Waberoya
Platinum Member
- Aug 3, 2008
- 15,169
- 10,785
Bwana Kibanda
Alisema kuwa kinachosisitizwa na Jukwaa la Wahariri si kwamba kilichoandikwa na MwanaHalisi ni sahihi ama si sahihi lakini akatoa dodoso kuwa kuna gazeti flani la leo limeandika habari ileile japo kwa namna tofauti.
Wana JF , samahani kama hoja yangu inaweza ikamuudhi mtu , nauliza kwa kutaka kujua hili swala ambalo nimeishawahi kulizungumzia huko nyuma. Ukikasirika niite majina yeyote yale, lakini usisahau kujibu hoja yangu, naamini mtanielewa.
Sikufurahi Kubenea kufungiwa , lakini pia sikufurahi alivyoripoti taarifa yake, taarifa yake imejaa uncertanities nyingi. Alivyokuwa akiripoti saga kibao zilizopita alijitahidi kuweka na vithibitisho. Naamini taarifa ile ingekuwa na vithibitisho fulani ingemuwia vigumu hata waziri kulifungia lile gazeti.
Kumbukeni, na hata yeye SK anaeelewa hilo watu wana view mbalimbali kuhusiana na gazeti lake wako wanaosema la muungwana, kwa wachache wanamapinduzi tunaona si kweli, lakini ukiifanyia analyisis ile taarifa yake unaona kama ilikuwa na lengo la kumuinua Kikwete machoni pa watu wengi, kuwa aonekane kuwa ana vita na mafisadi, kumbe vita yenyewe ni personal zaidi.
Kubenea kama mwanamapinduzi( niaminivyo mimi) alitakiwa awe mwangalifu na habari ile maana kama kweli ni adui wa serikali basi walikuwa wanatafuta chance,SASA ONA KIBANDA ANAVYOSEMA HAPO JUU KUWA ILE TAARIFA SIYO SAHIHI, HIVYO ANAONA KWA SABABU WENGINE WANAANDIKA KAMA ALIVYOANDIKA KUBENEA BASI ASIFUNGIWE!!!. Kubenea anatakiwa kuwa tofauti kama tofauti ambayo tayari ameishaionyesha kuwa gazeti lake ni taa! alitakiwa kuwa macho sana kuwa anatafutwa. hivyo basi wahariri ninawauliza
1. Kama kubenea mnakiri kuwa taarifa yake haikuwa sahihi mnataka tuseme kuwa akifanya makosa asiwe punished simply because ana rekodi nzuri?
2. Kwa maneno ya Kibanda; Je ni habari ngapi ambazo zinaandikwa nchini aidha hazina vithibitisho( kumbukeni tarime) ambazo huwa published kila siku? we have to do some investigative news, kama SK naye taarifa haikuwa imeiva angecool down, au ndiyo utamaduni wa wahariri wengi(kuwa kama ALASIRI) title is good but content is gabbage? kisa mnataka tununue tu magazeti yenu?
3. Je niandike habari mbovu/mbaya haijahaririwa kwa sababu na gazeti lingine wanafanya hivyo?
4. Katika wahariri walioandamana ni wangapi basi ambao wameshaandika taarifa mbalimbali walau kama SK?
5. Mnaonyesha (wahariri/waandishi) mko wengi sana ukiachilia mbali na taarifa za ufisadi chache tunazozipata kupitia magazeti machache, je mmekubaliana nini? mtaandika kama Kubenea?,mngeieleza serikali kuwa mtaandika zaidi ya Kubenea, mnataka kubenea afunguliwe ili nyie muendelee kuwadumaza watanzania kwa habri za udaku na ugoni, huku maovu yamejificha kila kona Tanzania hayaripotiwi?
6. Mlipotoa kifungo kwa mkuchika hamuoni kuwa mna prove kumbe kuandikwa gazetini ni mpaka uwe 'somebody' na sio kwa manufaa ya wananchi? na msiowaandika nao mmewafungia? Kwa nini msimfungie Kikwete na usanii wake anaouleta hapa TZ? hamuwezi? why?
7. Kubenea, ni lini na namna gani anaweza kuthibitisha ukweli wa habari yake? maana kama umefungiwa kwa' uzembe' wako kama kibanda anavyosema je huoni hujatutendea haki sisi wananchi tunaoamini kuwa wewe ni smart guy
8. Je kabla ye Kubenea kufungiwa wahariri walikuwa hawajui kuwa sheria ya mwaka 76 imepitwa na wakati?(au hamsomi JF?) na je SK akifunguliwa leo mmejiandaa vipi kupingana na sheria hiyo?
9. Waandishi wa habari muwe mfano, vyama vya upinzani havitafanikiwa mpaka katiba ibadilishwe, je waandishi wa habari kama watu wa mstari wa mbele katika mapambano yeyote, hamuoni inaonyesha siku zote mnafanya kazi chini ya kiwango? tangu 76 ??
10. Kibanda ukisema kuwa habari ya SK haikuwa sahihi, ila unashangaa gazeti lingine limeandika kama hivyo unataka kutupa picha gani? huoni kuwa kuna ka utoto fulani hapa ambako nikidescribe vizuri nitaonekana nakutukana? why dont you be smart mpaka 'MAADUI WAKIWA NA NENO JUU YAKO WASHINDWE PA KUANZIA'
wenu katika lindi la mawazo
waberoya