MKATA UFUTA
Member
- Jul 1, 2012
- 21
- 3
Mimi ninataka niseme ukweli kwa sababu siogopi mtu, mimi ni taasisi inayojitegemea, sina imani na wewe mwenyekiti (Meya wa Jiji la Mwanza), umekuwa hufuati kanuni, utaratibu wako wa kuendesha vikao kila mara unataka kusababisha vurugu, ninataka baada ya hapa nipewe karatasi mimi nitakuwa wa kwanza kuandika jina langu ili nipate idadi ya madiwani 10 wanaoweza kuleta hoja kuomba tukupigie kura ya kutokuwa na imani na wewe, alisema diwani huyo kijana.
Habari zaidi soma hapa Raia Mwema - CHADEMA yatikisa mashabiki wake
Hii ni kauli ya Chagulani kwenye Kikao cha Baraza la Madiwani wa Jiji la Mwanza alipowataka Madiwani wapige kura ya kutokuwa na imani na Meya wa Jiji hilo Bw. Josephat Manyerere (CDM). Kwenye orodha ya waliosaini kumpiga chini meya Manyerere jina la Chagulani ni la kwanza, kisha linafuatiwa na mwenzake Matata halafu wanafuata madiwani wa CCM na CUF. Hakuna jina la diwani mwingine wa CDM aliyesaini.
My Take:
1. Ni Kweli Chagulani hakutakiwa kuogopa wala kujali chochote na kwamba yeye ni taasisi inayojitegemea? Hana taasisi (Chama) kilichomu-endorse ambacho alipaswa kuongozwa na katiba, sheria na taratibu zake? Si kwamba, hii ni jeuri kuu ambayo haieleweki ni wapi inatoka?
2. Kwa nukuu hii si kwamba, Bw. Chagulani alikuwa anatekeleza mradi aliotumwa na CCM? Kitendo cha yeye kuanza kwa kujihami kuwa, haogopi mtu na kwamba yeye ni taasisi huru inayojitegemea kinatafsiriwa wazi, alikuwa na maelekezo kichwani kutoka kwa chama chake yaani CDM lakini alikaidi makusudi pengine ni kutokana na yeye kuwa na mradi aliokuwa anautekeleza (Bila shaka kuupata umeya/malipo kutoka CCM)
Tujadili.
Mnyonge mnyongeni ila haki yake mpeni. Na kwamuungwana ni ngumu nyeusi kuita nyeupe!! Hivi kunamkazi gani wa Mwanza asiyejua madudu yaliyofanywa na aliyekuwa meya. Think Deep CHADEMAS!!! Mbona baada ya kukemewa na CHAGULANI, baadae Meya alioondolewa? Tatizo walitaka eti Meya akaripiwe kwenye vikao vya chama. Hivi huyu Meya si alichaguliwa katika vikao vya madiwani? Kwanini asiwajibike kwao? Stahili hii ya vikao vya chamani kwenye utekelezaji wa taratibu za madiwani, hivi inatofauti na vikao vya ndani vya wabunge wa CCM ambavyo vimekuwa kiini cha kulinda mafisadi bungeni?
MIMI nimeanza kuogopa sasa!! Kwani hapa inaonekana kunya anye kuku akinya bata kaharisha. Tuliiondoa CCM tuwe na taratibu mpya za uedeshaji mambo. Ambapo Tanzania kwanza, Chama baadae.
NDUGU mtoa mada, tafuta ukweli na jiepushe na mlengo, kwani chadema tunaamini katika ukweli. Na ukweli ni kuwa CHADEMA mwanza kuna mgogoro. Issue si Chagulani wala Matata, Tuutafute UKWELI kwa ustawi wa TZ na CHADEMA