Kaya 644 Magomeni kota zagomea kusaini mkataba kununua nyumba

Hapa ilihitajika elimu kwa umma kabla ya kuwasainisha.
P
Walioishi hapo ni mababu na mabibi zao ambao pia walikuwa wamepangishwa na halmashauri!! Sikujua huu utaratibu WA kuwafidia wajukuu wa wapangaji pesa na nyumba bila Mkataba ulitoka wapi!? Just politics!! Eneo ni strategical Kwa biashara na Sio kujenga na kugawa Bure!! Majengo ya biashara Malls zingezaa ajira nyingi, my country!! Makazi wangejenga chanika na Mabwe Pande
 
Hutaki kuingia kwenye mkataba unafukuzwa tu, sisi tuko nje hapo tunazitamani nyumba hizo.

JPM alilazimisha zijengwe kisa tu Manji alikuwa na Nia ya kuweka shopping mall Kali hapo, ili kumkomoa, akasema wananchi hao wajengewe nyumba, Sasa tangu lini serikali inajengea wananchi nyumba?
Inashangaza Just double standard na Kodi zetu
 
Hapa ilihitajika elimu kwa umma kabla ya kuwasainisha.
P

Wengi wanaoishi hizo nyumba ni watumishi wa umma, wanalipa kodi wanapojisikia PIA kodi ni ndogo sana, watumishi wa umma wanapenda dezo sana, na wengi walioingia hapo ni kwa vimemo.

sasa wao wanataka wauziwe kwa bei wanazozitaka wao (inaonekana kabisa), serikali inaela ujinga, eti wanaenda kumwambia Raisi,

watu weusi tuna shida mahali, KABISA
 
Wakazi 644 wanaoishi Magomeni Kota wamegoma kusaini Mkataba wa Manunuzi ya nyumba hizo kwa madai bei mpya walizopewa ni kubwa na haziendani na hali ya Uchumi wao.

Wakazi hao wamesema bei mpya iliyowasilishwa ni kati ya Tsh. Milioni 48 kwa Chumba na Sebule hadi Tsh. Milioni 56 kwa Vyumba 2 na Sebule kwa malipo ya miaka 15, kiwango ambacho wamedai ni kikubwa na ni mtego wa kuwafukuza.

Kwa mujibu wa taarifa ya TBA, Bei iliyopendekezwa na Serikali Juni mwaka 2022 ya Tsh. Milioni 12 hadi Tsh. Milion 17 kwa malipo ya marejesho ya miaka 10, haikukidhi thamani ya eneo, haikujumuisha faida na huduma za muhimu.

================

Wakazi 644 wa Magomeni Kota wamegomea kusaini mkataba wa kuanza kununua nyumba hizo, kwa madai kwamba bei waliyoletewa sio rafiki na haiendani na hali ya uchumi wao.

Aidha wamemuomba Rais Samia Suluhu Hassan aingilie kati kwa kuwa bei ya Serikali iliyowasilishwa ni kati ya Sh48 milioni na Sh56 milioni ni kiwango kikubwa wanachochukulia kama mtego wa kutaka kuwafukuza.

Kwa mujibu wa taarifa iliyowasilishwa juzi na serikali kupitia kwa Wakala wa Majengo Tanzania (TBA) ambaye ni msimamizi wa mradi huo, mkataba huo unaanza kutumika kuanzia Februari 8 mwaka huu hivyo Kaya hizo zinapaswa kusaini kwa bei waliyoletewa.

Mwanasheria wa wakazi hao, Twaha Taslima akisoma barua iliyoandikwa na Mtendaji Mkuu wa Wakala wa Majengo Tanzania (TBA), Daud Kandoro, kwenda kwa wakazi hao, jana siku ambayo walifanya kikao mkoani Dar es Salaam, alisema bei iliyowasilishwa na serikali awali ilikuwa ndogo.

“Bei ambayo ilipendekezwa na Serikali awali ilikuwa ni Sh12 milioni hadi Sh17 milioni, iliyotolewa Juni mwaka jana, haikukidhi thamani ya eneo, haikujumuisha faida wala huduma za maeneo yanayozunguka makazi hayo ambayo ni jumuishi,” amesema.

Taslima amesema, "Njia mojawapo ya kuchukua ni kuiomba Serikali au kwenda mahakamani. Bei ya chumba na sebule kwa Sh48. 5 milioni na vyumba viwili na sebule Sh56.8 milioni inaweza isiwe rafiki na mnunuzu asimudu," alisema Taslima.

Mwenyekiti wa Wakazi wa Magoneni Koti, George Abel, amesema kwamba bei zilizokokotolewa siyo rafiki kwa wakazi hao, licha ya Serikali kuongezewa mkataba wa kulipa na kuishi kutoka miaka 10 hadi 15.

Amesema kuwa bei hiyo inatakiwa kila mkazi alipie Sh300,000 kwa mwezi hivyo kwa mwaka ni Sh3.6 milioni akisema kiasi hicho ni kikubwa ikizingatiwa baadhi ya wakazi tayari ni wazee na wastaafu.

"Tumepokea barua hii ikiwa zimebaki siku tatu tu kwamba tusaini mkataba wa manunuzi, tukutane tujadiliane kabla ya tarehe 8, Februari, mwaka huu, hizi bei si rafiki haziendani na hali za wakazi walio wengi," amesema Abel.

Mmoja wa wakazi wa nyumba hizo, Salama Goronga (65), amesema barua hiyo iliyosomwa kwao, ikionyesha bei hiyo imewahuzunisha kwa kuwa haiendani na hali zao kimaisha.

"Mimi nina wajukuu, na iliposomwa barua machozi tu yameanza kunitoka hiyo pesa nitatoa wapi, nitaondoka hapa niende wapi," amesema Salama.

Mkazi mwingine, Mwajuma Hamisi (82), amesema ana watoto wawili wa walioolewa ndio wanaomtunza kwa kumnunulia chakula na mahitaji mengine, hivyo itawawia vigumu leo hii waanze kumtafutia kodi mara atakapoondoka kwenye makazi hayo kutokana na kushindwa kulipia.

"TBA wanaotaka hizo nyumba, leo bei hii, kesho hii, tutalipaje mimi mzee, wanitoe hapa si aibu kwangu, mamilioni hayo nitayatoa wapi," amesema Mwajuma.

Alipoulizwa Kaimu Mkurugenzi kutoka idara ya miliki TBA, Said Mndeme amesema “Masuala hayo aulizwe mkuu wa taasisi ndiye anayejua,” amesema

MWANANCHI
 
View attachment 2508191

Dar es Salaam. Wakazi 644 wa Magomeni Kota wamegomea kusaini mkataba wa kuanza kununua nyumba hizo, kwa madai kwamba bei waliyoletewa sio rafiki na haiendani na hali ya uchumi wao.

Alipoulizwa Kaimu Mkurugenzi kutoka idara ya miliki TBA, Said Mndeme amesema “Masuala hayo aulizwe mkuu wa taasisi ndiye anayejua,” amesema.

Mwananchi
Walidhani watapewa bure? Zile zilikuwa kampeni na hadaa za Jpm.

Sisi tulijua mapema tu
 
Dunia nzima masikini hatuishi Downtown kwenye makazi rasmi yenye hadhi

wawape fursa ya kuuza hizo nyumba, watakuja Wahindi watanunua kwa bei ya juu na watabaki na chenji ya kwenda kujenga Majohe baada ya kulipia TBA
Magu aliyesimamia zijengwe alisema wakae hao maskini downtown,

Ajenge mjomba, akifariki anakuja kuziuza asohusika?
 
Chumba kimoja na sebule mtu akinunue Kwa ML 50?

WOSIA wa mahehemu haufuatwi!!!

Ukiona NCHI , Mungu ameruhusu atawale mtoto au ......... Anataka KUTUADHIBU.

Tuombe TOBA na REHEMA juu ya nchi yetu.

Aaaamen.
Wewe ulitaka wauze kwa kiasi gani?
Kwani watu wanalazimishwa kuzinunua hizo apartments?
Kama hao wakazi wanaona ni bei kubwa waachanane nazo, kuna sehemu kibao za kuweza kununua au kujenga nyumba na kuishi kwa gharama nafuu. Na pia kuna wananchi kibao wako tayari hata leo kuja kuzinunua hizo apartments kwa bei hiyo hiyo.
 
View attachment 2508191

Dar es Salaam. Wakazi 644 wa Magomeni Kota wamegomea kusaini mkataba wa kuanza kununua nyumba hizo, kwa madai kwamba bei waliyoletewa sio rafiki na haiendani na hali ya uchumi wao.

Aidha wamemuomba Rais Samia Suluhu Hassan aingilie kati kwa kuwa bei ya Serikali iliyowasilishwa ni kati ya Sh48 milioni na Sh56 milioni ni kiwango kikubwa wanachochukulia kama mtego wa kutaka kuwafukuza.

Kwa mujibu wa taarifa iliyowasilishwa juzi na serikali kupitia kwa Wakala wa Majengo Tanzania (TBA) ambaye ni msimamizi wa mradi huo, mkataba huo unaanza kutumika kuanzia Februari 8 mwaka huu hivyo Kaya hizo zinapaswa kusaini kwa bei waliyoletewa.

Mwanasheria wa wakazi hao, Twaha Taslima akisoma barua iliyoandikwa na Mtendaji Mkuu wa Wakala wa Majengo Tanzania (TBA), Daud Kandoro, kwenda kwa wakazi hao, jana siku ambayo walifanya kikao mkoani Dar es Salaam, alisema bei iliyowasilishwa na serikali awali ilikuwa ndogo.

“Bei ambayo ilipendekezwa na Serikali awali ilikuwa ni Sh12 milioni hadi Sh17 milioni, iliyotolewa Juni mwaka jana, haikukidhi thamani ya eneo, haikujumuisha faida wala huduma za maeneo yanayozunguka makazi hayo ambayo ni jumuishi,” amesema.

Taslima amesema, "Njia mojawapo ya kuchukua ni kuiomba Serikali au kwenda mahakamani. Bei ya chumba na sebule kwa Sh48. 5 milioni na vyumba viwili na sebule Sh56.8 milioni inaweza isiwe rafiki na mnunuzu asimudu," alisema Taslima.

Mwenyekiti wa Wakazi wa Magoneni Koti, George Abel, amesema kwamba bei zilizokokotolewa siyo rafiki kwa wakazi hao, licha ya Serikali kuongezewa mkataba wa kulipa na kuishi kutoka miaka 10 hadi 15.

Amesema kuwa bei hiyo inatakiwa kila mkazi alipie Sh300,000 kwa mwezi hivyo kwa mwaka ni Sh3.6 milioni akisema kiasi hicho ni kikubwa ikizingatiwa baadhi ya wakazi tayari ni wazee na wastaafu.

"Tumepokea barua hii ikiwa zimebaki siku tatu tu kwamba tusaini mkataba wa manunuzi, tukutane tujadiliane kabla ya tarehe 8, Februari, mwaka huu, hizi bei si rafiki haziendani na hali za wakazi walio wengi," amesema Abel.

Mmoja wa wakazi wa nyumba hizo, Salama Goronga (65), amesema barua hiyo iliyosomwa kwao, ikionyesha bei hiyo imewahuzunisha kwa kuwa haiendani na hali zao kimaisha.

"Mimi nina wajukuu, na iliposomwa barua machozi tu yameanza kunitoka hiyo pesa nitatoa wapi, nitaondoka hapa niende wapi," amesema Salama.

Mkazi mwingine, Mwajuma Hamisi (82), amesema ana watoto wawili wa walioolewa ndio wanaomtunza kwa kumnunulia chakula na mahitaji mengine, hivyo itawawia vigumu leo hii waanze kumtafutia kodi mara atakapoondoka kwenye makazi hayo kutokana na kushindwa kulipia.

"TBA wanaotaka hizo nyumba, leo bei hii, kesho hii, tutalipaje mimi mzee, wanitoe hapa si aibu kwangu, mamilioni hayo nitayatoa wapi," amesema Mwajuma.

Alipoulizwa Kaimu Mkurugenzi kutoka idara ya miliki TBA, Said Mndeme amesema “Masuala hayo aulizwe mkuu wa taasisi ndiye anayejua,” amesema.

Mwananchi
Serikali ya Tz, daima kigeugeu, si wawazi na ubabaishaji mwingi kwa wawekezaji, si wa ndani, si wa nje!
 
Wewe ulitaka wauze kwa kiasi gani?
Kwani watu wanalazimishwa kuzinunua hizo apartments?
Kama hao wakazi wanaona ni bei kubwa waachanane nazo, kuna sehemu kibao za kuweza kununua au kujenga nyumba na kuishi kwa gharama nafuu. Na pia kuna wananchi kibao wako tayari hata leo kuja kuzinunua hizo apartments kwa bei hiyo hiyo.
Maelekezo ya Magu wakati anaahidi kuzijenga alielekeza waliopo wasiondolewe,

Alitaka maskini wakae nao nyumba nzuri za kisasa.

Nyumba hamkujenga ninyi, kwann mzitolee mate?

Kwann kujitafutia LAANA za kujitakia?

Jengeni zenu hata kule makueni au kule Kiembe samaki mzifanye apartment za biashara.
 
Back
Top Bottom