Adam wewe kama msomi ulipaswa ujue nini cha kusema na wapi. Nimewahi kuwa kiongozi wa mradi kwa kitaifa unaofanyika kimataifa nijuavyo mimi katibu/mtendaji ndio anashauriana na mwenyekiti kuitisha vikao, mara nyingi ratiba ya vikao huwa inajulikana hivyo mtendaji muda ukikaribia humwalifu mwenyekiti ili waweze kutekeleza ratiba. Ukiona mwenyekiti ndo anakuwa mbele sana, bila mtendaji ujue ni ktk hali ya dharura na ukweli ni migongano ktk uongozi. Mikutano ya kawaida ya h/w inabidi CD/DED atoe taarifa sasa kama taarifa hazipo meya ataitisha kikao ili diwani aje kuchukua posho kisha aaondoke???? kwa hiyo ni muhimu sana CD kuhusika ktk mipango ya vikao, anawasiliana na meya kwa maana ya kufix tarehe na mambo madogomadogo kama yapo;
Zaidi Adam kama uliona meya anapwaya au anafanya vivyo isivyo ulipaswa kumshauri meya kwanza nje ya vikao, ndani ya vikao vya chama, kumshitaki ngazi za juu za chama, na kama hupati msaada wowote na hali inazidi kuwa mbaya ndipo umwage kwenye vikao vya wananchi/baraza la madiwani ambalo ni la wazi.
Ni kuulize swali kama meya anapotoshwa na CD tunafanyaje??? maana umeya sio taalum, CD ndo amempelekea meya asaini huku akijua meya anahitaji baraka za baraza, kwani nini cd asipewe onyo kwa makosa hayo??? tumeona hata kwa rais wa nchi, meya ni rais wa h/jiji la mwanza, iweje mtendaji amtegesheeee huoni hila hizo za KICCM CCM??? CD ni mdhoefu sana wa miaka na miaka wa vikao vya madiwani na mamlaka yake meya ni mgeni kabisaaa, dhamana kubwa hasa mambo ya kisheria ya uendeshaji wa jiji ni CD, kama anampotosha meya apigwe chini.
Kuhusu mtendaji wa kata, kwanza sio vema kwa msomi kuchagua mtu wa kufanya nae kazi, huo nao umeonesha udhaifu. pili kama mwanachadema unajua CCM haina watu hata ukibadilisha vipi, sasa unalalamika kuhusu WEO atatoka wapi??? ni mpaka wananchi wapige chini kabisa CCM ndo mambo yanyoke 100% kwa sasa tunalazimika kufanya nao kazi hivyo hivyo tukisubiri uamuzi wa wananchi 2015. au nawewe unataka uletewe WEO mpenzi wako???? nani amekuhakikisha atakayekuja ni mzuri kuliko aliyepo???
Kwenye siasa fitina ni siasa, unapaswa uzishinde na wala sio kutulalamikia kuwa unafanyiwa zengwe, siasa ni zengwe amini usiamini; maana hata ndani ya chama kunawatu wanataka nafasi yako achilia mbali nje ya chama. na ni haki yao, so kuwa smart kushinda fitina za siasa, acha kukurupuka utanasa kwenye mtego; i mean himili mkiki ya siasa na usilalamike kuhusu zengwe, maana hata wewe unafanya mizengwe kwa upande mwingine. Ukiona unaelemewa unapaza sauti, hakuna wa kukuonea huruma pigana na kuwa smart it will work.
Fumagila nimefika maana nilifanya siasa mwaka 2010, nakuunga mkono daraja hilo lijengwe tena kuwa mwehu kabisa; ila usipoteze sheria za mchezo wa siasa; tumia wananchi daraja litajengwa. Na kwa kutumia forum hii nimtake meya ajenge daraja hilo kwa bajeti ya mwaka huu, kama atapuuzia haya.
Mwisho maana sitaki nikujibu hoja zote, kuwa makini hasa na watu unaunda kundi nao, i repeat kuwa makini; ndani yake wamo vijana wa CCM/serikali; nimekuona nao, nawafahamu siku mingi sana na wananifahamu. Nimewaona kwenye kundi lako tena wanachangia sana hoja. Na hapo ndo wasiwasi wa shughuli zako uliponiijia, wale vijana ni smart guys be careful labda kama nawe wewe ni mmoja wao. JUA KUWA NGUVU YA UMMA inatokana na umma wenye nguvu; Watanzania kwa sasa wamejenga umma wenye nguvu.
kula like yangu mzee.