usipokuwa na hekima wewe uliebadilisha asili hizo kwa elimu ukashindwa kuzipatanisha jamii hizi kwa elimu yake na badala yake ukaasist mfarakano huo unakuwa hovyo zaid ya uhovyo.
 
Na sisi tuwalipe na kuwaomba radhi.namkubari Uhuru kenyata.
 
Back
Top Bottom