Kauli hizi za Zitto zinatupa picha gani?

Lengeri

Senior Member
Jul 3, 2009
180
15
wana jf hizi hapa chini ni baadhi ya kauli za mbunge kijana Zitto ambazo amezitoa nyakati tofauti

jee kwa kauli hizi Credibility yake i wapi??
je Zitto Anaaminika kama kiongozi thabiti??


1st September 2009, 02:15 PM

Ndugu zangu,

Katika kipindi hiki sikutaka kabisa kuingia na kujibu hoja yeyote ndani ya JF kuhusiana na uchaguzi wa vijana Taifa. Hata hivyo mtaniwia radhi kujibu hili ili kuweka rekodi sahihi kutokana na upotoshaji ambao unafanyika kwa makusudi kabisa ili kushusha heshima yangu katika jamii.

Moja, mimi ni mumbe wa Baraza la Vijana la CHADEMA kwa nafasi yangu ya kuwa mjumbe wa Kamati Kuu wa kuchaguliwa kuwakilisha vijana na nikiwa Mbunge mwenye umri wa ujana (miaka 33). Hivyo kushiriki kwangu kwenye vikao ni jambo la kawaida kabisa kwani nina haki ya kupiga kura. Vile vile nina haki ya kuamua mgombea gani wa kumuunga mkono katika uchaguzi. Niseme waziwazi kuwa David Kafulila ndiye mgombea niliyemwunga mkono na kumfanyia kampeni waziwazi bila kificho chochote kile. Hii inatokana na tabia yangu ya kutokuwa mnafiki. Nilimwunga mkono David Kafulila na alishinda kwa kupata kura 99 dhidi ya kura 73 ambazo alipata mgombea mwingine John Heche ambaye alikuwa anaungwa mono na kundi lililonipinga kuwa Mwenyekiti wa CHADEMA Taifa.

Huyu aliyeandika post hii ni mmoja wa vijana wa makao makuu ya CHADEMA ambaye amekuwa akinipinga siku zote kwa chuki tu ya kuwa mimi nimepaata umaarufu wa kisiasa kuliko yeye na kundi lake.

Mama yangu mzazi ni mwanachadema. Ni kiongozi mwandamizi wa CHADEMA kutoka mkoa wa Kigoma na amekuwa msaada mkubwa wa chama katika Manispaa ya Kigoma. Ninaomba sana masuala yangu ya kisiasa na mahasimu wangu wasimhusishe mama yangu mzazi. Ninaomba sana sana mumuweke mama yangu pembeni. Mwandishi wa post hii tafadhali naomba usimhusishe mama yangu na tofauti zetu za kisiasa. Ninaomba sana hili liheshimiwe.

Pili, ni dhahiri kulikuwa kuna makundi katika uchaguzi wa BAVICHA. Mimi niliweka wazi msimamo wangu wa kumwunga mkono kafulila. Wakurugenzi wa Makao makuu ya chama kuanzia Katibu Mkuu mpaka wakurugenzi kama John Mnyika, John Mrema na hata maafisa kama Halima Mdee walikuwa wanampinga David Kafulila. Hawa wanaogopa uwezo wa Kafulila wa kukataa kutumika na kuwa independent katika maamuzi yake.

Hii sio mara ya kwanza kwa Kafulila kuzuiwa haki yake. Kijana huyu alipitishwa kugombea Ukurugenzi wa vijana na jina lake kwenda katika Kamati Kuu. Ajenda ya uteuzi wake ikasitishwa baada ya kuhofia kuwa atashinda. Mtindo huo huo wameutumia sasa kufuta uchaguzi na kuupeleka mbele mpaka baada ya miezi 6. Mimi nimekataa

1. Uchaguzi umefanyika.
2. Matokeo hayakutangazwa
3. Hakuna aliyekata rufaa

Hivyo, wazee wanapata wapi 'locus' ya kufuta uchaguzi?

Hata hivyo wenye mamlaka ya kufuta uchaguzi ni Kamati Kuu ya chama maana kuna taratibu za rufaa ndani ya chama chetu. Nimetaka Kamati Kuu iitishwe ili taratibu zifuatwe.

Huyu mtu aliyeleta post hii hapa anataka kuspin ili kupinda ukweli bila aibu.

David Kafulila kashinda round ya kwanza zaidi ya 50%. Wamekataa kutangaza matokeo na kuleta fujo kwenye mkutano.

Kuna tuhuma dhidi yangu kuwa nimetoa rushwa. Huku ni kutapatapa kwani tuhuma hizi zinatolewa bila ushahidi. Hivi huyu mwandishi na akili zake timamu anaweza kuweka akilini kwake kuwa mimi naweza kutoa rushwa hadharani? Eti nimevuta kiti na kuita watu kutoa rushwa. Bila adabu anamhusisha mama yangu mzazi.

Mama yangu ana maamuzi yake binafsi na mfano dhahiri ni uchaguzi wa chaha wangwe ambapo mimi nilimwunga mkono arfi na yeye akamwunga mkono Chacha wangwe waziwazi na bila kificho.

Uchaguzi wa vijana haukua na rushwa. Uchaguzi wa vijana wa chadema umefanyika kwa amani kabisa na matokeo hayakutangazwa kwa kuwa mgombea 'wao' hakushinda.

Wanasema eti Mtemelwa aliyekuwa ananiunga mkono alishindwa Temeke. Hawasemi watu waliowatuma kwa kutumia fedha za chama kugombea mikoa 15 na kutupwa chini na watu wanaoniunga mkono. Ukiwemo mkoa wa Dodoma na Shinyanga ambao walitumwa wakurugenzi wa chama kama Benson Kigaila na Erasto Tumbo na kushindwa. Habarindiyohiyo nakuomba ukumbuke kuwa baada ya uchaguzi kinachofuata ni ukaguzi wa fedha za chama katika kipindi hiki na jinsi zilivyotumika. Nashukuru Mungu kuwa ukaguzi huo sasa utafanywa na CAG

Katika spirit ya umoja na mshikamano wa chama tutamaliza suala hili katika Kamati Kuu ya chama.

Ninaomba sana vijana wa Makao Makuu - hasa Mrema, Mnyika na wengineo waache spinning za kipumbavu ambazo hazijengi umoja na mshikamano wa chama. Waache kuchafua jina langu. Wakumbuke kuwa kuna maisha mbele yetu na kuna kazi ya kujenga chama chetu.

Vijana hawa wakumbuke kuwa majungu hulipwa hapa hapa duniani. Wasubiri nao watakuwa wabunge na watapata ajenda zao za kuwafanya kuwa maarufu.

Wakumbuke pia mimi na Mbowe tunafahamiana kabla yao na tutakaporekebisha tofauti zetu na kugundua wapambe nuksi watakuwa kwenye aibu kubwa. Dunia hadaa!

Haya ambayo nimeyaandika hapa JF nimewaambia vijana hawa 'face to face' ili waache uwongo, uzandiki, majungu, fitna na chuki.

Kafulila kashinda uenyekiti wa vijana. Mpeni ushindi wake. Msibake demokrosia.

Poleni wana JF. Haya hayakuwa ya hapa lakini imebidi. Mwenyekuelewa kaelewa.

1st September 2009, 02:30 PM

This is part of spinning. Uwongo, uzushi nk. Tatizo wanaopanga haya wanasahau kuwa tuliyapanga wote dhidi ya marehemu Chacha Wangwe. Unatengeneza uwongo, unausambaza, na hatimaye wewe mwenyewe unauamini kuwa ni kweli.

Kama kuna kitu kilimuuma marehemu wangwe na alikufa nacho ni kile cha kumsema kuwa alikuwa anatumiwa na mafisadi. Namshukuru Mungu kuwa nilimwomba radhi Chacha kabla na baada ya kifo chake siku ya postmorterm kwa kumzushia uwongo.

Asha ni mmoja wa wenzangu tulioshiriki kumtenda Chacha. Wanatumia mtindo ule ule na wanapita njia zile zile. Rashidi wa Kuli alisema, YANA MWISHO HAYA!

Asha, (ninakujua wewe ni nani) kuwa mkweli wa nafsi yako! Utalipwa hapa hapa duniani kwa uzushi wako na wenzako.

To put record clear - Kasisiko sio ndugu yangu wa damu. Ni mwenyekiti wangu tu wa Mkoa Kigoma. Pili, Baregu hajahudhuria kikao hata kimoja cha wazee toka ajue ukweli wa mambo.

Tatu, chama jana kimechagua rasmi Baraza la Wazee na mgombea aliyekuwa ananiunga mkono waziwazi ameshinda. Inakuwaje bado vikao vya wazee vya chama vinaendeshwa na Mtei na Ndesamburo?

Pili, vyombo vyote vya habari vilikuwapo katika hotuba ya Mtei. Imekuwaje NIPASHE peke yake ndio ione alisema kuna ufisadi kwenye chaguzi za chama? Mhariri mtendaji wa Nipashe ni jesse kwayu kutoka Machame. Mmiliki wa Nipashe ni Reginald Mengi kutoka Machame.

Spinns sio sustainable. Acheni tujenge chama chetu.

2nd March 2007, 01:51 PM
Imenibidi kujisajili kwa jina langu halisi ili niweze kujibu baadhi ya hoja humu ndani ya forum.

Ninaiamini sana forum hii ndio maana ikipita siku sijasoma hoja za humu ndani najiona nimekosa kitu.

Nina heshimu mawazo ya watu wote kuhusiana na uamuzi wangu wa kutogombea ubunge mwaka 2010.

Kama mwanasiasa alivyosema huu ni uamuzi nilioufikia toka mwaka jana mwezi wa nane baada ya Bunge la Bajeti. Nilipopata nafasi ya kufanya mahojiano na gazeti la Sunday News nilisema azma yangu hii. Makala ile ilirushwa humu ndani ya forum na baadhi ya watu kuijadili kidogo.

Sina la kusema la zaidi ya Mwanasiasa, ni kama yupo ndani ya kichwa changu. Ndivyo, nahitaji uzoefu katika management. Sina uzoefu huo maana nimefanya kazi kwa mwaka mmoja tu toka nimalize masomo nchini Ujerumani. Hata kazi hiyo katika shirika la FES ilikuwa ninaongoza mradi wa sera za biashara ya kimataifa. Nilikuwa naongoza ofisi yangu mwenyewe na sikuwa na watu chini.

Inabidi nifafanue baadhi ya masuala maana habari hii ya kutogombea imewakwaza watu wengi sana wakiwemo viongozi wangu wa chama. Leo hii asubuhi nimetoka kuongea kwa simu kwa muda wa dakika 45 na Mheshimiwa Ndesamburo akinitaka niachane na mawazo hayo.

Jana nilisononeka sana baada ya kusikia sauti ya mwenyekiti wangu Mhe. Mbowe akinilalamikia ni kwa nini nimefikia uamuzi huo. Wote wanasema ninavunja nguvu watu wanaotaka kugombea kwa sababu mimi nimevutia vijana wengi sana katika siasa. Ni kweli nakubaliana na hoja zao wote. Na ninaomba radhi kwa wanaokwezeka na uamuzi wangu wa kutogombea.

Moja, nimeshawahi kusema huko nyuma kuwa mimi sina bei (i have no price tag). Mtu yeyote anaejenga hoja zake juu ya uamuzi wangu wowote kwamba unatokana na kununuliwa au kushawishiwa na CCM namwona ananionea. Lakini sitamlaumu kwani sasa ni kawaida kwa wanasiasa kununuliwa na pia rushwa imeingia mpaka katika mifupa ya watanania kiasi kwamba kila kitu hupewa sababu ya rushwa! Rekodi yangu, anagalau katika hili, ipo wazi. Sinunuliki.

Sina tamaa ya mali.

I am not a materialist.

Nitanunuliwaje? Wanaonijua hawawezi kusema hivo.

Nimekuwa kiongozi wa wanafunzi pale Mlimani, usafi wangu unajulikana. Nilipomaliza masomo yangu Ujerumani nilirudi nchini na kuajiriwa. Nilipunguza muda wa kazi ofisini kwangu mpaka nusu siku ili kupata muda kufanya kazi za chama changu. Nilikuwa kila mwezi ninaachia jumla ya sh 700,000 kwa ajili ya chama changu. Pia hata pensheni yangu maana inalipwa kutokana mshahara ambao mimi nilikubali kupata kidogo ili kutoa muda wa kufanya kazi katika chama changu. Mafanikio ya sasa ya CHADEMA huwezi kuyataja bila angalau kunipa sentensi moja katika ushiriki wa mafanikio hayo.

Pili, ndugu zangu ninakipenda sana chama changu. Ninaona chama changu kama movement kwa ajili ya kuimarisha demokrasia nchini kwetu Tanzania na hatimae kuboresha maendeleo. Siwezi kamwe kusaliti chama changu. Uamuzi wowote ninaouchukua kwa vyovyote vile huwa napima madhara kwa chama changu. Ninaangalia mbali sana.

Lakini ni ukweli usiopingika kuwa toka nimekuwa Mbunge sifanyi haki kwa chama. Muda ninaoutumia kwa chama ni mchache sawa na hakuna. Ninaandika hapa nikiwa mjini Shinyanga. Nipo Wilaya ya saba toka nimeanza kazi hii ya kukusanya maoni ya wananchi kuhusu Shirikisho. Kila Wilaya nakutana na viongozi wa chama changu. Kwa kweli, ni lazima watokee watu kujitoa muhanga na kujenga chama ngazi ya chini kabisa. Jana nilikuwa Kishapu. Katika kikao, mwenyekiti wa CCM Wilaya bado anaonekana kama wa wakati ule wa mfumo wa chama kimoja kiprotokali nk. Mwenyekiti wa CHADEMA wa Wilaya anaonekana mtu tu tena kana kwamba mhaini vile. Hii ni kwa sababu muda unaotumika kufanya siasa ni mkubwa zaidi mijini. Chama changu kina mkakati wa kwenda chini kujenga misingi katika vitongoji. Kazi hii ni lazima iungwe mkono na viongozi waona mbali wa chama.

Nimesema, nataka kutumia muda mwingi zaidi kujenga chama changu ili kiwe tayari kushika dola, ama chenyewe peke yake au katika mseto na vyama vingine.

Sishangai watu kusema maneno wanayosema. Inaaminika kuwa Tanzania ukiwa Mbunge umeukata. Wengine wanashangaa kuwa naacha ulaji. Wengine wanasema nimenunuliwa na CCM na wengine wanasema nabwaga manyanga. Najua kuna faida nyingi kuw MBUNGE. Lakini zote hizo ni za muda tu. Kama tunataka kujenga chama imara, ni lazima baadhi yetu tutoke katika Bunge, tusaidie wengine kuingia Bungeni na tuwanoe vizuri ili wawe bora zaidi yangu.

Nataka tu niwajulishe kuwa sikufanya press conference Maswa. Hapana. Nilikuwa katika mazungumzo ya kawaida na watu miongoni mwao alikuwapo mwandishi Mwanga. Nilikuwa naeleza jinsi nisivyoridhika na Bunge lilivyo. Frustrations ndani ya Bunge kwa mtu yeyote makini zipo wazi. Kwa kweli sifurahii Bunge kwa sasa. Sipendi kuwa judged basing on which political group do i belong to, but on the merits of my arguments! Bunge letu linaangalia hoja yako kutokana na chama gani upo na wala sio umuhimu wa hoja yako katika maslahi ya Taifa. Sababu kubwa ni kuwa tupo wachache wabunge wa upinzani au hata wale wa CCM wenye muono wa kitaifa. Yule mwandishi ameamua kutoa to the public fikra zangu. Niliowakwaza naomba radhi. Ila ninaamini maamuzi yangu ni maslahi ya mbele ya chama changu. Maslahi yangu binafsi yangenituma nikae Bungeni zaidi na zaidi. Na ninaweza kwani mpaka sasa ninahudumia wananchi wangu vizuri sana. Anaebisha amuulize Lowasa! Alienda Kigoma Kaskazini alichokiona alibaki kuweweseka toka Kigoma mpaka Tabora.......

Tukumbuke Mwalimu Nyerere aliacha uwaziri Mkuu mwaka 1962 ili ajenge chama cha TANU. Vilevile Stephen Harper aliacha Ubunge wa Canada akaunda NGO ya kuimarisha nadharia ya conservatism kule Canada. Alitoa chama chake kutoka wabunge 12 mpaka 23, kisha mpaka 91 na uchaguzi wa tatu akashinda na kutangazwa kuwa Waziri Mkuu kijana zaidi Canada. Alijiuzulu Ubunge chama chake kikiwa na Wabunge 12 tu na kwenda kuanzisha The Canadiana Citizens Coalition. Tena yeye hakungoja uchaguzi. Alilaumiwa. Lakini chama kilipofikisha wabunge 90+ alionekana shujaa na miaka michache tu baadae aliungansiha nguvu za Conservatives wakaunda chama kimoja na kushinda uchaguzi. Uamuzi wangu sio mgeni hata kidogo katika dunia ya siasa.

Kama kawaida yangu nipo wazi kwa mawazo.... i am always open to ideas but not conclusions on my ideas. Asante Mwanasiasa kwa maelezo yako murua.

Sifungi Mjadala maana sikuuanzisha.....

11th June 2009, 05:09 AM

Mwanzoni nilipoona mada hii na majibu ya baadhi ya watu hapo awali sikuona umuhimu sana wa kujibu kwani ni mada ya zamani sana, mwaka 2007. Nilisema kwa mara ya kwanza kuwa sitagombea ubunge mwaka 2010 mwezi September mwaka 2006 na kuripotiwa na gazeti la SundayNews. Nilirejea tena kauli hiyo mwezi March mwaka 2007 nikiwa Wilayani Maswa mkoani Shinyanga na kuleta mjadala mkali sana katika JamboForums wakati huo.

Mwezi March mwaka 2008 nilihojiwa na gazeti la The EastAfrican na kusisitiza kuwa nia yangu ni kutumikia kipindi kimoja tu cha Ubunge na kupumzika kwa miaka mitano kabla sijarudi tena Bungeni...... soma hapa ...allAfrica.com: Tanzania: Zitto Kabwe - The Country's One-Man Backbench (Page 1 of 2)

Mara zote nilisema kuwa sababu kubwa ya kuamua kuwa Mbunge wa kipindi kimoja ni kurudi kusoma zaidi na kupata fursa ya kufanya kazi maana toka nimemaliza shule nimefanya kazi mwaka mmoja tu (Shirika la Friedrich Ebert Foundation) na hivyo kujiona kuwa ninakosa 'some skills' za uongozi ili kutumia kipaji changu 'to the fullest' na kutumikia nchi yangu. Hata siku moja sijawahi kutia shika nia yangu ya kutumikia Taifa. Lakini siku zote nimekataa kuwa carrier politician. Ninapenda nikimaliza kazi zangu za kisiasa niweze kuwa na uwezo wa kufundisha katika vyuo vikuu taaluma yangu nitakayobobea. Baada ya kuwa Mbunge kwa takribani miezi 9 tu (na hasa baada ya kikao cha bajeti cha mwaka 2006/2007) niliona dhahiri kuwa kwa Bunge letu hili, mabadiliko ni nadra sana. Hivyo nikasema mapema kabisa kuwa nitakuwa Mbunge wa 'term' moja. Nilisema mapema ili watu wa Kigoma Kaskazini wenye mawazo ya kutaka kugombea wajue 'incumbent' hatagombea. Nilifanya kwa nia njema kabisa. Ninadhani nina uhuru wa kuamua kutogombea kama nilivyoamua kugombea bila kusukumwa na mtu. Mimi sikuombwa kugombea ubunge. Niliamua mwenyewe.

Sasa kuhusisha uamuzi wangu huu nilioutoa miaka mitatu iliyopita na kununuliwa ni ufinyu tu wa mawazo ya baadhi ya watu wenye malengo yao. Kwanza nimesema mara kwa mara kuwa sinunuliki. Hakuna kiwango cha fedha cha kuninunua. Nimejiwekea misingi ya maisha ya kusema kile ninachoamini. Sasa kama ninachoamiani unakipenda, ninashukuru. Kama hukipendi kikatae. Nimejieleza sana kuhusu suala la Dowans. Niliunga mkono ununuzi wa mitambo ile ili kuliokoa shirika la Umeme - tanesco. Nilisikiliza maelezo ya watu waliopinga na kuyaheshimu. Nilipinga kutukanwa na kuzushiwa kuwa nimehongwa (wengine mpaka wamesema kiwango cha hongo - mara VX mpya, mara dola 70,000 na leo nimeona kuwa nimewekewa pesa katika yangu ya Stanbic sh 800 milioni)

- Nimekuwa Mbunge miaka 4 sasa. Kweli siwezi kuwa na pesa za kununua VX mbili tatu nk? Mwaka 2007 nilinunua gari ya kifahari kabisa (pamoja na msaada wa marafiki wa nje) aina ya Hummer, nayo nilihongwa na nani? Nimekuwa mjumbe wa Kamati ya Afrika Mashariki kwa miezi 6 nalipwa kila siku 200,000 shs. Pia nimekuwa mjumbe wa Kamati ya Madini ya Bomani kwa miezi 4 na nusu na kulipwa 350,000 kila siku. Kweli ndugu zangu nishindwe kununua VX ya 60m, tena second hand pale AfriCarriers? Mbona mnanitukana ndugu yenu? Nimesomea kiasi cha kutosha Biashara ya Kimataifa na kufanya kazi za 'consultancy' Wizara ya fedha na wizara ya Biashara na Viwanda kuandaa mkakati wa nchi katika mazungumzo ya Economic Partnership Agreements dhidi ya EU. Nimekuwa nikilipwa vizuri tu. Nimefanya kazi kwa Mwaka mmoja na Rais Kohler kuhusu mpango wa Ujerumani kuhusu Afrika. Nimefanya consultancy na EU kuhusu nafasi ya Zanzibar katika Biashara ya Kimataifa....... Kweli jamani, hata kama mtu ana ajenda ya siri, siwezi kupata fedha za kununua gari ninayoipenda? Hivi sasa nina gari 5 - Prado 2 (zote sasa nimezigawa kwa Wagombea Ubunge watarajiwa wa CHADEMA mwakani, Nissan Patrol 1 ambayo inatumika Jimboni kwangu, Prado 2 moja anayotembelea Jacquiline, my partner na VX ambayo ninaitumia mimi kwa ziara ndefu za Chama. Gari zote nimeziorodhesha katika fomu za maadili na zile za kuzitoa nitazitoa baada ya kubadili umiliki.

Ninapenda kurudia kusema kuwa sikuhongwa kutaka TANESCO wanunue mitambo ya Dowans. Sijawahi si tu kukutana na mmiliki wa Dowans, bali hata mlinzi wa kampuni hiyo na kufanya hiyo dili inayosemwa sana humu na baadhi ya watu kutaka kuamini bila hata ushahidi.

Nimeshangaa sana watu kuhusisha kuacha kwangu Ubunge na mambo hayo ya Dowans kana kwamba hiyo kampuni ili ilikuwapo September 2006 wakati ninatangaza kutogombea.

Watu kadhaa hawakukubaliana na sababu zangu za kutogombea. Ninaheshimu mawazo yao. Wengine ni watu ninaowaheshimu sana kama Mzee Mtei na Dkt. Salim (ambaye, nitamke kwa mara ya kwanza, aliplay role kubwa sana kunifanya niwe Mbunge). Wengine ni mazoea tu kwamba unaachaje ulaji? Yaani unaacha mshahara wa 12m kwa mwezi Zitto? Wengine hawaamini kuona Bunge bila Zitto. Basi kila mtu ana sababu zake.

Kitu kimoja kinaniumiza sana. Licha ya kutekeleza asilimia takribani 75% ya ahadi zangu Jimboni na kuilazimisha serikali kufanya miradi mikubwa ya maendeleo jimboni kwangu (leo barabara ya kwanza ya lami katika Mkoa wa Kigoma toka nchi ipate uhuru imezinduliwa na Pinda Jimboni kwangu - Barabara ya Mwandiga Manyovu), ninatumia muda mchache sana kuwapo Jimboni. Hii inaniumiza sana. Kwa siasa zangu, siwezi kuwa parochial MP, hivyo hili linanifanya nione uamuzi wangu wa kutogombea uendelee na kwamba hata nikirudi Bungeni baada ya miaka 5 au Kumi, ninadhani nitagombea Jimbo mojawapo la Dar es Salaam kwani ninatarajia kuendelea kufanya siasa za kitaifa.

Ninaacha Ubunge nikiwa nimefanya mambo ninayojivunia sana. Nimesababisha mabadiliko makubwa katika uendeshaji wa Bunge kupitia mabadiliko ya kanuni za Bunge, niliufanya mjadala wa sekta ya Madini kuwa mjadala wa kitaifa na kupelekea kuundwa Kamati iliyotoa ripoti nzuri sana na nimekuwa mstari wa mbele kuhakikisha kuwa ripoti hiyo inatekelezwa, kwa mwaka mmoja ambao nimekuwa mwenyekiti wa Kamati ya Mashirika ya Umma mabadiliko makubwa sana yanatokea na soko la Hisa la Dar (kwa juhudi zangu) sasa liktakuwa na Kampuni nyingi sana 'listed', nimesimamisha zoezi la kubinafsisha mashirika mpaka tathmini ifanyike, nimepelekea uchunguzi mkali kufanyika kuhusu mashirika kadhaa ambayo yalibinafishwa kiharamu ikiwemo uchunguzi wa kampuni ambayo ilinunuliwa na Rostam Aziz ambaye wengi humu mnaamini kanihonga, nimechangia kwa kiasi kikubwa kufanya mijadala ya Bunge kuwa yenye uhai na hata kuamsha wabunge wengine ambao hawakuwa wakisema licha ya kuwa Bungeni vipindi vingi, nimechangamsha siasa za nchi wakati ambapo chama tawala kina zaidi ya asilimia 80 ya wabunge. Mara zote nimeweka maslahi ya nchi mbele kiasi kwamba Dola, narudia Dola, haina wasiwasi na 'eventuality' ya mimi kuongoza dola nikitaka kwani maslahi ya nchi hayatakuwa na mashaka. Nimejenga imani kubwa na civil service na parastatal heads na hivyo kuwa na machinery muhimu za kuongoza nchi.

Sitagombea Ubunge. Ninakwenda kusoma 'Resources Economics' na nikimaliza nimeanza mchakato wa kuomba kazi ama somaliland au Southern Sudan ili nishikrika katika ujenzi wa 'institutions' kwa nchi hizi. Ninaamini kuwa maarifa na uzoefu nitakaoupata vitanisaidia sana nitakaporudi kwenye siasa. Ninaamini pia kuwa kuna Watanzania vijana wengi sana wenye uwezo mkubwa wa uongozi lakini hawana fursa kama niliyopata mimi. Nitawasaidia hawa ili watoe mchango wao katika kujenga Taifa letu zuri sana. Nimetimiza wajibu wangu. Ninajivunia sana rekodi yangu ya kazi ya Ubunge mpaka sasa.

Mtu mmoja humu amewahi kuandika kuwa wengi humu hamumuelewi Zitto. Nakubaliana nae sana.Wengi humu mnaniunderestimate sana! Save this thread........ mtahitaji kuirejea huko mbele.....
 
Last edited by a moderator:
....
This is part of spinning. Uwongo, uzushi nk. Tatizo wanaopanga haya wanasahau kuwa tuliyapanga wote dhidi ya marehemu Chacha Wangwe. Unatengeneza uwongo, unausambaza, na hatimaye wewe mwenyewe unauamini kuwa ni kweli.

Kama kuna kitu kilimuuma marehemu wangwe na alikufa nacho ni kile cha kumsema kuwa alikuwa anatumiwa na mafisadi. Namshukuru Mungu kuwa nilimwomba radhi Chacha kabla na baada ya kifo chake siku ya postmorterm kwa kumzushia uwongo.

Asha ni mmoja wa wenzangu tulioshiriki kumtenda Chacha. Wanatumia mtindo ule ule na wanapita njia zile zile. Rashidi wa Kuli alisema, YANA MWISHO HAYA!

....
.

Ni uongo gani huo waliomtunguia Chacha Wangwe? Je walishiriki zaidi? siri za chama hizo...ukiongea wanakuduu...
 
Hizo ndiyo siasa na wanasiasa wa bongo.! we unashangaa hilo,kwa tanzania mwanasiasa anaweza kukana hata jina lake ili afanikishwe mambo yake ya kisiasa.

aliyesema siasa ni mchezo mchafu hakukosea.

uoni maprofesa,madtari na wasomi wakisema pumba kwenye majukwaa,utadhani ni watoto wa drs la 2,hiyo ndiyo bongo
 
Vijana wa kutumwa na Mbowe utawajua tu!

Wamekubaliana wameyamaliza huku chini chini wanawatuma kuja ku SPIN hapa JF.

Huyo boss wenu ilikuwa adondoshwe na yuko pale kwa nguvu ya baba mkwe tu. Mkielewa hilo mtaacha ujinga wenu wa kuja kumchafua Zitto.

Zitto na Dr. Slaa ndio wameifanya CHADEMA iwe hapo ilipo sasa; huyo Mbowe anafaidi ruzuku tu na totoz wa kuteuliwa ambao ni juhudi ya akina Wangwe, Zitto, na Dr. Slaa.
 
Hizo ndio politics, hivyo mtu huwa anabadilika kutokana na maeneo na mtindo hata watu sasa hapa mimi sioni sababu ya kubadilika wa Zitto.!!

Sasa sisi ndio inabidi tufanye kazi ya kusimamia ukweli na sio tena kuja na majungu kama haya
 
Kitu kimoja alichoongea zitto humu na ninachokubaliana nea ni kuwa kweli watu wengi wanamu underestimate sana,,,,,they cant measure him up,,,,,,ha ha ha sadly but it is true,,,,,hata mbowe hakutegemea uenyekiti wake ungetishiwa hivyo.......ha ha ha
 
  • Thanks
Reactions: DSN
Hizo ndio politics, hivyo mtu huwa anabadilika kutokana na maeneo na mtindo hata watu sasa hapa mimi sioni sababu ya kubadilika wa Zitto.!!Sasa sisi ndio inabidi tufanye kazi ya kusimamia ukweli na sio tena kuja na majungu kama haya
Sawa wanasiasa hubadilika lakini mara nyingi husubiri vumbi likatulia kisha wanakuja na uongo mwingine. Haya ya Zitto tunayoyaona leo mie naita KUKURUPUKA.
 
Mpo busy ku recycle habari ile ile, sasa kama mnamuona hafai mbona mlimpigia magoti akubali unaibu katibu mkuu.

Vibaraka wa Mbowe mmefulia!
 
Hili swali nalazimika kujiuliza na kuwaulizeni wenzangu, hivi kwanini wnaCCM waliopo hapa JF (mfano Engineer, mkamaP nk) wanamtetea sana Zitto?

Mimi ninatambua kuwa Zitto ni mmoja wa wapiganaji muhimu ktk ukombozi tunaoutafuta. Ktk kundi hilo wapo makanda mbalimbali wa upinzani. Kinachojitokeza sasa CCM wanajifanya wapo pamoja na Zitto na siyo wapinzani wengine, kwanini?
 
Hili swali nalazimika kujiuliza na kuwaulizeni wenzangu, hivi kwanini wnaCCM waliopo hapa JF (mfano Engineer, mkamaP nk) wanamtetea sana Zitto?

Mimi ninatambua kuwa Zitto ni mmoja wa wapiganaji muhimu ktk ukombozi tunaoutafuta. Ktk kundi hilo wapo makanda mbalimbali wa upinzani. Kinachojitokeza sasa CCM wanajifanya wapo pamoja na Zitto na siyo wapinzani wengine, kwanini?

To me what matters most is fact. The question of why some people are always defending Zitto seems to be a misplaced one. People here at JM comments according to their analysis. That's is my understanding!!
 
Hili swali nalazimika kujiuliza na kuwaulizeni wenzangu, hivi kwanini wnaCCM waliopo hapa JF (mfano Engineer, mkamaP nk) wanamtetea sana Zitto?

Mimi ninatambua kuwa Zitto ni mmoja wa wapiganaji muhimu ktk ukombozi tunaoutafuta. Ktk kundi hilo wapo makanda mbalimbali wa upinzani. Kinachojitokeza sasa CCM wanajifanya wapo pamoja na Zitto na siyo wapinzani wengine, kwanini?

Simple!

Kama umeshasema ni wana CCM(sina hakika) wanachofanya ni kulalamika indirectly, kuwa, mbona mnataka muitoe CCM madarakani ila hali tabia ya CHADEMA na wao CCM ni copyright? kama vile mapacha? kwa nini mnataka muwaondoe, so wanajaribu kulia katika umma, kuwa CHADEMA NA CCM ni sawa, so afadhali CCM wabaki madarakani after all, wanachoringia CCM ni kuwa hakuna ukabila, ila system ya kutafuta viongozi ni sawa kabisa na CHADEMA!

Nimejibu if and only if Mkamapa na Engineer ni CCM!

Be careful kuwa si kila aliye kinyume na CCM ni mpinzani, na si kila aliye kinyume na CHADEM haipendi CHADEMA na ni fisadi

Zito CHADEMA wanasema alichukua fedha leo hii mnampa unaibu katibu mkuu??!!!!

sielewi is your turn Nemesis, nisaidie hapa!
 
Hili swali nalazimika kujiuliza na kuwaulizeni wenzangu, hivi kwanini wnaCCM waliopo hapa JF (mfano Engineer, mkamaP nk) wanamtetea sana Zitto?

Mimi ninatambua kuwa Zitto ni mmoja wa wapiganaji muhimu ktk ukombozi tunaoutafuta. Ktk kundi hilo wapo makanda mbalimbali wa upinzani. Kinachojitokeza sasa CCM wanajifanya wapo pamoja na Zitto na siyo wapinzani wengine, kwanini?

Nemesis,

Tayari umeshajua Engineer ni CCM? Kadi ulinipatia wewe?

Naona umesharikoroga tayari au kama ni majani yameshakuzidi nguvu. Angalia tu kaka wanaume wasikupitie.

Hata kadi sina ila nitakata mwakani ili nimpigie kura Mwakalinga na kisha nitaichoma moto.

Hivi vyama mimi havinisaidii kitu; badala yake umaskini wangu unazidi kuongezeka tu. Mtu yeyote ambaye nitamwona anafaa na ana uwezo wa kubadili maisha hata kama sio yangu basi ya mtoto wangu, nitampigia debe kwa nguvu zote na kumpigia kura.

Zitto kama ilivyo Mwakalinga, wanawakilisha hili kundi la vijana wanaotaka kufanya kitu cha maana lakini mizengwe juu yao ni mikubwa mno. Ndio maana hapa tunaambiwa kambi ya Mwakalinga njaa kali lakini sisi hatupo kwa ajili ya fedha, tunataka maendeleo. Tutapiga kampeni hata kwa miguu.

Machama yenu bakini nayo wenyewe.
 
Last edited by a moderator:
Sawa wanasiasa hubadilika lakini mara nyingi husubiri vumbi likatulia kisha wanakuja na uongo mwingine. Haya ya Zitto tunayoyaona leo mie naita KUKURUPUKA.
Hapana shaka kuwa Zitto Kabwe ni Muwazi ndio maana tunapata hata mada za kujadili hapa JF na Pia tazama Robo tatu ya posts zote hapa Zinahusu CHADEMA. Ndio maana niliyasema haya kuwa CHADEMA ni Chama Mbadala kwa CCM japo baadhi ya watu walipinga, Tazama wiki nzima iliyopita ilifunikwa na Habari ya uchaguzi wa Chadema na hivyo, CHADEMA wapo imara sana
 
Hili swali nalazimika kujiuliza na kuwaulizeni wenzangu, hivi kwanini wnaCCM waliopo hapa JF (mfano Engineer, mkamaP nk) wanamtetea sana Zitto?

Mimi ninatambua kuwa Zitto ni mmoja wa wapiganaji muhimu ktk ukombozi tunaoutafuta. Ktk kundi hilo wapo makanda mbalimbali wa upinzani. Kinachojitokeza sasa CCM wanajifanya wapo pamoja na Zitto na siyo wapinzani wengine, kwanini?

Teh teh teh teh
Sema tu unachotaka kusema kwamba Zitto tumempa fedha ndio tuna mtetea kwi kwi kwi kwi kwi.

Naona bora ccm, ngoja nikukumbushe kuna fisadi RA(igunga), fisadi lowasa(arusha), fisadi mwakyembe (mbeya),fisadi magufuri(kagera),fisadi mkono(mara),fisadi mramba (kili),fisadi msabaha(pwani), fisadi muhidhihir (mtwara) na komba nk.

CHADEMA fisadi Mbowe (kili), fisadi Ndesa(kili),fisadi komu(kili) ,fisadi mtei(kili) nk teh teh teh teh

Umeona wana kitu common kimoja(fisadi) tofauti ni huyo fisadi anatokezea wapi.? ndiyo advantage ya ccm.
Habari ndiyo hiyo.
 
Zitto yupo sahihi, akisema Olesendeka au mama malechela dhidi ya wana ccm wenyewe kwa wenyewe tunashangilia, basi zitto anahaki ya kuwasema wanachadema wenzake kama akina olesendek, na tunabudi tuwashangilie akiwasema..CHADEMA ni chama dhaifu sana na imejitokeza, embu tajeni wanasiasa wangapi wanaojulikana na kuibeba CHADEMA ni Dr slaa na Kabwe full stop..hakuna cha huyo mbowe wala nini
 
Wanabodi,,
Duh kusema kweli Zitto hahitaji fedha za Rostam wala mjinga yeyote yaani itakuwa tammaa ya kupita kiasi..

1. Mbunge kwa miaka minne pato lake ??????... kwa siku.

2.Mjumbe wa kamati ya Afrika Mashariki kwa miezi 6 -Malipo ni Tsh 200,000 kwa siku.

3. Ni mbunge wa kamati ya madini ya Bomani kwa miezi 4 - akivuta 350,000 kwa siku..

Kwa mtaji huu jamaa yupo fit.. Na hakika wala sijui huko Chadema kuna nani anavuta fedha kama jamaa yetu inawezekana kabisa kuna ile roho ya BARA yaani ukame (roho mbaya, kikorosho, roho ya kwa nini, na kadhalika)..
Mimi kama Mtanzania na mtoto wa mjini mwenye kutazama mbali hasa ktk fikra za Wadanganyika..Nitahoji tu kile mabcho wengi wanashindwa kukisema..
Mkuu Zitto hicho kipato unachokizungumzia hapo juu ndicho sababu ya jichjo unalopigwa.. kuwa muwazi hapa aahcana na hizi habari za VX ..Kwa lugha ya kijicho cha Mtanzania wanahcojaribu kusema ni hivi:-

Duh..Ni kiasi gani cha fedha Zitto anatengeneza kila mwezi ktk kamati hizi?..Je hivi kweli Zitto haoni kuwa hizo ni fedha nyingi sana kwa malipo ya kazi wanayoifanya na kuwa moja ya sababu kubwa ya chama kupinga matumizi makubwa ya seriukali?... Je hizi fedha na malipo makubwa inaweza kuwa sababu ya CCM kumkatama Zitto ajitenge nasi?.. Je hala malipo ya posho na kadhalika ndizo fedha za Mafisadi zinazozungumziwa?..
Kwa hiyo Zitto kajitengenezea maadui kutokana na kipato zaidi anachovuta toka CCM kwa kazi ambayo yeye kama Mpinzani inaonyesha anauza sera za Chadema.

Kibaya zaidi ni pale Zitto anapofikiria kwamba Bungeni ni sehemu ya mtu kuwakilisha mawazo yake binafsi, mahala ambapo mtu anatakiwa kuwa judged kutokana na kauli yake mwenyewe..yaani kila mtu ata walk in na mawazo yake bila kujali chama!.. Hii sijui mkuu kaipata wapi!..

Anafikiria kuwa na Uhuru wa kufikiria anachotaka yeye na kukipendekeza mbele bungeni kuwa ndi vyo inayotakiwa kuwa?..Mkuu huu si uwanja wa Tennis ambapo kuna wachazaji wawili kila mmoja akijiwakilisha..Bungeni ni Team work kama uwanja wa soccer (football) ujuzi wako wa kusema au kucheza ni lazima ufuatane na formation ya mchezo mzima kuwa wewe team captain haikupi haki na nguvu ya kuwa juu ya utawala wa team Chadema ktk mashambulizi yake.

Bungeni sii mahala pa kujipatia sifa, kujitangaza au kila mtu kutoa mawazo yake binafsi ila ni mahala ambapo Itakadi zinapotawala mjadala mzima ktk kutatua matatizo na sii Zitto au Mkandara anapendekeza kitu gani.. Biungeni ni mahala pa kutunga sheria kupitisha maazimio ambayo tayari yameisha fanyiwa uchunguzi kabla ya kuwekwa mbele yenu. Bungeni ni mahala Zitto anapozungumza huchukuliwa kama Chadema Mrengo wa kati Kulia wamesema hivi na sii anavyotaka yeye kuwakilisha mawazo yake mwenyewe kwa jinsi anavyojisikia..
Haiendi hivyo mkuu wangu Zitto.. Ukomavu wa kisiasa ni pamoja na kutambua tofauti hizi... huwezi kudai kwamba unapokuwa Bungeni unawakilisha mawazo yako.. Hili ni kosa jingine..
 
Last edited:
Back
Top Bottom