Katibu Tawala Songwe: Mke mwenye pesa haachwi kisa Mchepuko

Mjanja M1

JF-Expert Member
Oct 7, 2018
3,660
12,305
Katibu Tawala wa Mkoa wa Songwe, Happiness Seneda amewashauri Wanawake kujiimarisha kiuchumi ili kuwa na maamuzi katika Familia huku akisema Wanawake wakiwa na fedha itakuwa ngumu kuachwa na Wanaume zao na hata kama Wanaume zao wakiwa na michepuko ila hawatowaacha wa njia kuu wenye pesa.

Amesema hayo wakati akiongea na Wanawake Wajasiriamali wa kikundi cha Tujijenge cha Wilayani Mbozi ambapo amewasisitiza kuwa wasiogope kujaribu fursa.

“Msiogope kujaribu fursa, pambaneni, umeolewa ukiwa na hela yako na kama na wewe unatoa mchango hayo mapenzi ni next level, maisha ya saa hizi usikae tu kazi yako ni kutega goli, lazima uwe na hela yako”

“Mkikaa mkianza kupanga jambo na wewe unachangia hata huyo Mwanaume atakuwa na respect anaona hili jukwaa nikiliacha litaweza kujisimamia, kwa muktadha huo hakuachi hovyo, ofcourse atakuwa na michepuko si mnajua wale Ndugu zetu (Wanaume) michepuko ndio habari yao laini ile njia kuu itabakia palepale kwa sababu unaweza kujisimamia kwahiyo tupambane kwasababu tunaweza na tuchukue fursa kipindi hiki ambacho Kiongpzi wetu mkubwa ni Mwanamke na huyu Mama (Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan) anapambana sana kutoa fursa kwa akina Mama”

Credit - AyoTv
 

Hii inaonyesha ni kwa kiasi gani kama taifa tumeporomoka kimaadili. Na kama huyo Happy ameolewa, hapa anajaribu kutueleza kuhusu tabia zake na hali ya ndoa yake.
 
Sawa sawa Happiness Seneda uko songwe eehh mtoto wa Baba mmoja mkorofi sana...amelala sasa...upole wako ....aibu zile duuuu...leo kumve unayajua ya mitaanii ? Hongera kila la kgeri katika utumishi wako
 
Back
Top Bottom