Kauli za waziri mkuu ni tata au ni nini?

Ringo Edmund

JF-Expert Member
May 10, 2010
4,879
1,125
Toka ateuliwe kuwa waziri mkuu mh mizengo pinda amewahi kutoa kauli nyingi sana ndani na nje ya bunge baadhi nazikumbuka na baadhi nimezisahau na kuna ambazo labda sikufanikiwa kuzisikia.
ila kwa zile ninazokumbuka kama ni za kuelekeza zimekuwa hazifanyiwi kazi sijui ni makusudi au ni kuwa hazitekelezeki au hazina uzito?
1.wanaoua maalbino nao wauawe.
hii kauli haijafanyiwa kazi mpaka leo kiasi cha kujiuliza alikuwa anatania au alikuwa anamaanisha.swali linalokuja hapo je alitaka serikali ndo iwaue au wananchi?

2.ningekuwa na uwezo ningemfukuza jairo.hili sijui limetekelezwaje ila linafanyiwa kazi.

3.katibu mkuu wa wizara ya afya na mganga mkuu ninawasimamisha kazi kwa sababu wako kwenye uwezo wangu ila waziri na naibu namsubiri rais.hapo napo kuna walakini jairo na blandina wanateuliwa na rais iweje mmoja uwe na uwezo nae na mwingine ushindwe?

4.ninalirudisha gari niletewe la gharama nafuu zaidi.hapo wadau naombeni msaada.

5.

6.

7.

kauli ni nyingi.

naombeni mnaozikumbuka zilizotekelezwa na ambazo zimeshindikana mzilete hapa tuzijadili.
 
marufuku serikali kununua magari ya kifahari matokeoa yake yakanunuliwa magari karibu 65 yenye zaidi ya mil 200..akapewa moja akagoma kulitumia akaagiza mtu wa chini yake alitumie...
 
Tatizo ni kuwa PM wetu hakuzoea kusema uongo, maana ili uwe mwongo kamili lazima uwe na uwezo mkubwa wa kumbukumbu, kukosa uzoefu huo na kubanwa na mafisadi ambao wanamlazimisha kufanya ndivyo sivyo ndilo tatizo kubwa hapo.
 
Back
Top Bottom