KATIBA mpya HAITAELEWEKA

VUTA-NKUVUTE

JF-Expert Member
Nov 25, 2010
6,135
17,802
Amini usiamini,Katiba mpya itakuwa ngumu sana.Ibara zake zitakuwa hazitafsiriki nje ya Mahakama.Kwanini? Nimetafakari kwa kina sana juu ya waliopo kwenye Tume ya Maoni ya Katiba Mpya ambayo ina wajibu,pamoja na mambo mengine,wa kuandaa Rasimu ya Katiba mpya. Kwenye Tume hiyo inayoongozwa na Jaji Joseph Sinde Warioba,yumo Profesa Palamagamba J.A.M.Kabudi aliyekuwa Mkuu wa Kitivo cha Sheria-UDSM.Pia,yumo Dr.Sengondo Mvungi.Achilia mbali Jaji Mkuu Mstaafu Agustino Ramadhani.

Ni hawa hawa walioshiriki kuiandaa na kuiandika Sheria ya Mazingira ya Tanzania(kati ya sheria ngumu kueleweka na kutekelezwa Tanzania). Wameandika vitu vingi mno na vyenye mizungukozunguko ya hapa na pale humohumo.Haieleweki mapema na vyema.

Hiyo ni tisa,kumi ni Jaji Joseph Sinde Warioba.Huyu,akiwa pamoja na Jaji Bomani na wanatimu wengine,waliandika sheria ndefu na ngumu ya Bahari (The Law of the Sea,1982).Ni hapo walipotunukiwa hadhi ya 'u-jaji' kama heshima. Sheria hii haitafsiriki kirahisi bila msaada wa kimahakama.Ngumu sana sheria hiyo.

Hoja yangu hapa ni kwamba,Katiba mpya itakuwa ngumu kumeza.Yatafichwa mambo mengi,hapa katikati, kama ilivyo ile ya 1977 inayoendelea kutumika.Na kama Serikali hii dhalimu ya CCM itaendelea kuwa madarakani huku ikiidhibiti Mhakama kama ilivyo sasa,itakuwa 'imekula' kwetu.Tutakuwa hatuna pa kukimbilia.Mahitaji yetu ya Katiba mpya yatakuwa ni bure.Tutajuta kwakweli kupigia chapuo Katiba mpya. Na tujiandae kwa picha hii kwa jinsi tutakavyoweza.
 
Back
Top Bottom