Katibu wa CCM wilaya Ya Hai Ndugu Kumotola afanya Ziara Hai

Kimetah

JF-Expert Member
May 8, 2013
1,049
188
Kazi Inaendelea Hai,ILANI YA CCM INATEKELEZWA.

Ziara Ya Kustukiza iliyofanywa na Katibu wa CCM wilaya Ya Hai Ndugu Kumotola,akikagua utekelezaji wa ilani ya ccm Katika Kata Ya Bondeni,imekuwa ya mafanikio makubwa baada ya kutangaza neema ya ujio wa nishati ya umeme.

Akizungumza katika shule ya sekondari lerai,akiwa ameambatana na katibu mwenez wa ccm wilaya ya Hai,meneja wa tanesco wilaya ya hai na mkandaras wa mradi,Ndugu Kumotola alitangaza na kuelekeza umeme ufike shule ya lerai kabla ya mwezi wa tisa,pia amewasihi walimu pamoja na wanafunzi kushirikiana na mkandarasi ili zoezi la kufikisha umeme katika shule ya sekondari lerai ufanyike haraka, Pia amewasihi waalim kutia juhudi katika kuwaandaa wanafunzi ili kufikia malengo yao.

Meneja wa tanesco pamoja na mkandarasi waliahidi mbele ya Katibu Kutekeleza kwa wakati uletaji wa umeme.
Kwa upande wa walimu,wameshukuru sana kwa kuletewa mradi huo waliousubir kwa mda mrefu,pia utarahisisha utendaj wa kazi kwa vitendo.


Hakika Yajayo Yanafurahisha, Tupo Tayari.
 
Hahaha kwanini wanakagua kwani miradi ilijengwa na watendaji wa serikali ya CHADEMA?!
Wao wenyewe nao wanakaguana?! Vipi yeye kibali alipewa, au aliambatana na DC?!
 
Back
Top Bottom