Kauli za Rais zinavunja moyo watendaji wake

Hivi hawa wamachinga ndio wapiga kura wake tuu. Na sisi wengine ambao hatu wesi tembea kwa miguu kkoo sasa, hataki kura zetu?
 
Rais wetu kwakweli ana nia yadhati yakuwasaidia masikini ila kwahili naona amekurupuka au ameshauriwa vibaya.
kitaalamu wamachinga hawalipi kodi kwasababu nivigumu kumpata na hata ukiweka mikakati yakumpata utatumia garama kubwa sana zaidi yakodi utakayokusanya hivyo nihasara.

kwakauli ya Rais manake ameongeza mwanya wa watu kutokulipa kodi.
 
Kwa jambo hili Mkuu wetu amekosea sana. Nadhani hata hao washauri wake wa karibu wanashindwa kumshauri maana ana jazba sana. Unaweza kuwa na nia ya kumshauri ukajikuta umefutwa kazi pasipo sababu.
 
Nimeshangazwa sana na huu uamuzi kwa kweli. Haya majiji na miji itakuwa michafu sana.
 
mimi naona dawa si kukurupuka kuwafukuza au kuwaacha apo apo wafanye biashara, mwarovera ni kutafuta suluhisho la kudumu.

Suluhisho ambalo halitaathiri shughuli zao, shughuli za wenye maduka na watumiaji wa barabara.
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom