Kauliza muulizaji kwanini majina ya Waasisi wa African Association hayapo katika historia ya TANU

Mohamed Said

JF-Expert Member
Nov 2, 2008
20,921
30,264
KAULIZA MUULIZAJI: ‘’KWA NINI MAJINA YA WAASISI WA TANU 1954 YAPO KATIKA HISTORIA YA UHURU WA TANGANYIKA LAKINI WAASISI WA AFRICAN ASSOCIATION 1929 HAYAONEKANI POPOTE?’’

Kijana alichonitafutia ni historia ya Muungano wa Tanzania mwaka wa 1964.

Akanifahamisha kuwa amesoma kitabu cha historia ya muungano kilichoandikwa na Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania (2022).

Katika kitabu hiki alikuta orodha ya majina ya waasisi wa TANU lakini hakuona majina ya waasisi wa African Association.

Ametafuta kwingi lakini hakuweza kuyapata majina hayo ya waasisi wa African Association.

Kauliza kwa nini majina ya waasisi hawa hayapo na kama nayajua majina yao.

Jibu langu kwake ni kuwa swali hili kalileta sipo alistahili kuwauliza CCM swali hili kwani wao ndiyo warithi wa historia ya TAA na TANU vyama vilivyotokana na African Association.

Nilimjibu hivyo na nikamueleza kuwa mimi nayajua majina ya waasisi wa African Association na mengine lakini itakuwaje ikiwa CCM wakayakataa majina hayo kuwa si ya waasisi wa African Association?

Kijana akasisitiza kuwa angependa kuyaona majina ambayo mimi ninayo yamsaidie katika utafiti wake wa historia ya muungano.

Kwa faida ya wanafunzi wa historia ya uhuru wa Tanganyika naweka hapo chini majina ya waasisi wa TANU na chini yake naweka majina ya waasisi wa African Association taarifa nyingine muhimu katika historia ya TANU:

Waasisi wa TANU 1954:

1. Mwalimu Julius Kambarage Nyerere
2. Germano Pacha – Jimbo la Magharibi
3. Joseph Kimalando – Jimbo la Kaskazini
4. Japhet Kirilo – Jimbo la Kaskazini
5. C.O. Milinga – Jimbo la Mashariki
6. Abubakari Ilanga – Jimbo la Ziwa
7. L.B. Makaranga – Jimbo la Ziwa
8. Saadani A. Kandoro – Jimbo la Ziwa
9. Suleman M. Kitwana – Jimbo la Ziwa
10. Kisung’uta Gabara – Jimbo la Ziwa
11. Tewa Said Tewa – Jimbo la Mashariki
12. Dossa A. Aziz – Jimbo la Mashariki
13. Abdulwahid Sykes – Jimbo la Mashariki
14. Patrick Kunambi – Jimbo la Mashariki
15. Joseph K. Bantu – Jimbo la Mashariki
16. Ally Sykes – Jimbo la Mashariki
17. John Rupia – Jimbo la Mashariki

Waasisi wa African Association 1929:

1. Cecil Matola (President)
2. Kleist Sykes (Secretary)
3. Mzee bin Sudi
4. Ibrahim Hamisi
5. Zibe Kidasi
6. Suleiman Majisu
7. Ali Said Mpima
8. Rawson Watts
9. Raikes Kusi

TAA Political Subcommittee 1950:

1. Dr. Vedasto Kyaruzi (President)
2. Abdul Sykes (Secretary)
3. Mufti Sheikh Hassan bin Ameir
4. Sheikh Said Chaurembo
5. Hamza Mwapachu
6. Steven Mhando
7. John Rupia

TAA Executive Committee 1953:

1. J.K. Nyerere (President)
2. Abdulwahid Sykes (Vice-President)
3. J.P. Kasella Bantu (General Secretary)
4. Alexander M. Tobias na Waziri Dossa Aziz (Joint Minuting Secretary)
5. John Rupia (Treasurer)
6. Ally K. Sykes (Assistant Treasurer)
7. Committee Members: Dr Michael Lugazia, Hamisi Diwani, Tewa Said, Denis Phombeah, Z. James, Dome Okochi, C. Ongalo na Patrick Aoko.

(Tanganyika Standard 19 June, 1953)

1711578031997.png

1711578155096.png

Hamza Mwapachu (1913 - 1962)
Abdulwahid Sykes (1924 - 1968)
1711578292316.jpeg

Sunday News 20 October 1968
 
Kina Sykes unyama ni Mwingi sana ,kila sehemu wapo hao.
King...
Baada ya mimi kuandika kitabu cha historia ya maisha ya Abdul Sykes Oxford University Press, Nairobi wakanitia katika mradi wa kuandika historia kwa ajili ya shule za msingi.

Mradi huu ni wa kusomesha lugha ya Kiingereza na Historia kwa wakati mmoja kupitia vitabu vitakavyoandikwa.

Nimeandika kitabu, "The Torch on Kilimanjaro," (2007).

Oxford University Press, New York na Harvard wakanitia katika kuandika Dictionary of African Biography (2011) nikaandika historia ya Kleist Sykes.

Kitabu cha Abdul Sykes kimebadili historia ya uhuru wa Tanganyika na historia ya Julius Nyerere kuunda TANU na kupigania uhuru wa Tanganyika.
 
Uasisi wa TANU hauna uhusiano wowote na uasisi wa African Association. Ni Kama ambavyo uasisi wa vyama vya Shiraz Party na African Party hauna uhusiano na uasisi wa CCM ingawa vyama hivyo ndivyo viliungana na kuwa ASP ambayp nayo baadaye iliungana na TANU kuwa CCM, lakini mazingira ya uanzishwaji wa CCM hayakutakona na mazingira ya unanzishwaji wa Agrican Party au Shiraz Party.

African Association ilitransfrom kuwa Tanganyika African Association kabla ya kuwa transfromed tena kuwa TANU. Zilioperate katika mazingira tofauti na malengo tofauti
 
Kichuguu,
Mimi huwa sifanyi ubishi kwani ubishi hauna tija yoyote.

Mimi hupenda kusomesha yale ambayo si wengi wanayajua.

Ikiwa wewe unaona African Association haina uhusiano na TAA na TAA haina uhusiano na TANU sitakubishia.

Sikubishii kwa kuwa hadhira yangu ni kubwa na ina wasomaji na wanafunzi wengi ambao wananufaika na ninayoandika katika historia ya uhuru wa Tanganyika.

Lakini umeona African Association imenzishwa 1929 Kleist Sykes Katibu Muasisi.

1948 African Association ikabadili jina na kuwa Tanganyika African Association (TAA) Abdul Sykes katibu na mjumbe katika TAA Political Subcommittee mwaka wa 1950.

Mwaka wa 1953 Nyerere akachaguliwa kuwa Rais wa TAA na Abdul Sykes Makamu wa Rais; mdogo wake Ally Sykes Makamu Mweka Hazina.

Mwaka wa 1954 TANU ikaundwa na Abdul Sykes na Ally Sykes ni kati ya waasisi 17 wa chama cha TANU.

Katika hayo hapo juu kuna historia ya kusisimua ambayo nimeiandika katika kitabu cha Abdul Sykes.

Kinachomstaajabisha kila msomaji wa kitabu hiki ni kuwa historia ya TANU imeandikwa na hayo waliyosoma kutoka kwangu hayamo.

Leo kitabu changu si tu kimebadili historia ya TANU bali hata historia ya Mwalimu Nyerere.

Angalia video hiyo hapo chini nikizungumza na Afisa kutoka Makumbusho ya Taifa:


View: https://youtu.be/wO86ftnPSa4
 
Tatizo una ajenda yako ya siri ambayo haina maslahi kwa taifa.
 
Tatizo una ajenda yako ya siri ambayo haina maslahi kwa taifa.
Yoda,
Sina agenda yoyote ya siri.

Mimi si mtu wa kwanza kuandika historia ya wazee wangu.

Labda wewe hukuipenda historia hii kwa kuwa kuwa imedhihirisha historia iliyokuwa ikidhaniwa ni kweli si ya kweli ilipotoshwa.

Hawa walioandika historia ya uongo wakaisomesha na kuieneza pote hawa ndiyo waliokuwa na agenda ya siri.
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom