Katibu Mkuu wa CCM, Aondoke?

...OK mmemaliza kutafuna fedha za walalahoi kwa mikutano yenu isiyo na faida bali hasara tuu,unaambiwa dodoma Landcruisers za milioni mia mia zilikuwa zimejaa kuliko Los Angeles...damn hawa mafisadi!
 
nilisharipoti kabla,huyu huyu mburushi Rostam AZIZ yumo tena CC.. Yaani nchi inaendelea kuliwa na hawa wanamtandao,yaani kanunua hadi nyumba karibia na ikulu..?
uko wali mwalimu?fufuka uje uwaone mabepari uliowakataa wanashika nchi..utabiri wako umetimia,...ccm si mama yangu..
 
nilisharipoti kabla,huyu huyu mburushi Rostam AZIZ yumo tena CC.. Yaani nchi inaendelea kuliwa na hawa wanamtandao,yaani kanunua hadi nyumba karibia na ikulu..?
uko wali mwalimu?fufuka uje uwaone mabepari uliowakataa wanashika nchi..utabiri wako umetimia,...ccm si mama yangu..
 
Yaani JK hakudiriki kabisa hata kupendekeza jina la prof. Mwandosya? Inaelekea ugomvi wao haujaisha.
 
Yaani JK hakudiriki kabisa hata kupendekeza jina la prof. Mwandosya? Inaelekea ugomvi wao haujaisha.

Wenye data watuambie, Nilisoma hapa forum kwamba JK hajafanya ziara mkoani Mbeya kwa nini? Sasa katika mazingara kama hayo unategemea ampendekeza Mwandosya. You must be kidding.
 
Wenye data watuambie, Nilisoma hapa forum kwamba JK hajafanya ziara mkoani Mbeya kwa nini? Sasa katika mazingara kama hayo unategemea ampendekeza Mwandosya. You must be kidding.

Nilikuwa nategemea prof. Mwandosya ni katika mawaziri waandamizi, kwahiyo angalau angependekezwa kwenye wale 30.

Hivi kwani ni Mbeya tu ambako JK hajapita? Huenda kuna mikoa mingine pia.
 
FD, as a matter of fact sikufikiria hilo ila it makes more sense than kumuacha tu. Mzee Makamba ana kipaji cha kuzungumza na ushawishi na hasa kuweza kujibu hoja kwa kutozijibu hoja. Niliangalia Mwanri anavyozungumza kuhusu masuala mbalimbali, kwa kweli si mshawishi bali ni mtu ambaye anafaa kutoa maagizo na kufuatilia utendaji. Mzee Makamba kwa upande mwingine ni mtu ambaye anaweza kukiuza CCM kwa ucheshi wake, na kwa kutumia 'wit' na kwa vile anaijua vizuri CCM nadhani si mtu wa kumpoteza kabisa.. Hivyo ila hilo la Katibu Muenezi nadhani itakuwa demotion kwake. Ila kwa kada kama yeye nadhani atapiga saluti na kuwa tayari kukitumikia chama.

Je Mzee Malecela asipoutaka/pewa Umakamu tena, anaweza kuwa Katibu Mkuu?

Akiwa mkuu wa Kigoma kulitokea yale matatizo ya wakimbizi. Katika pilikapilika ilitokea mnuso fulani na Makamba alikuwa mgeni rasmi lakini katika mnuso kulikuwa na wageni kutoka nje. Ilipofika wakati wa mgeni rasmi kutoa hotuba Makamba alinyanyuka na kusema Thank you very much na akakaa chini. Huo ndio wit wake.
 
Nahisi kama humu ndani JF ama tumeingiliwa ama tumeelemewa, na hasa la pili la kuelemewa ama yote kwa pamoja, maana tumeshindwa kuunganisha mada zinazofanana, kwa mfani ya mkutano wa CCM, maana kuna mada nyingi sana zinagongana.. Mfano hii na hii niliyoianzisha Jumanne mchana (EAT). Zipo mada nyingi zinazofanana na watu hawasomi wanabandika tu. Huwa inatokea hata mm nabandika tu, lakini si kiwango cha JF inayoaminika sana kwa sasa na Watanzania walio wengi.

http://www.jamboforums.com/showthread.php?t=6983

Nilisema:
Chiligati, Mkuchika, Makala, Mh'd Dewji

Tuwaangalie hawa, John Chiligat, George Mkuchika, Amos Makala na Mohamed Dewji, wanaweza kuingia katika sekretarieti moya ya CCM

Ukimuondoa Dewji na kumuongeza Membem wote wameingia katika sekretarieti. Katika thread hiyo hiyo nilifika mahali nikahitimisha kwamba Makamba anaweza kurudi na kuahidi kukamilisha matokeo yote katika kipindi cha dakika 30 kabla ya kuishiwa fedha katika mtandao wangu...
 
Unamsema Mwandosya, Je rafiki yake mkuu Lowassa. au yeye anaingia moja kwa moja?
 
Watendaji wote waliokuwemo kwenye Sekretarieti iliyopita wameondolewa isipokuwa Makamba anayeendelea kuwa Katibu Mkuu. Waliondolewa ni Naibu Katibu Mkuu, Jaka Mwambi, Katibu wa Itikadi na Uenezi, Aggrey Mwanri na Mweka Hazina, Rostam Aziz
.

Hii inachanganya, inakuwaje tena Rostam anatajwa yumo tena?
 
Mtanzania,
Lowassa anaendelea kwa kutumia nafasi ya PM
sijaelewa kuhusu maelezo hayo hapo juu kuhusiana na Kamati kuu maanake tukisema hivyo hata Mwandosya na Kingunge bado wanaendelea na nafasi zao za Uwaziri au?
Kifupi, nafasi ya Lowassa ktk chama ni ipi maanake Uwaziri mkuu ni wadhifa wa Kitaifa!..
 
Waziri Mkuu, Spika, na Makamu wa rais, wanaingia cc kwa kazi zao as of ccm ikiwa mdarakani, lakini sio mawaziri hawaingii huko kwa uwaziri wao.
 
Ngoja na mimi nianze kupondea JF kama wanasisiem hapa

yaani inakuwaje sasa hivi ni wanasisiemu tu ndio wanachangia hapa kwenye mtandao? inabidi kuwe na balance? hii JF inaanza kukosa muelekeo sasa, mbona hakuna vyama vingine hapa?

yaani huyu KadaMpinzani yuko all over na analeta tu mambo ya sisiemu? hii JF imekosa mwelekeo. BTW mbona watu wanakuwa banned kisha wanarudi na majina mengine?
 
Kuhusu Kada, sio tu yupo all over the place, mimi saa nyingine anayoandika SIELEWI!

Kuhusu CCM, ningekushauri ulete mawazo mmbadala na endelevu kama unayo!
 
Back
Top Bottom