Katibu wa ccm tawi la north london Neema Kumba ajitosa uchaguzi uvccm, taifa

nngu007

JF-Expert Member
Aug 2, 2010
15,862
5,797
KATIBU WA CCM TAWI LA NORTH LONDON NEEMA KUMBA AJITOSA UCHAGUZI UVCCM, TAIFA



_MG_0693.jpg

KADA wa Chama cha Mapinduzi (CCM) kupitia umoja wa vijana wa CCM
(UVCCM) na Msomi wa digrii ya uchumi, Neema Kumba


Neema akikabidhiwa fomu jana na Sophia Duma Makao Makuu ya UVCCM jijini Dar es Salaam .
--
DAR ES SALAAM, TANZANIA


KADA wa Chama cha Mapinduzi (CCM) kupitia umoja wa vijana wa CCM

(UVCCM) na Msomi wa digrii ya uchumi, Neema Kumba, amejitosa kwenye

uchaguzi mkuu wa umoja huo Taifa kwa kuchukua kugombea nafasi ya NEC na

uwakilishi UWT.
Akizungumza na waandishi wa habari mapema jana, Agosti 3, jijini

Dar es
Salaam, muda mfupi baada ya kukabidhiwa fomu hiyo na Mkuu wa Idara ya

Oganizesheni na siasa UVCCM, Taifa, Sophia Duma, Kumba ambae awali alikua Katibu

wa CCM, tawi la North London, Nchini
Uingereza, alipokua akichukulia digrii yake

ya uchumi, alisema lengo ni
kuakikisha mikakati thabiti inajengeka kwa kiwango

kikubwa miongoni
mwa vjana na wanawake wote nchini.


"Kwa umakini wangu na maarifa niliyoyapata kwenye elimu na uwepo wangu

ndani ya chama, ndani na nje ya nchi, ni wakati sasa na mimi kuwasaidia

wenzangu hasa Vijana na wanawake ambao mara nyingi wamekua wakisahauriwa na huu

ndio wakati wa kuwainua" alisema Kumba.
Mbali na kuchukua fomu hiyo ya NEC na

uwakilishi UWT, Taifa, pia tayari
alisha chukua fomu ya kuwania nafasi ya

Mwenyekiti Uvccm, Wilaya Ilala.
Mpaka sasa tayari wanachama mbalimbali wa UVCCM,

wamejitokeza kuchukua
fomu za kuwania uongozi ambapo mwisho wa kurudisha fomu

hizo, Agosti 6.







5996140674267894691-3546614973785534087

 
Hawa wana Wadhamini nini? Wengi Wanarudi kugombea Madaraka... Mimi naweza nikapata VUMBI
 
ingependeza kujua yeye kama aspiring leader anafanya nini hsasa UK, alikwenda kwa lengo gani na kama bado ana lengo hilo lililompeleka au la, we dont need leaders wasio na targets za maisha bali kudandia tunafasi tunatojitokeza ilimradi waishi
 
Back
Top Bottom