Katibu Mkuu wa Wizara ya Maji na Umwagiliaji, Prof. Kitila Mkumbo, ang'atuka uanachama ACT-Wazalendo

Mwigulu Nchemba mwenye jimbo lake anakuja,
Faru J lazima akutwishe zigo na hiyo wizara ya wasiojulikana

Ukiboronga hapo sababu tosha ya kukata jina lako

M4C kitengo cha ujasusi wako vizuri rangi halisi ya prof imeonekana
Hawa jamaaa inteligensia yao ni hatari wakimnyooshea mtu kidole kwamba ni kirusi ujue kuna ukweli
 
Nitajie angalau Sera moja tu ya Ccm ambayo ni mbaya halafu uniambie Sera ya chadema inasemaje kama Sera mbadala. Tanzania hatuna tatizo la Sera, tuna tatizo la MTU na MTU.

Sera na falsafa mojawapo ya CCM iliyopo katika Katiba yao ni kwamba nchi yetu ni ya Kijamaa na inajengwa kuelekea Uchumi wa Kijamaa. Huu ni uwongo wa dhahiri kwa sababu hatuna Ujamaa Tanzania.
 
Ikiwa wanachama wa vyama vinavyochipukia wananunuliwa, na wa vyama vikongwe wananunuliwa na kupewa nyadhifa walizojiuzulu kwa jina la dola! Je wanaokataa kununuliwa itakuwaje?:eek:

Najiuliza tu...
 
Mwafrika mpe cheo tu
Anachanganyikiwa kabisa... ndio maana wazee walitukataza kufunga ndoa na baadhi ya koo kama si makabila.
Sinenei ukabila bali uhalisia, kuna watu wa koo fulani hawaaminiki kiasili, yaweza onekana ni unyanyapaa lakini tuliusiwa kwamba ukoo ule wana asili ya maradhi au... au... au...
Kuchukua tahadhari ni muhimu
 
Sasa hapa sijui atachukua kadi upya au atahaisha ile ya zamani aliyokuwa anailipia kimyakimya


Kwa taarifa tu huyu ndio yule aliyepatwa kunenwa na polepole kuwa kigogo mmoja wa upinzani atatimkia Ssm
 
KARIBU CCM mzee unabii umetimia hii ni nyumba ya hapa kazi tuu Njoo piga kazi
 
Kitila Mkumbo hakuwahi kuwa mpinzani. Haiwezekani kwa serikali ya CCM imwache mtumishi wa umma awe mwanachama wa waziwazi wa chama cha upinzani kama ilivyokuwa anafanya Kitila Mkumbo isipokuwa kama amepewa kazi maalum ya kufanya na CCM huko upinzanini. Kumbuka alichofanywa Baregu.
 
Back
Top Bottom