Kauli ya Rais Kikwete juu ya milipuko ya Mabomu Gongo la Mboto

Ni kweli mimi kuna mjeshi alinambia Gongo la mboto kuna mabomu heavy duty pakilipuak dar yote yaweza kuteketea by then he was refering to Mbagara. Anasema kuna mabomu yanaweza piga mpaka Morogoro na yamechakaa. Nadhani gongo la mboto ndo ghala kuu la hizo silaha. Twafa... Tusiwahurumie wa G/mboto tu we are not sure what next na kama kweli huko G/mboto hali ni shwari kweli kwani I don't trust a single word that comes fro these politicians
JK Kasema kweli sio uongo,si uliona Slaa alivyomchemsha kidogo tu kuwa ni mmiliki wa dowans, kaongea hadi mambo ya siri, mara Msabaha aliniomba niwashinikize hazina kulipa down payment $10M kwa Richmond
 
Kesho mtarajie Picha kuuuubwa front page Daily News, Mtanzania na Habari leo ikimwonyesha JK akisalimia majeruhi au akizungumza na Majenerali wa Jeshi.

Lengo kuonyesha yuko karibu na wananchi wake.

Hivi kwa nini mabaya huwapata wanyonge tena walio wema huku watesi wakiendelea kutesa??? Kwa nini mabomu yanaiogopa au kuikwepa Ikulu???

Inaniuma kwa sababu nimekesha nawatafuta niece wangu (Kulwa na Dotto) wenye miaka 11. Tumekanyaga kote kuanzia U/taifa, vituo vya polisi, Hospitali ya Amana na Muhimbili lakini hakuna majibu.

Eti leo viongozi wachukue ujiko kwa madhira waliyasababisha wao wenyewe.

Pole sana, Mungu awatunze hao niece wako pamoja na watoto / watu wengine. Pia Mungu awasaidie kupata amani na utulivu wa moyo wote walioathirika. Walioumia wapone haraka na waliofiwa wapate faraja. Inasikitisha sana!!!! Tunawakumbuka na kuwaombea katika wakati huu mgumu.
 
Regam hayo ni magalika anayoleta Mungu mpaka Farao hawahache watoto wake waende. Atapiga moja baada ya jingine mpaka CCM watalegea wenyewe watuachie nchi yetu.

inchi yetu ni ya amani na utulivu uliotukuka. haya mabomu ni ajali tuu kwani walitueleza kuwa baada ya mabomu ya mbagala hakuna milipuko mingine itakayo tokea. sasa tunajiuliza hii tume itakayo undwa itakuja na lipi jipya?
hii tunayojivunia (eti amani na utulivu) ndo inatugharimu sasa. sisi watz ni mambumbumbu, wanafiki, waoga, wajinga, wa*****. laiti kama haya yanayotokea yangetokea nchi zingine sidhani kama yangevumilika. (mabomu, umeme, bei za bidhaa juu, ufisadi, uchakachuaji wa kila kitu n.k) haya yanatosha kabisa kuishinikiza serikali kuondoka madarakani. kweli yaliyosemwa kuwa nchi haitawaliki yanaanza kutimia. najaribu kupika picha kama ningekuwa ndio jk, akianani ningeondoka tuu! kwani nini bana?
 
Majeshi yetu yamekuwa yakijishughulisha na siasa mno, na kusahau wajibu wao na matokeo ndio haya.
 
Inatia uchungu...wakati fulani ni ngumu sana kuamini kuwa watu wamejengwa kifikra hata kuweza kumsingizia Mungu kwa kila linalotokea, eti "ni Mapenzi ya Mungu" au kumsingizia mtu anaeitwa bahati mbaya..hapana. Tumezoea kusema "afanye maamuzi magumu", sasa kama ameshindwa kufanya maamuzi magumu, tunasubiri nini hasa kishuke kutoka juu (kama kweli ni mapenzi ya...) ndo kituambie ameshindwa kufanya maamuzi magumu..na hivyo bora kufikiria vinginevyo..hayo maamuzi magumu yarejee kwetu sasa..maana sijui nani tena atakuja kusema na sisi tumeshindwa kufanya maamuzi magumu!..pole kwa wote waliopatwa na masahibu, na waliofariki warehemiwe.
 
Hakika wapo watanzania ambao uwezo wao ni mdogo hata kufikia kushindwa kutofautisha malengo na sababu za JK kwenda kushuhudia yaliyotokea Gongo la mboto. Kilichotokea gongo la mboto na Mbagala siyo mara ya kwanza kutokea hapa Duniani na imekuwa ikitokea katika nchi zilizoendelea pia kama vile India, Russia, Germany.

JK haendi kugawa fedha anakwenda kuwapa pole waliofikwa na janga pamoja nakujionea hasara iliyosababishwa na mabomu hayo kwa kuwa yeye anawajibika kwa kila Mtanzania ikiwemo wewe mwenye uwezo finyu , Kama akili zako zinakutuma kwamba watendaji wabovu ndiyo wamesababisha janga hili basi nakusihi uende kuanza chekechea kabisa kwa kuwa kwa sasa huna la kuchangia zaidi ya kuishia kulalamika lalamika pasipo kujiuliza na kutafakari mambo.

Wewe ndio punguani kweli kweli.
Janga kama hilo lilishatokea huko mbagala miaka miwili iliyopita na ikaundwa tume ambayo ilitumia mamilioni ya kodi zetu.

Lengo la tume lilikuwa ni kutafuta chanzo cha janga hilo na kutoa mapendekezo nini kifanyike ili janga kama hilo lisitokee tena hapa nchini. Tume ilifanya kazi iliyotumwa na ikakabidhi ripoti yake kwa wahusika.

Bahati mbaya wananchi hatukufahamishwa kilichomo ndani ya ripoti hiyo lakini Waziri wa Ulinzi pamoja na mkuu wa majeshi walituthibitishia kuwa milipuko kama hiyo haitatokea tena hapa nchini.

Sasa ni miaka miwili tu tangu watuthibitishie hivyo inatokea milipuko mingine na kuua raia wema huku ikiwaacha mamia wakiwa vilema na wengine bila makazi. Kama hadi hapo huoni kuwa wahusika wanapaswa kujiuzulu basi wewe ni mbumbumbu.
 
great thinkers
no research, no right to speak.
Tafakari kbala ya kutenda.
Hizi ni fact au chuki binafsi kwa jk
wacheni kumsakama jk bila ya kuwa fact

what to research? what still remain known after all three past events of the same kind? you want to waste time by researching the obvious?
 
Majeshi yetu yamekuwa yakijishughulisha na siasa mno, na kusahau wajibu wao na matokeo ndio haya.

hasa shimbo, nilitegemea kama yeye ni askali na kweli anapenda amani ya Taifa hili idumu basi hasingeruhusu uzembe wa kusababisha watu kuuawa kwa mabomu.
Lkn nahisi sasa hawa askari wa chini akiri itaanza kuwaingia hasa wanapoona wao wanakufa na raia wanakufa tu bila sababu, watajua wanavyotumika bure kuwakinga akina shimbo, mafisadi na wanasiasa wachakachuaji!
Naamini ndani ya jeshi bado wamo wazalendo na wapenda amani na maedeleo ya WaTZ!!
 
Nimeona picha eti katika suti kwenye maafa JK bana

RAIS%2BJakaya%2BKikwete%2Bakizungumza%2Bna%2Bwaandishi%2Bwa%2Bhabari%2Bbaada%2Bya%2Bkukagua%2Beneo%2Bla%2Btukio%252C%2Bkambi%2Bya%2BJWTZ%252C%2BUkonga..JPG
 
JK anasema hakuna mabomu bali hayo ni maneno ya Redio Mbao tu; ametuasa tusisikilize Redio Mbao. Sikumwelewa kwa vile ametumia kiswahili kigumu sana eti RADIO MBAO. Niliwahi kwenda ku-Google Radio Mbao nikaipata hapa www.radiombao.com, lakini bado sielewi kama hiyo ndiyo RADIO MBAO ambayo Rais alituzuia tusisikilize kwa vile mimi mwenyewe sijawahi kuiskiliza, sijui ndugu zangu huko vijijini kama nao wanaweza kuisikiliza hiyo RADIO MBAO kwa vile najua kuwa wao hawana intanet
 
Anglia global publishers inaonyesha alivyokuwa anamkoromea mwandishi aliyetaka kumpiga picha akamwambia asikilize asipige picha na baadae akacheka kidogo.
 
Back
Top Bottom