Kenya kama Malawi, wapanga kupeleka vibarua wa Mashamba ya Israel kwa ujira wa Ksh. 228,000 (4,000,000Tsh)

ChoiceVariable

JF-Expert Member
May 23, 2017
43,177
49,923
Kenya inapanga Kupeleka Vijana wapatao 1,500 kuwa Vibarua wa Mashamba ua Wayahudi Kufuatia Vibarua zaidi ya 10,000 wengi wao kutoa Thailand kukimbia Vita vya Israel vs Hamas hivyo kuacha mashamba ya waloweso yakiwa hayana Vibarua.

Israel Kwa Sasa imekuwa inakimbilia Afrika ambako watu Wana shida na njaa Kali kupata Vibarua wa Mashamba Kwa kuingia makubaliano na Nchi zinazotaka kuwauza watu wake kuwa Manamba.Kenya imeungana na Malawi katika ku export Manamba bila kujalisha vita vinavyoendelea.


View: https://twitter.com/Kenyans/status/1732659113245409360?t=dKV8Sq3MVESiicFRnoy9vQ&s=19

Kwa mtu mweusi utu sio kipaombele akina pesa ndio maana wakati wa biashara ya utumwa mawakala walikuwa Weusi wenzetu.

Swali.
Je Wabongo mko tayari kuwa Manamba kwenye mashamba ya Wayahudi mlipwe Ujira wa Shilingi Milioni 4?

View: https://twitter.com/BBCAfrica/status/1732724178812387367?t=3YyJH021dtzxhz1K23xAdA&s=19

Pia soma Malawi: Rais Chakwera akosolewa kwa kutuma vijana 221 wa Malawi kufanya kazi katika mashamba nchini Israel
 
Utumwa ni maamuzi ya MTU ili mtu akufanye mtumwa anaanza kucheza na hisia zako Kwa kuamini bila kufanya kazi ngumu utakufa njaa.

Huwa nasema Kama ilivyo ccm inatumia simba na yanga kuitawala nchi Kwa kuwapumbaza watoto ,vijana na wazee

MTU ukiona hataki utumie Akili zako Bali hisia lazima akutawale Leo kesho daima.
 
Hata mimi wakija tanzania naenda,mshahara wa laki 6 ninazolipwa kama mwalimu niliyefanya kazi kwa zaidi ya miaka 10 hautoshi kabisa yaani ,watoto watatu,mke jumlisha mikopo ya bayput ,nmb,crdb,napaki na kiasi cha 200K,sasa mtu unalipwa 4M kwa mwezi mbona pesa ndefu,waje na tz, I will be the first
 
Utumwa gani hapo. Hiyo salary hata daktari hapati na ndio wanaenda kupewa tena kwenye mazingira mazuri, haki zinazingatiwa, bima, mapumziko, na mkataba unaovunjwa au wenye kikomo.

Kuna mmoja namjua ameenda Israel kakaa mwaka karudi na some few millions kwa diploma yake ya kilimo kutoka LITA. Kaja wiki kadhaa kabla ya mashambulizi ya Hamas alikuwa kwenye ufugaji.
 
Hata mimi wakija tanzania naenda,mshahara wa laki 6 ninazolipwa kama mwalimu niliyefanya kazi kwa zaidi ya miaka 10 hautoshi kabisa yaani ,watoto watatu,mke jumlisha mikopo ya bayput ,nmb,crdb,napaki na kiasi cha 200K,sasa mtu unalipwa 4M kwa mwezi mbona pesa ndefu,waje na tz, I will be the first

Tafuta financial freedom Kwa kuwekeza na Kuwa na matumizi sahihi ya jala zako .

Paycheck to paycheck life ,ulibidi kuachana nayo baada ya Mwaka wako Wa kwanza Wa ajira.

Your problem is not about meager salary but financial intelligence

Whatever what you earn all you need is to set goals toward into financial freedom.

Bright and broke is only you looking for
 
Nyinyi kupeleka "beki tatu" Saudia sawa ila Kenya kupeleka manamba Israel inakuwa nongwa!

 
Mbona wasichana wakazi za ndani wengi Sana wanapelekwa nchi za kiarabu kila uchao tena kwa mishahara chini ya hapo sijasikia kelele mkuu?! Na wengine wanafia huko ukiacha wanaonyanyasika, kubakwa na kupokonywa passport zao!!

Sembuse hii ya Israel Tena mshahara mkubwa Sana kuliko hata bekitatu wanaopelekwa katika nchi zenye mateso lukuki za kiarabu?!

Kuna rafiki yangu ni operator wa mitambo ya ujenzi, alienda Qatar wakati wa maandalizi ya kombe la dunia, kulikuwa na ujenzi wa viwanja na maeneo mengine ya kufikia wageni.

Kampuni za Qatar zilichukua Sana wafanyakazi kutoka nchi za Pakistan, India, Nepal, Indonesia, Bangladesh, Philippines na huku kwetu Afrika. Wakiwaahidi ujira mzuri na marupurupu manono pia maeneo ya kufikia mazuri yenye viyoyozi (air condition), refrigerator, Wi-Fi , etc pia mshahara mzuri wa kuanzia million moja na nusu na kuendelea.

Wengi walisaini mkataba hapa bongo na kuelekea Qatar, walilipiwa nauli na mambo mengine, kufika kule waliletewa mkataba mwingine ulioandikwa kwa lugha ya kiarabu lugha wamsiyoijua wakasainishwa kinguvu , wakakuta hakuna cha Wi-Fi, ac, Wala refrigerator, na kwenye chumba kimoja wanalala nane badala ya watu wawili walioahidiwa kwenye mkataba hapa Bongo kabla ya kwenda Qatar.

Na mshahara wakaanza kulipwa laki saba badala ya m 1.5 waliyoahidiwa kwenye mkataba wa awali.

Na hakuna pa kushtaki Wala kulalamika ,kazi mnaamka saa tisa usiku kwenda site kurudi saa kumi na mbili jioni kinyume na masaa nane ya kazi waliyosaini kwenye mkataba wa hapa bongo, na hauruhusiwi kufanya kazi nyingine nje ya mkataba na Kama utakutwa unashtakiwa na kufungwa.

Sasa mtu na skills zake huko uarabuni analipwa Kama kibarua wa hapa bongo kwenye Miradi mikubwa Kama stiglers gorge, sembuse Israel inayolipa unskilled labour mshahara wa mamilion ????!!!!!!

Tuwe serious Basi wakuu!!
Kama hao wa Israel wakija na huku Bongo hata Mimi nishtueni please niende mbio...!!
 
Tafuta financial freedom Kwa kuwekeza na Kuwa na matumizi sahihi ya jala zako .

Paycheck to paycheck life ,ulibidi kuachana nayo baada ya Mwaka wako Wa kwanza Wa ajira.

Your problem is not about meager salary but financial intelligence

Whatever what you earn all you need is to set goals toward into financial freedom.

Bright and broke is only you looking for
Endelea kusoma Vitabu vya kina kiyosaki ila ground ni kugumu
 
Utumwa ni maamuzi ya MTU ili mtu akufanye mtumwa anaanza kucheza na hisia zako Kwa kuamini bila kufanya kazi ngumu utakufa njaa...
Kwani utumwa ni nini? Hawa wahindi wana viwanda hapa nchini na wameajiri sisi weusi kwa ujira kidogo sana 4000 kwa siku na hamuoni ni utumwa.

Sasa kwenda kufanya kazi kwa 4m mnalalamika ni utumwaaa! Wale ma house girl kule uarabuni mbona hamsemi ni utumwa??
 
Hivi vitu rais samia ndio vya kuhangaikia afanye mpango watanzania na sisi twende uko sio kuhangaikia house girl kwenda OMAN kwa mshahara wa laki 6.
Wewe nae ni mbuzi tuu, kwenye Mpango wa Saudia na UAE Kuna watu wa fani mbalimbali wakiwamo hao uliowakariri.

Mwisho Samia hawezi wauza watu wake kisa Pesa.Kati ya maslahi ya kibiashara na utu,siku zote ccm inasimama upande wa utu.
 
Back
Top Bottom