Katika Picha: Maandamano ya wanahabari Leo

Status
Not open for further replies.
Nashangaa wamekubaliana wasitaje jina la Mkuchika lakini mabango mengi yana jina hilo!

Kumbe jina la Mkuchika litaendelea kutamba pamoja na kifungo kutoisha

``We would like to put the record straight that all the local newspapers, television and radio stations will no longer cover Mkuchika by any means``

Editors Forum chairperson Sakina Datoo

Ndio maana nilisema uamuzi wa kugoma kum cover Mkuchika ni kichekesho as long as he remains the minister of information. Hususan ambae mnamwona ni dikteta.

Sasa taarifa za haya maandamo kuhusu vitendo vya Mkuchika ina maana hawataandika kwenye magazeti kesho ? Manake ni habari za kuhusu Mkuchika hizi. Au sio ?

Hawa waandishi nao wamedata. Huwezi kusema unamuwekea mtu media blackout halafu unaandamana dhidi yake ku call attention kuhusu issue za mtu huyo huyo.

Yani kwa mawazo yao, kumwandika Mkuchika ni kama benefit au favor hivi kwa Mkuchika. Na kumgomea ni kama punishment fulani, wanadhani. Kumbe wanamnyima kunde. Hawajui hata walichogomea ni nini hasa.
 
Mkuu Max,

Ahsante sana kwa kazi nzuri.

Taaaraaatibu tutafika tu!! Maji hayachemki kwa kuanzia nyuzi 100.
 
``We would like to put the record straight that all the local newspapers, television and radio stations will no longer cover Mkuchika by any means``

Editors Forum chairperson Sakina Datoo

Ndio maana nilisema uamuzi wa kugoma kum cover Mkuchika ni kichekesho as long as he remains the minister of information. Hususan ambae mnamwona ni dikteta.

Sasa taarifa za haya maandamo kuhusu vitendo vya Mkuchika ina maana hawataandika kwenye magazeti kesho ? Manake ni habari za kuhusu Mkuchika hizi. Au sio ?

Hawa waandishi nao wamedata. Huwezi kusema unamuwekea mtu media blackout halafu unaandamana dhidi yake ku call attention kuhusu issue za mtu huyo huyo.

Yani kwa mawazo yao, kumwandika Mkuchika ni kama benefit au favor hivi kwa Mkuchika. Na kumgomea ni kama punishment fulani, wanadhani. Kumbe wanamnyima kunde. Hawajui hata walichogomea ni nini hasa.

Kuhani,

For all I know by "to cover" they may very well mean writing favorably or cooperating with him, as in going to his press conferences.

With our calibre of penmanship, you just don't know anymore.
 
Kuhani,

For all I know by "to cover" they may very well mean writing favorably or cooperating with him, as in going to his press conferences.

With our calibre of penmanship, you just don't know anymore.

``We would like to put the record straight that all the local newspapers, television and radio stations will no longer cover Mkuchika by any means``

Hii ina maana anything to do with Mkuchika is out the window!!

Sasa haya maandamano hayamhusu Mkuchika ? Kesho hawataandika kwenye magazeti yao kuhusu haya maandamano ?

Hawajui hata walichogomea ni nini hawa waandishi. Wamelikoroga.
 
Nani kasema Watanzania tuna utamaduni wa kufungwa na maneno yetu?

Ikiwa rais wa Zanzibar kaenda mbele ya hadhira na kusema viongozi wa Tanzania hawana utamaduni wa kuwajibika kutokana na maneno yao, unategemea kidudumtu kama kiandishi cha habari kifikirie mara mbili kabla ya kutoa maneno makali kama hayo?

Kibaya ni kwamba hakuna mtu yeyote aliyewaomba au kuwashurutisha waseme hivyo. Kuwa mwangalifu sana unapotoa ahadi, zinafunga .
 
Na hili ni jopo la waandishi, Pundit, jopo la Wahariri.

Wamekaa chini wakasema tunamfungia/tunamgomea/tuna m-blackout Waziri.

Apparently walijipayukia tu!

Unafungia ku cover habari za mtu wakati bado Waziri ? Ha haa aaaaa !!
 
Mie nasubiri magazeti ya kesho kuona kama wataandika habari za maandamano ya Mkuchika. Hawa jamaa ni vilaza tu hawajui walifanyalo ni wa kusamehewa....
 
Na mimi ndio hicho nasubiri nikijaliwa uzima kesho nione.

Wataandika hizi habari au hii nayo ina fall under ``all the local newspapers, television and radio stations will no longer cover Mkuchika by any means.``

Halafu ukilaza wao unanishangaza sana. Nadhani journalism has got to be one of the easiest professions to learn, huhitaji hata kwenda Nyegezi na UDSM, ambako apparently ni kazi bure anyway. All you gotta do is watch and read from other world class press and you get a clue. I mean it's so bad it's pathetic.
 
Wahariri waandamana Dar wakiwa wameziba midomo

Na Boniface Meena

KWA mara ya kwanza katika historia ya habari nchini, wahariri wa vyombo mbalimbali vya habari nchini jana waliandamana kuishinikiza serikali kuliondolea gazeti la Mwanahalisi kifungo cha miezi mitatu, huku wakiwa wamebandika plasta midomoni kuashiria kuminywa kwa uhuru wa vyombo vya habari.

Gazeti hilo la kila wiki lilifungiwa kwa miezi mitatu baada ya kuandika habari inayoeleza mikakati inayoendelea ndani ya Chama cha Mapinduzi ya kumuondoa Rais Jakaya Kikwete kwenye mchakato wa kuwania urais kupitia chama hicho katika uchaguzi wa mwaka 2010.

Katika maandamano hayo yaliyoanzia Mtaa wa Lugoda na kuishia ofisi za Wizara ya Habari, Utamaduni na Michezo, wahariri hao, ambao waliungwa mkono na taasisi nyingine za kijamii, walisema wanapinga kwa kauli moja uamuzi wa serikali kulifungia gazeti hilo na kudai kuwa kitendo hicho ni kuvinyima uhuru vyombo vya habari.

Wakiwa wamebeba mabango yaliyokuwa na ujumbe tofauti ukieleza athari za kuchezea uhuru wa vyombo vya habari, wahariri hao waliandamana kupitia Barabara ya Kilwa, Sokoine na kumalizia Samora, ambako kuna ofisi za wizara hiyo.

Mabango hayo yalikuwa na ujumbe kama "Uhuru wa habari ni chanzo cha demokrasia," "Sheria ya magazeti ya 1976 ni ya kikandamizaji- haifai" na ujumbe mwingine ukisema, "Kufungiwa MwanaHalisi ni njama za mafisadi" na "MwanaHalisi jela, mafisadi huru".

Baada ya kufika jengo hilo, wahariri walituma wawakilishi wao kwenda ndani ya ofisi kukabidhi barua iliyokuwa na ujumbe wao na ubarua hiyo ikakabidhi kwa kaimu mkurugenzi wa Idara ya Habari- Maelezo, Habib Nyundo ambaye badala ya kuzungumzia hoja zilizo kwenye barua hiyo alipinga maandamano hayo na kudai kuwa Jukwaa la Wahariri, ambalo liliandaa maandamano hayo, halijasajiliwa kisheria.

"Jukwaa la wahariri halijasajiliwa na msilitumie kwani halipo kisheria," alisema Nyundo.

Lakini akizungumza na waandishi wa habari baada ya kukabidhi ujumbe wa Jukwaa la Wahariri, Absalom Kibanda, ambaye ni kaimu mwenyekiti wa chombo hicho, alisema: "Nashangazwa na kauli ya serikali kwamba jukwaa hili la wahariri halijasajiliwa. Hilo lililosajiliwa wahariri wake wako wapi?

"Uhariri si kazi ya kudumu na hilo jukwaa la wahariri ambalo serikali inadai limesajiliwa liko wapi na wahariri wake wako wapi. Wahariri wote wa vyombo vyote vikubwa vya habari ndio sisi hapa. Hao hilo Jukwaa la Wahariri lililosajiliwa wako wapi.

"Serikali lazima ijue kuwa enzi za kuwadanganya wananchi zimepitwa na wakati."

Jukwaa la Wahariri ambalo liliandaa maandamano hayo liko kwenye mchakato wa kusajiliwa, lakini halitajisajili Wizara ya Mambo ya Ndani kama lilivyokuwa la awali. Jukwaa hilo lilitazamiwa kuwasilisha maombi yake Wizara ya Viwanda na Biashara, likitaka hadhi ya kampuni.

Kuhusu kitendo cha serikali kulifungia gazeti la MwanaHalisi, Kibanda alisema: "Walitakiwa kwenda mahakamani kulifungia gazeti hilo kama walivyozuia mgomo wa walimu. Kulifungia inatia shaka kwani serikali na CCM zina mkono katika vyombo vya habari.

"Inashangaza serikali haitaki kujifunza kutoka kwa vyombo vya habari na inashangaza jinsi gani wanavyojaribu kuvunja uhusiano na vyombo vya habari.

"Nia ya kuikosoa serikali ni kwa ajili ya mustakabali wa taifa na siyo wa mtu binafsi. Taifa kwanza, mambo mengine baadaye."

Mbali na hilo pia Kibanda alihoji kitendo cha mkurugenzi wa MwanaHalisi, Saed Kubenea kutakiwa kuripoti polisi makao makuu kila siku kwa ajili ya kuweka saini katika kitabu bila kupewa maelezo yoyote.

Kibanda alisema atawasiliana na taasisi za kisheria ambazo ni wadau wa habari kuangalia jinsi ya kupambana na amri hiyo, akiita kuwa ya unyanyasaji.

Mwenyekiti wa taasisi ya vyombo vya habari vya kusini mwa Afrika, Misa-TAN, Ayoub Rioba, ambaye alishiriki maandamano hayo, alisema tabia ya serikali kufungia vyombo vya habari si tabia ya nchi inayofuata demokrasia.

"Watanzania hatuko tayari kuangalia mienendo inayotetea maslahi binafsi kupitia vyombo vya habari," alisema Rioba.

Naye mkurugenzi mtendaji wa Chama cha Waandishi wa Habari Wanawake nchini (TAMWA), Ananilea Nkya alisema kitendo ilichofanya serikali ni kuwafunga mdomo wananchi.

Alisema ni muhimu serikali ikatafakari uamuzi huo upya kwani inatafuta ugomvi na vyombo vya habari.

"Serikali ilifungulie haraka sana gazeti la Mwanahalisi kwani kulifungia ni kuwafunga wananchi mdomo," alisema Nkya.

Mhariri wa gazeti la Kulikoni, Nyaronyo Kicheere alisema kila kunapotokea habari mbaya, lazima kuwepo na mlalamikaji ambaye ndiye huchukua hatua ya kufungua kesi.

"Katika suala hili, mlalamikaji ni nani... Ridhiwani Kikwete amelalamika? Hakuna aliyelalamika, lakini serikali imeamua kulalamika kwa niaba na kuchukua hatua kwa niaba ya mlalamikaji. Hii siyo sahihi," alisema mwandishi huyo mwandamizi.

Ridhiwani, mtoto wa Rais Kikwete, alihusishwa kwenye habari hiyo iliyochapishwa na gazeti la MwanaHalisi.

Alisema uamuzi wa serikali katika kulifungia Mwanahalisi ni kijichimbia shimo kwa kuwa haina hoja katika suala hilo.

"Serikali haiwezi kuwa kila kitu kwa kutoa maamuzi ambayo hayana hoja ya msingi," alisema Kicheere.

Alisema anashangazwa na serikali kufanya uamuzi huo wakati mtoto wa Rais Kikwete, Ridhiwani ambaye alihusishwa kwanye habari ile hajawahi kwenda mahakamani kulishitaki Mwanahalisi hivyo serikali imeingilia nafasi ya watu wengine.

Mwananchi Tanzania News Paper
 
Maoni na uchambuzi

Mwananchi Tanzania News Paper
Date::10/28/2008

Serikali isipuuze kilio cha wahariri

JANA wahariri wa magazeti nchini, walifanya maandamano ya amani hadi ofisi za Wizara ya Habari, Utamdauni na Michezo, kupinga uamuzi wa serikali uliotolewa na waziri kulifungia gazeti la MwanaHalisi kwa miezi mitatu.
Maandamano hayo yalipata kibali cha Jeshi la Polisi huku wahariri wakiwa wameziba midomo kwa gundi za plastiki kuonyesha kwamba kitendo kilichofanywa na waziri ni kuvinyima uhuru vyombo vya habari kwa kutumia sheria ya magazeti ya mwaka 1975 ambayo haiendi na mazingira ya sasa ya demokrasia katika mfumo huru wa vyama vya siasa na vyombo vya habari.

Tunaunga mkono maandamano hayo kwa sababu kitendo kilichofanywa na waziri dhidi ya gazeti la MwanaHalisi, sisi hatukiungi mkono na si sahihi, bali tunakiona ni kitendo cha ukandamizaji na vitisho kwa vyombo vya habari, kwa kutumia sheria ambazo chanzo chake ni ukoloni.

Sisi tunaamini kuwa, kama wahusika waliona wamekashifiwa na habari hiyo wangekwenda mahakamani au kwenye Baraza la Habari Tanzania, kuwasilisha malalamiko yao badala ya serikali kuchukua haki zote za kuwa polisi, mahakama na hakimu wa kuamua ilivyoamua.

Ni dhahiri kwamba, adhabu iliyotolewa kwa MwanaHalisi ni kubwa mno, kwani imekuja kuwaumiza hata wafanyakazi wengine wa gazeti hilo ambao hawahusiki na uandishi wa habari na hivyo kuachwa wakitaabika na familia zao.

Tunaiomba serikali iangalie upya uamuzi wake wa kulifungia gazeti hilo kwa kutumia sheria mbaya ya magazeti ya mwaka 1976 ambayo inakwenda kinyume na uamuzi wa chi yetu wa kujenga demokrasia nchini.
 
Mie nasubiri magazeti ya kesho kuona kama wataandika habari za maandamano ya Mkuchika. Hawa jamaa ni vilaza tu hawajui walifanyalo ni wa kusamehewa....

Wangekuwa vilaza usingekuwa na huo mshawasho wa kuona wataandika nini.Kilaza ni wewe unayesubiri kuona vilaza wataandika nini.Assume wasipoandika huyo mkuchika tutakuitaje????
 
Mie nasubiri magazeti ya kesho kuona kama wataandika habari za maandamano ya Mkuchika. Hawa jamaa ni vilaza tu hawajui walifanyalo ni wa kusamehewa....
Kwa uelewa wangu finyu, habari zitakazoandikwa kwenye magazeti ya kesho zitahusu maandamano ya waandishi habari kupinga uamuzi wa Mkuchika. Kwa hiyo subject haitakuwa Mkuchika per se bali waandishi wa habari. Walichosusia waandishi wa habari, kwa uelewa wangu, mathalani, Mkuchika akiitisha press conference hawatahudhuria. Mkuchika akitoa tamshi lolote halitaandikwa, na Mkuchika akifanya uamuzi wowote wa kikazi hautaripotiwa. Am I missing something here? Yaani Mkuchika will not have any "favourable" reporting in the news media.
 
Jasusi,

I alluded to this earlier.

Lakini tamshi lao lilikuwa kali sana, mtu angesameheka kama angepata picha kwamba hawa watu hawataliandika jina la Mkuchika tena, maana wamesema "by any means".
 
"Kwa uelewa wangu finyu, habari zitakazoandikwa kwenye magazeti ya kesho zitahusu maandamano ya waandishi habari kupinga uamuzi wa Mkuchika. Kwa hiyo subject haitakuwa Mkuchika per se bali waandishi wa habari. Walichosusia waandishi wa habari, kwa uelewa wangu, mathalani, Mkuchika akiitisha press conference hawatahudhuria. Mkuchika akitoa tamshi lolote halitaandikwa, na Mkuchika akifanya uamuzi wowote wa kikazi hautaripotiwa. Am I missing something here? Yaani Mkuchika will not have any "favourable" reporting in the news media."

Jasusi,
you got this SPOT ON. There is no ambiguity in what they meant, unless kama mtu una hobby ya kupenda kujichanganya akili.
 
Wangekuwa vilaza usingekuwa na huo mshawasho wa kuona wataandika nini.Kilaza ni wewe unayesubiri kuona vilaza wataandika nini.Assume wasipoandika huyo mkuchika tutakuitaje????
Tutamuita Kilaza. Na hadi sasa inaelekea hakuandikwa kwa magazeti mawili niliyoona. Ngoja tusubiri.
 
Max Kazi nzuri brother. Nilitamani na mimi niwepo nipate angalau picha mbili tatu.
Anayedharau maandamano haya hajui impact yake. Ni sawa na aliyedharau maandamano ya walimu akidhani hayana maana.
Katika jumuiya yetu ya kitanzania wengi wanadhani maandamano hayana faida. Hii ni kwa hasara yao wenyewe.
 
Unajua nimesema mara nyingi sana hapa kwamba kwa kawaida vilaza huwa hawajijui kuwa ni vilaza, kama vile mlevi ambavyo huwa haamini kuwa amelewa mpaka awe mdondo,

And besides, kwa vile wao by nature ni vilaza, huamini kwamba kila mtu next to them ni kilaza, halafu hupigia kelele wananchi wengine kuwa ni vilaza kumbe in a real sense wao ndio vilaza, period!

Lakini njia ya muongo kwenye mpapai ni mbali sana, wanaumbuka hapa kila siku na bado wanaendelea kuumbuka, pathetic! Kilaza ni kilaza tu, hakuna cha Europe wala US, once kilaza always kilaza tu!

Hongera kwa wanaume wa shoka walioandamana, sisi tuko nao kwa njia ya PC, wanaotupigania ni sisi wananchi wanyonge, na taifa letu lililopotea, vilaza ni vilaza tu hatuna majina mengine ya kuwaita zaidi ya what they are yaani vilaza!

Mungu Awape Baraka Waandishi Wote Walioandamana, kwa niaba yaetu wanyonge na walalahoi.
 
.......umeshaonyeshwa na walioshika mabango yenye jina la Mkuchika.
 
You wonder exactly nini tofauti ya hawa small vilaza na a big kilazaa, yaani Mkuchika mwenyewe!

Kwa sababu at leats we know Kubenea na waandishi waliondamana stands for what, sasa hawa vilaza na Mkuchika wao, hivi they stand for what as far as our nation well being is concerned??
 
Hapa kuna vitu viwili vinakinzana.

Kuna watu wenye standards za Tanzania, ambapo waandishi wanaweza kusema "hatuwezi kumuandika Mkuchika by any means" halafu kesho yake wakamuandika.

Halafu kuna watu wanaotaka umakini na kila mtu kuheshimu maneno yake na ahadi zake.

Ukichagua lile la kwanza halafu kesho ukaanza kupiga kelele ufisadi unachekesha, ufisadi unaanza kidogo hivi hivi, mara umeona mikamera ukataka kuleta dramatics bila kupima maneno, ukatoa mitamko iliyokuzidi kimo ambayo kesho huwezi kuiheshimu.Kesho utapewa ofisi kwa sababu ya maneno yako ya kupinga rushwa "by any means" halafu utayasahau kama ulivyosahau kwamba "by any means" hatutam cover Mkuchika.

Halafu kuna watu humu wanaleta mambo ya "Us versus them", kwamba if you are against Mkuchika you must be with the journalist, and if you criticize the journalist you must be with Mkuchika, sorta like George Bush in his doctrine of "If you are not with us you are with the terrorist" .Yaani upumbavu huu hauamini mtu assertive anaweza kukaa na kuona makosa pande zote mbili. Kwamba kwa kuwa ni waandishi wa habari na wanaandika kuhusu ufisadi wasisemwe ni ujuha wa hali ya juu, kama wanachemka wanasemwa vizuri tu.
 
Status
Not open for further replies.
Back
Top Bottom