Nyumba za Magomeni ndugu zangu mmeokota dodo!

Tengeneza Njia

Senior Member
Jul 29, 2022
121
204
Nimesikia ndugu zetu wapangaji wa nyumba za Magomeni wanamuomba Mh. wauziwe nyumba zile kwa Tsh 17M? Kweli?

Serikali imesema itawauzia kwa Tsh 48M (chumba na sebule) na 56 + (kwa nyumba kubwa), na hii inalipwa kwa muda wa miaka 15.

Piga mahesabu yako vizuri kwa huyu atakaye lipa 56+ atatakiwa kulipa laki tatu tatu kila mwezi kwa muda wa miaka hiyo 15

Hii si bei ya kodi ya mwezi kabisa ya nyumba ya hadhi hiyo? Naona hawaoni uzito wa mali hii wanayotaka kumilikishwa kwa mteremko!
 
Hao jamaa kweli wameokota dodo, kama wanajimudu badala ya kuunga unga walipe baada ya miaka 15, wanaweza nunua kwa muda mfupi.

Then waje kuuza kwa bei kali mbele ya safari, waende zao kununua viwanja vikubwa nje ya mji, wajenge nyumba kubwa zaidi ya hizo, na waachane na maisha ya kubanana hata kama wako ghorofani.

Au wanaweza pia kuamua kuondoka hapo wakapange uswahilini, wakusanye kodi nzuri coz sehemu nyumba zilipo ni center ya mji, then hiyo kodi waka invest sehemu nyingine mbele ya safari..
 
Hao jamaa kweli wameokota dodo, kama wanajimudu badala ya kuunga unga walipe baada ya miaka 15, wanaweza nunua kwa muda mfupi...
Hizo nyumba baada ya miaka 15 hutazitamani.

Labda kama maintainance ni juu ya Serikali, na watafanya kama inavyotakiwwa.

Milioni 48 unajenga nyumba nzuri Chanika. Wengi wao hawastahii kukaa Magomeni, hata mjini huwa hawaendi.
 
Nafikiri tungekuja na mkakati hizo nyumba zibaki kupangishwa tuu. Ukiweza kupanga ndani ya miaka 15 nyumba itakua mali yako.

Huwezi jenga nyumba mjini kwa iyo bei ya million 17 tena Magomeni
 
Nimesikia ndugu zetu wapangaji wa nyumba za Magomeni wanamuomba Mh. wauziwe nyumba zile kwa Tsh 17M? Kweli...
inshu sio muda wa kulipa bali ni kiasi cha fedha,yaani chumba kimoja na sebule kwa 48milioni? wengi hawataweza.

Wataishi tu bure kwa muda huo then baada ya hapo wataondoka tu wakaishi mahali pengine watakapokuwa wametafuta viwanja.Mtu na familia chumba kimoja mtaishi vipi?
 
Mkuu bei mbona ni reasonable kwa hapo daslamu,tena mnasema eneo ni la kati kati ya mji, hapo bei hiyo ni ndogo Mkuu,baadae ukiamua kupangisha unakula tu pesa
 
Hizo nyumba baada ya miaka 15 hutazitamani.

Labda kama maintainance ni juu ya Serikali, na watafanya kama inavyotakiwwa.

Milioni 48 unajenga nyumba nzuri Chanika. Wengi wao hawastahii kukaa Magomeni, hata mjini huwa hawaendi.
Chanika?
Ikiwa shughuli zako unafanyia town, kujenha Cjanika ni ghali sana kwa usafiri wa kila siku.
 
Hizo nyumba baada ya miaka 15 hutazitamani.

Labda kama maintainance ni juu ya Serikali, na watafanya kama inavyotakiwwa.

Milioni 48 unajenga nyumba nzuri Chanika. Wengi wao hawastahii kukaa Magomeni, hata mjini huwa hawaendi.
Ni kweli miaka 15,hizo nyumba kama zitakosa maintanance,zitakuwa hazifanani kabisa,thamani ya hizo nyumba itapaa kwa sababu ya location,kwakuwa ziko katikati ya jiji...
 
Ambaye atashindwa kununua kwa bei hiyo, aruhusiwe kuuza haki ya kununua kwa mtu mwenye uwezo.
Nimemuona mzee wa miaka 85 akilalamika eti hana pa kwenda unabaki unawaza, mzee kama huyu alikuwa wapi wakati Dar ikiwa mapori ambayo yalikuwa yanagawiwa bure? Alishindwaje kupata hata ardhi ya miguu ya 20 kwa 20?
 
Historia inasaidia kutoa mafunzo! ukute kipindi hiko aliona ni kupoteza pesa.
 
Ambaye atashindwa kununua kwa bei hiyo, aruhusiwe kuuza haki ya kununua kwa mtu mwenye uwezo.
Nimemuona mzee wa miaka 85 akilalamika eti hana pa kwenda unabaki unawaza, mzee kama huyu alikuwa wapi wakati Dar ikiwa mapori ambayo yalikuwa yanagawiwa bure? Alishindwaje kupata hata ardhi ya miguu ya 20 kwa 20?
Usikute enzi zake alikuwa panya road au mla bata viwanja vyote mjini hakosi(utani tu)
 
Nimesikia ndugu zetu wapangaji wa nyumba za Magomeni wanamuomba Mh. wauziwe nyumba zile kwa Tsh 17M? Kweli?

Serikali imesema itawauzia kwa Tsh 48M (chumba na sebule) na 56 + (kwa nyumba kubwa), na hii inalipwa kwa muda wa miaka 15.

Piga mahesabu yako vizuri kwa huyu atakaye lipa 56+ atatakiwa kulipa laki tatu tatu kila mwezi kwa muda wa miaka hiyo 15

Hii si bei ya kodi ya mwezi kabisa ya nyumba ya hadhi hiyo? Naona hawaoni uzito wa mali hii wanayotaka kumilikishwa kwa mteremko!

Huijui serikali wewe

Hizo bei wanazozisema mwanzo. zinakuwa na interest kila mwaka.

Uliza watu walionunua nyumba za nssf ama NHC wanavyoshangaa deni linapandiana tu.

Ukitaka uzifaidi hizo bei ni uwe na hela cash.. usinunue kwa kulipa kidogo kidogo
 
Back
Top Bottom