Acha hangaya,hata nyerere alikuwa anafanya hivyo,elewa mamlaka ya uteuzi ni ya rais tu huwa hayakaimiwi
Basi makamu wa rais apande Ndege akafanye kazi za rais huko nje maana Samia anakutana na Kamala Harris huko kama rais wa JMT.
Iko hivi kikatiba Kuna mambo makamu wa rais hawezi kufanya hata kama anakaimu urais, kwa mfano hawezi kutengua teuzi za rais na wala hawezi teua yeyote.
Hawezi vunja bunge, wala kuvunja Baraza la mawaziri au kufukuza mkuu wa majeshi etc
Sidhani kama wewe ulikuwa unalijua Bunge la Speaker Sitta. Unajua kwanini Speaker Sitta hakupitishwa tena kugombea kiti cha Speaker baada ya uchaguzi mkuu uliofutia?
Speaker Sita hakuwa na mahusiano mazuri na JK, na vile JK alikuwa ameshachafuka akawa hana nguvu ya kulidhibiti bunge.
Wewe si unaamini Katibu wa Bunge (ambaye ni mteule wa Rais) ndiye anayelisimamia Bunge? Imekuwaje tena?
Katibu wa bunge anafanya kwa maagizo ya rais, kama rais mwenyewe kashaingiza ubaridi yeye anafanyaje? Unajua uhasama uliokuwa ndani ya ccm wakati huo wa JK?
It doesn’t make any sense! Ubaridi wa kujisababishia kupoteza control ya Bunge?
Unauliza au unapigia jibu mstari? Wakati huo Mkapa, Kinana nk walikwenda kwenye kikao cha ccm cha kuondoa mpasuko, lakini kikao hicho kilivunjika baada ya wajumbe kutukanana mpaka matusi ya nguoni. Katika mazingira ya uhasama wa hivyo unategemea nguvu za kulidhibiti bunge zitoke wapi?
Kubali tu, Katibu wa Bunge hana uwezo wa kulidhibiti Bunge, under any circumstances!
Over years ofisi makamu wa rais has done little at all. Some have served as surrogates wakati rais akiwa nje ya nchi. In practice, makamu wa rais na ofisi yake is merely the spillover of unwanted or extra presidential responsibilities kama kukata tepe, nk na ku-balance power between Tanzania Mainland and Zanzibar (though baada ya uchaguzi the position becomes useless in practice). Kwangu, ofisi ya makamu ya rais is merely ceremonial and probably should be abolished kama sehemu ya kubana matumizi as we already have prime minister office. Very unlikely though. Maybe baada ya Magufuli kufariki wengi watafikiria zaidi when deciding who should the vice president.
Kama ni ushindi ulikuwa unasaka kwenye hili ww ndio mshindi. Lakini ukweli uko wazi.
Hiyo nafasi ya makamu ni kivuli tu. Umuhimu wake unaonekana pale anapofariki raisi kwamba tusiwe na uchaguzi. Raisi akiwa hai makamu wake ni kama hayupo tu. Huoni kila baya la awamu ya 5 anatajwa JPM na sio samia.Rais wa Tanzania anapata wapi uhalali wa kujifanya kwamba yeye ni indispensable (unsubstitutable)? Kwamba Tanzania bila yeye haiwezi kitu chochote?
Kwa mara nyingine tena, nimeona Chifu Hangaya (akiwa Washington, DC) amefanya uteuzi wa viongozi watatu, kama press release niliyoambatanisha inavyoonesha. Kama kawaida anaendelea na ukiukaji wa Katiba yetu.
Kwa mujibu wa Ibara ya 47(1)(c) ya Katiba yetu, Makamu wa Rais atafanya kazi zote za Rais kama Rais hayuko kazini au yuko nje ya nchi. Na kwa mujibu wa Ibara ya 37(6)(b) ya Katiba hiyo hiyo, ili Rais ahesabike kuwa yuko nje ya nchi, lazima awe nje ya nchi kwa muda unaozidi saa ishirini na nne.
Ingawa Ofisi ya Rais wa JMT yaweza kuwa mahali popote ndani ya mipaka ya JMT, katu haiwezi kuwa mahali popote tu duniani, kama Chifu Hangaya anavyotaka kuifanya. Ni lazima iwe ndani ya mipaka ya nchi yetu.
Vilevile, nchi haiwezi kuwa na Rais zaidi ya mmoja kwa wakati mmoja. Rais awapo nje ya nchi kwa muda unaozidi saa ishirini na nne, Makamu wa Rais (au Waziri Mkuu, endapo Makamu wa Rais naye hayupo) ndiye Rais wa nchi kwa kipindi hicho (Kaimu Rais)! Period. Why is she so insecure?
Hivi, Katiba ya Tanzania ipo ili itusaidie, kama kila uchao inasiginwa na wale walioapa kuilinda?
View attachment 2188837
Basi makamu wa rais apande Ndege akafanye kazi za rais huko nje maana Samia anakutana na Kamala Harris huko kama rais wa JMT.
Iko hivi kikatiba Kuna mambo makamu wa rais hawezi kufanya hata kama anakaimu urais, kwa mfano hawezi kutengua teuzi za rais na wala hawezi teua yeyote.
Hawezi vunja bunge, wala kuvunja Baraza la mawaziri au kufukuza mkuu wa majeshi etc
Nakumbuka wakati Mkapa akiwa Rais aliwahi kuugua na kutibiwa uswis kwa miezi kama mitatu,na itakumbukwa Mkapa alijiwekea utaratibu wa kuhutubia taifa kila mwisho wa mwezi. Ninakumbuka vizuri pamoja na Rais Mkapa kutokuwepo kwa sababu ya matibabu bado aliendelea kutoa hotubs hi yeye akiwa uswis wakati makamu wa Dr Dr.Shein yupo. Kwa hiyo bila shaka ni kawaida.
Mkuu JokaKuu, uko very right kwenye mengi...Tunatakiwa tujiulize maswali haya:-
1. Je, Raisi hayuko kazini?
2. Je, Raisi yuko nje ya nchi?
..Kwa maoni yangu, Makamu wa Raisi anapokaimu atatekeleza mambo ambayo utekelezaji wake unahitaji uwepo wa Raisi "PHYSICALLY."
..Kwa mfano, tendo la kuapisha Wateuliwa linaweza kufanywa na Makamu wa Raisi as Acting President. Lakini sidhani kama Acting President anaweza kuteua.
..Makamu wa Raisi ambaye ni Acting President anaweza kusaini mswada kuwa sheria, lakini sidhani kama anaweza kusaini mswada ambao Raisi mwenyewe hajiuridhia.
..Tukirudi kwenye teuzi za Raisi, suala hilo huwa ni mchakato, na tangazo linapotoka mara nyingi ni kuwa Rais alishiriki ktk hatua mbalimbali na alishatoa uamuzi.
..Mwisho, Ssh yuko ktk ziara nchini Marekani. Yuko nje kwa zaidi ya MASAA 24, je ina maanisha Ssh huko aliko amekuwa sio Raisi wa Tanzania?
..Nadhani mtoa mada alitakiwa kusoma vifungu vya katiba zaidi ya hivi alivyovileta, na zaidi kudurusu waandishi wa katiba yetu walilenga nini walipoandika kifungu kinachohusiana na Kukaimisha nafasi ya Raisi.
Cc Nguruvi3, Pascal Mayalla, Petro E. Mselewa , Pulchra Animo
Mahakama zenyewe zipo wapi brother? haya ni matawi ya CCM yote Bunge na MahakamaShida ni upinzani kutokuwa na viti vya kutosha Bungeni. Impeachment trial ya Rais hufanywa na Bunge, sio mahakama!