Kauli hizi za Zitto zinatupa picha gani?

Mnaoleta mifarakano na kuendeleza ujinga hapa JF na hata baada ya watu kuelewana nakumaliza tofauti zao , kwania kuuchochea mgogoro nadhani hamna nafasi.Hapa watu wengi wa JF si wapiga kula .Wanasema tu lakini siku ya kura na kampeni za uwanjani hawajitokezi .Nadhani sasa kama mnatumika kuja kuchafua Chama , kumachafua Zitto nk mjue kwamba tumesha jua mengi yenu na bora ujinga huu mkaufanyie nje ya JF .
 
Anasema sisi ndio hatumwelewi!

Dilunga,

Umezitoa wapi hizo?

Zitto bado ni kijana kwahiyo kutambiana kwa vijiweni bado kunakuwepo, vinginevyo ana nia nzuri tu.

Ila kama mtetea wa wanyonge inabidi apunguze hayo magari ya bei mbaya.
 

Wewe Dilunga "unajifanya mjuaji".....eehh........lol

Sio hivyo Mkuu, tunajaribu tu kumwelewa kiongozi wetu, "Mbunge wa Taifa" Zitto Zubeir Kabwe.

Kwamba, anatuhakikishia "mimi sio materialist" ila mkuu anasukuma mi Hummer, mi Prado, mi VX, mpaka mashine nyingine anasema anagawa kwa kina "Jacquiline"; lakini yeye "sio materialist"!

Halafu, hold a second now, alipotangaza tofauti zake na Mwenyekiti, alisemaje, yeye ni nani, bepari au Mjamaa, alisemaje tena? Haha ahaaaaaaa!

Tunajaribu tu kumuelewa. Zitto anasema, Ogah, sisi ndio hatumuelewi!
 
Zitto yupo sahihi, akisema Olesendeka au mama malechela dhidi ya wana ccm wenyewe kwa wenyewe tunashangilia, basi zitto anahaki ya kuwasema wanachadema wenzake kama akina olesendek, na tunabudi tuwashangilie akiwasema..CHADEMA ni chama dhaifu sana na imejitokeza, embu tajeni wanasiasa wangapi wanaojulikana na kuibeba CHADEMA ni Dr slaa na Kabwe full stop..hakuna cha huyo mbowe wala nini

You are right, Kunya anye kuku akinya bata kaharisha!

Teh teh teh teh
Sema tu unachotaka kusema kwamba Zitto tumempa fedha ndio tuna mtetea kwi kwi kwi kwi kwi.

Naona bora ccm, ngoja nikukumbushe kuna fisadi RA(igunga), fisadi lowasa(arusha), fisadi mwakyembe (mbeya),fisadi magufuri(kagera),fisadi mkono(mara),fisadi mramba (kili),fisadi msabaha(pwani), fisadi muhidhihir (mtwara) na komba nk.

CHADEMA fisadi Mbowe (kili), fisadi Ndesa(kili),fisadi komu(kili) ,fisadi mtei(kili) nk teh teh teh teh

Umeona wana kitu common kimoja(fisadi) tofauti ni huyo fisadi anatokezea wapi.? ndiyo advantage ya ccm.
Habari ndiyo hiyo.

Na wamempa uongozi tena! japo 'CCM' mmempa hela! haiingii akilini, Zito mziki mzito, yuko juu kuliko jina la Chama, mshukuru anakaa chini na kuchukuliana nanyi, angekigawa chama vipande 100! kama angepokea fedha hao wana CCM lazima wangeirusha hewani, kapokelea wapi, sh.ngapi, ili CHADEMA ife!

Anasema sisi ndio hatumwelewi!

we need leaders who are open in what they possess! that shows they are clean!

Hapana shaka kuwa Zitto Kabwe ni Muwazi ndio maana tunapata hata mada za kujadili hapa JF na Pia tazama Robo tatu ya posts zote hapa Zinahusu CHADEMA. Ndio maana niliyasema haya kuwa CHADEMA ni Chama Mbadala kwa CCM japo baadhi ya watu walipinga, Tazama wiki nzima iliyopita ilifunikwa na Habari ya uchaguzi wa Chadema na hivyo, CHADEMA wapo imara sana

Nemesis,


Hivi vyama mimi havinisaidii kitu; badala yake umaskini wangu unazidi kuongezeka tu. Mtu yeyote ambaye nitamwona anafaa na ana uwezo wa kubadili maisha hata kama sio yangu basi ya mtoto wangu, nitampigia debe kwa nguvu zote na kumpigia kura.

Zitto kama ilivyo Mwakalinga, wanawakilisha hili kundi la vijana wanaotaka kufanya kitu cha maana lakini mizengwe juu yao ni mikubwa mno. Ndio maana hapa tunaambiwa kambi ya Mwakalinga njaa kali lakini sisi hatupo kwa ajili ya fedha, tunataka maendeleo. Tutapiga kampeni hata kwa miguu.

Machama yenu bakini nayo wenyewe.

So as me, naangalia ukweli, na nani atakuja kuileta Tz iwe ya maendeleo, hata tukifa we are happy that our grandchildrens gonna live happily in the land of their fathers!

To me what matters most is fact. The question of why some people are always defending Zitto seems to be a misplaced one. People here at JM comments according to their analysis. That's is my understanding!!

we are twins I guess, the facts always is superior than zillions words of justifying wrong things. 1+1=2, that is an answer. what they did CHADEMA was wrong, no matter how they can justify it!

..jamani uchaguzi umekwisha, vunjeni makundi.

There you are! Kama JF ni sehemu ya makundi, basi kuna watu wanaharibu sifa ya being great thinkers! Ila kuna watu tusio na makundi tunajadili yale yapaswayo kusemwa, no matter what!

Kwa sababu unasema kuna makundi, basi watajaribu kuwaweka kundi moja wale wasio na vyama humu, wale walio na mawazo sawa, wale wanao analyse mambo na kufikia same conclusion, na hili nalo ni kundi!!!! ila hili lina afadhali kuliko kutetea kuwa KINYESI NI MKATE, KWA SABABU TU UKISEMA TU KINYESI MKATE BASI TUTAKULA KWA KUSEMA HIVYO!

Na wale wanaosema kinyesi ni kinyesi watatupwa mbali na kuonekana wabaya, athari zake ni kuwa wale wanaosema kinyesi ni kinyesi watapita na kuishi popote kwa theory zao za ukweli, kwani kama kuna kosa unajiosha

wale wanaosema kinyesi mkate, wataishi bila raha, wana hasira, wanajificha, watanunua manukato meeengi ili mradi tu waonekane kuwa wanachosema ni sahihi, kinyesi hakina adabu hata ukivaa pampers harufu yake itatokeza tu, ngau yangekuwa ya kale, tungesema hayanuki HAYA YA JUZI TU NDANI YA CHADEMA, no way out yananuka tu!

Huwa nawaambia wana CHADEMA, bishaneni na watu ndani ya JF, ukweli uko huko vijijini ambao CCM wanawalisha sumu kuwa CHADEMA WANA UKABILA, na hakuna demokrasia, na vitaleta vita, NI WAJIBU WA CHADEMA kuishi wakijua hivyo! kuwa tunataka msafike mpate kura, na sio mbishane humu mkose kura! so ni wakati wa kuondoa hilo wingu hata kama si kweli SIASA IS WHAT IT IS!

are we bad then by being honesty toward you!
 
Last edited by a moderator:
Dilunga,

Mkuu mimi ndiye nilisema ya kwamba Hamumuelewi Zitto na Zitto alinukuu tu usemi wangu na najua kwa nini alisema hivyo kwani hadi leo hii hakuna mtu anayejua Zitto ana malengo gani na akayaweka hapa bayana na vizuri..

I Have a clue, lakini siwezi kuanza kubwabwaja ovyo wakati sina uhakika..Isipokuwa tu namwomba atulize ball, mambo yanakwenda na wakati na siku zote sii mdomo wala maneno mengi yanayomjenga mtu au legacy ya kiongozi, isipokuwa yale Aloyafanya.
 
Dilunga,

Umezitoa wapi hizo?

Zitto bado ni kijana kwahiyo kutambiana kwa vijiweni bado kunakuwepo, vinginevyo ana nia nzuri tu.

Ila kama mtetea wa wanyonge inabidi apunguze hayo magari ya bei mbaya.

huyu ni kijana takribani miaka 30 ,wajaluo wanasema
Vunja mfupa angali meno iko,
 
wana JF inaonyesha dhahiri Zito sio kiongozi bora kutokana na kauli zake mwenyewe!


Kaka uliambiwa kwamba ingia JF uongeze idada ya mashambulizi kwa Zitto? Maana una post 2 tu na mashambulizi tayari.

Kauli tata hazijawahi tolewa na Zitto pekee hata huko kwenye familia zenu mnazitoa makazini na hata CCM wanazitoa kila siku na zinabadilishwa kila leo .Mbona you do not vote against them kwa kuwa hawafai kuwa kiongozi?

Kwanza ukisema Zitto hafai kuwa kiongozi na labda si kiongozi wako na kwako na kwa wengi anafaa.
 
Nimefikia hitimisho la Zitto kuwa mijadala yote hii ni part ya sinema nzito inayoendelea Chadema..Zitto ni
1. Mbunge kwa miaka minne pato lake ??????... kwa siku.
2.Mjumbe wa kamati ya Afrika Mashariki kwa miezi 6 -Malipo ni Tsh 200,000 kwa siku.
3. Ni mbunge wa kamati ya madini ya Bomani kwa miezi 4 - akivuta 350,000 kwa siku..


Je ni fedha hizi za ziada toka kamati za JK ndizo zinaitwa fedha za mafisadi?..maanake mkuiu Zitto anatisha fedha anazovuta kwa mwezi inabidi huko Chadema watu wakune vichwa..
Ama kweli CCM wajanaj janmani sikuijua hii hadi nilipoingia Deep naanza kuiona picha ya mgogoro mzima wa Chadema.
Nitarudia kusema hivi, Zitto kajitengenezea maadui kutokana na kipato zaidi anachovuta toka CCM kwa kazi ambayo yeye kama Mpinzani inaonyesha anauza sera za Chadema.
 

Dilunga,

Umezitoa wapi hizo?

Ndugu yangu Mtanzania, unadhani nimemtengenezea Zitto mambo ambayo hakuyasema?


Mtu mmoja humu amewahi kuandika kuwa wengi humu hamumuelewi Zitto. Nakubaliana nae sana....Save this thread........ mtahitaji kuirejea huko mbele.....

Mtanzania,

Huwezi kumtetea Zitto eti "ni kijana" kwa hiyo anaweza kuongea mambo ya kijiweni eti ana nia nzuri, hell no! Kwanza ukishafika miaka 30 usijichukulie kijana, utabweteka, umeshakua! Na unapojivunia kuwa "Mbunge wa Taifa" then be responsible with what you say please! Jamani, tutajifunza lini kwamba tukimpenda "kijana" kwa sababu tu "ni kijana" tuwatafute pembeni tukanywe nao chai huko pembeni huko!

Kuhusu Zitto apunguze magari ya kifahari, binafsi sioni tatizo lolote kuwa na ma Hummer na ma Nissan Patrol na ma Prado na VX yako na kina Jacquiline. Unaweza kununua magari ya kifahari mpaka mbingu zidongoke, sawa kabisa, lakini usizunguke unajisifia "I am not a materialist... mimi sipendi mali." Kituko! Tena magari yenyewe gas guzzlers, ulikuwa member wa Energy sources commission! Hahahahaaaa....

Zitto anasema Mbowe ni bepari yeye ni Mjamaa!
 
Jamani naamini kuwa Zitto Zuberi Kabwe ndiye shujaa wa CHADEMA...kwakujaribu kupambana na akina the so called owners of the party [mbowe]
ila nae kaonyesha mapungufu kama binadam wengine kwa kujitoa jina lake, labda aliona hata angegombea angeibiwa kura na labda uchaguzi ungehairishwa kama ule wa vijana....
 
jamani mamluki nani kawatuma JF mnachafua kila kona?? Kuna mtu anasema eti mbowe anafaidi totoz tu na haja saidia chama, jamani, huyu mtu namjua ni CCM, baba, mama, sasa kuanza kumtukana Mbowe ili hali uchafu wenu CCM umewashinda, ni ustaarabu kweli??

Hata kama mnapewa pesa ya kulipia internet basi ni bora mtumie pesa hiyo kunywea ulanzi (ulaasi) kuliko kutusi watu, hasa wewe unayejiita engineer wa meli.
 
Jamani naamini kuwa Zitto Zuberi Kabwe ndiye shujaa wa CHADEMA...kwakujaribu kupambana na akina the so called owners of the party [mbowe]
ila nae kaonyesha mapungufu kama binadam wengine kwa kujitoa jina lake, labda aliona hata angegombea angeibiwa kura na labda uchaguzi ungehairishwa kama ule wa vijana....

Kumbuka CHADEMA aliikuta.
 
Kumbuka CHADEMA aliikuta.
hata kama kaikuta kunaubishi hamna mtu popular kama yeye ndani ya chadema, nani anasimama nae..si cha mbowe wala dr slaa nani anaweza simama na mbowe....zitto nikama Steven Gerrard wa chadema,kaikuta lakini ndo anabeba tim sasa..upo hapo
 
mpo busy ku recycle habari ile ile, sasa kama mnamuona hafai mbona mlimpigia magoti akubali unaibu katibu mkuu.

Vibaraka wa mbowe mmefulia!


ngugu wakigombana ..shika jembe ukalime ..wakielewana mtabaki na aibu!!!..

maana wengi hapa mlikuwa kama fisi ....mnamfuata mwanadamu nyuma ..mkiamini kuwa mikino inayoninginia itadondoka mpate nyama??!!! Meambulia sufuri..poleni!
sasa si muache wapumzike..au mnatafuta uchonganishi mwingine?
 
Nimefikia hitimisho la Zitto kuwa mijadala yote hii ni part ya sinema nzito inayoendelea Chadema..Zitto ni
1. Mbunge kwa miaka minne pato lake ??????... kwa siku.
2.Mjumbe wa kamati ya Afrika Mashariki kwa miezi 6 -Malipo ni Tsh 200,000 kwa siku.
3. Ni mbunge wa kamati ya madini ya Bomani kwa miezi 4 - akivuta 350,000 kwa siku..


Je ni fedha hizi za ziada toka kamati za JK ndizo zinaitwa fedha za mafisadi?..maanake mkuiu Zitto anatisha fedha anazovuta kwa mwezi inabidi huko Chadema watu wakune vichwa..
Ama kweli CCM wajanaj janmani sikuijua hii hadi nilipoingia Deep naanza kuiona picha ya mgogoro mzima wa Chadema.
Nitarudia kusema hivi, Zitto kajitengenezea maadui kutokana na kipato zaidi anachovuta toka CCM kwa kazi ambayo yeye kama Mpinzani inaonyesha anauza sera za Chadema.

Kama ni case hiyo
basi wabunge wa upinzani wasivute posho inayotolewa bungeni kwa kupitia serikali ya ccm,ama posho serikali ya ccm inapovipa vyama vya upinzani kila mwezi.

teh teh teh teh
aha nimekuelewa sasa kumbe unamaanisha wanamuonea gere kwa kuvuta pesa ndefu .teh teh teh.
 
teh teh teh teh
aha nimekuelewa sasa kumbe unamaanisha wanamuonea gere kwa kuvuta pesa ndefu .teh teh teh.
Ni pamoja na hilo! unajua tena kila sarafu ina pande mbili, ile ya Kichwa ambayo huwekwa sura ya mhusika (Zitto) na wadhifa wake kisha kuna ya pili - Mkia, ile ambayo huelezea thamani ya sarafu hiyo.
Ukiweza kupambanua hivyo kesi kama hizi hazikupi taabu!
 
jamani mamluki nani kawatuma JF mnachafua kila kona?? Kuna mtu anasema eti mbowe anafaidi totoz tu na haja saidia chama, jamani, huyu mtu namjua ni CCM, baba, mama, sasa kuanza kumtukana Mbowe ili hali uchafu wenu CCM umewashinda, ni ustaarabu kweli??

Hata kama mnapewa pesa ya kulipia internet basi ni bora mtumie pesa hiyo kunywea ulanzi (ulaasi) kuliko kutusi watu, hasa wewe unayejiita engineer wa meli.

Asante kwa kuwambia ukweli. Sisi M wamefulia kwa hili.
 
Hili swali nalazimika kujiuliza na kuwaulizeni wenzangu, hivi kwanini wnaCCM waliopo hapa JF (mfano Engineer, mkamaP nk) wanamtetea sana Zitto?

Mimi ninatambua kuwa Zitto ni mmoja wa wapiganaji muhimu ktk ukombozi tunaoutafuta. Ktk kundi hilo wapo makanda mbalimbali wa upinzani. Kinachojitokeza sasa CCM wanajifanya wapo pamoja na Zitto na siyo wapinzani wengine, kwanini?
Umemsahau Masatu, na Kibunango.
Hawa wamejawa na roho mubaya. Washindwe na walegee.
 
Back
Top Bottom