Katiba inaonesha Rais akiwa nje ya nchi majukumu yanabaki kwa Makamu. Kwanini Rais anatoa 'press' akiwa nje?

Wanafanya haya yote kwa sababu wao kila kitu wakitakacho kinapatikana kwa gharama za Serikali. Watajuaje matatizo ya Watanzania wakati wao hawayaishi hayo matatizo?
 
Acha hangaya,hata nyerere alikuwa anafanya hivyo,elewa mamlaka ya uteuzi ni ya rais tu huwa hayakaimiwi

That isn’t necessarily the point of contention here. The president isn’t supposed to discharge her traditional duties (work) from a foreign country!

Nyerere alifanya uteuzi wa viongozi gani akiwa nje ya nchi?
 
Basi makamu wa rais apande Ndege akafanye kazi za rais huko nje maana Samia anakutana na Kamala Harris huko kama rais wa JMT.

Iko hivi kikatiba Kuna mambo makamu wa rais hawezi kufanya hata kama anakaimu urais, kwa mfano hawezi kutengua teuzi za rais na wala hawezi teua yeyote.
Hawezi vunja bunge, wala kuvunja Baraza la mawaziri au kufukuza mkuu wa majeshi etc
 
Rais hapaswi kutekeleza majukumu yake ya kawaida ya Rais akiwa ughaibuni. That’s a national security issue!
 
Sidhani kama wewe ulikuwa unalijua Bunge la Speaker Sitta. Unajua kwanini Speaker Sitta hakupitishwa tena kugombea kiti cha Speaker baada ya uchaguzi mkuu uliofutia?

Speaker Sita hakuwa na mahusiano mazuri na JK, na vile JK alikuwa ameshachafuka akawa hana nguvu ya kulidhibiti bunge.
 
Speaker Sita hakuwa na mahusiano mazuri na JK, na vile JK alikuwa ameshachafuka akawa hana nguvu ya kulidhibiti bunge.

Wewe si unaamini Katibu wa Bunge (ambaye ni mteule wa Rais) ndiye anayelisimamia Bunge? Imekuwaje tena?
 
Wewe si unaamini Katibu wa Bunge (ambaye ni mteule wa Rais) ndiye anayelisimamia Bunge? Imekuwaje tena?

Katibu wa bunge anafanya kwa maagizo ya rais, kama rais mwenyewe kashaingiza ubaridi yeye anafanyaje? Unajua uhasama uliokuwa ndani ya ccm wakati huo wa JK?
 
Katibu wa bunge anafanya kwa maagizo ya rais, kama rais mwenyewe kashaingiza ubaridi yeye anafanyaje? Unajua uhasama uliokuwa ndani ya ccm wakati huo wa JK?

It doesn’t make any sense! Ubaridi wa kujisababishia kupoteza control ya Bunge?
 
It doesn’t make any sense! Ubaridi wa kujisababishia kupoteza control ya Bunge?

Unauliza au unapigia jibu mstari? Wakati huo Mkapa, Kinana nk walikwenda kwenye kikao cha ccm cha kuondoa mpasuko, lakini kikao hicho kilivunjika baada ya wajumbe kutukanana mpaka matusi ya nguoni. Katika mazingira ya uhasama wa hivyo unategemea nguvu za kulidhibiti bunge zitoke wapi?
 
Nakumbuka wakati Mkapa akiwa Rais aliwahi kuugua na kutibiwa uswis kwa miezi kama mitatu,na itakumbukwa Mkapa alijiwekea utaratibu wa kuhutubia taifa kila mwisho wa mwezi. Ninakumbuka vizuri pamoja na Rais Mkapa kutokuwepo kwa sababu ya matibabu bado aliendelea kutoa hotubs hi yeye akiwa uswis wakati makamu wa Dr Dr.Shein yupo. Kwa hiyo bila shaka ni kawaida.
 
Over years ofisi makamu wa rais has done little at all. Some have served as surrogates wakati rais akiwa nje ya nchi. In practice, makamu wa rais na ofisi yake is merely the spillover of unwanted or extra presidential responsibilities kama kukata tepe, nk na ku-balance power between Tanzania Mainland and Zanzibar (though baada ya uchaguzi the position becomes useless in practice). Kwangu, ofisi ya makamu ya rais is merely ceremonial and probably should be abolished kama sehemu ya kubana matumizi as we already have prime minister office. Very unlikely though. Maybe baada ya Magufuli kufariki wengi watafikiria zaidi when deciding who should the vice president.
 
Kubali tu, Katibu wa Bunge hana uwezo wa kulidhibiti Bunge, under any circumstances!
 
Over years ofisi makamu wa rais has done little at all. Some have served as surrogates wakati rais akiwa nje ya nchi. In practice, makamu wa rais na ofisi yake is merely the spillover of unwanted or extra presidential responsibilities kama kukata tepe, nk na ku-balance power between Tanzania Mainland and Zanzibar (though baada ya uchaguzi the position becomes useless in practice). Kwangu, ofisi ya makamu ya rais is merely ceremonial and probably should be abolished kama sehemu ya kubana matumizi as we already have prime minister office. Very unlikely though. Maybe baada ya Magufuli kufariki wengi watafikiria zaidi when deciding who should the vice president.

Yale mazoea kwamba Makamu wa Rais has always been of very little importance yametutokea puani safari hii. Now we know, a weak VP is risky to the country!
 
Hi
Rais wa Tanzania anapata wapi uhalali wa kujifanya kwamba yeye ni indispensable (unsubstitutable)? Kwamba Tanzania bila yeye haiwezi kitu chochote?

Kwa mara nyingine tena, nimeona Chifu Hangaya (akiwa Washington, DC) amefanya uteuzi wa viongozi watatu, kama press release niliyoambatanisha inavyoonesha. Kama kawaida anaendelea na ukiukaji wa Katiba yetu.

Kwa mujibu wa Ibara ya 47(1)(c) ya Katiba yetu, Makamu wa Rais atafanya kazi zote za Rais kama Rais hayuko kazini au yuko nje ya nchi. Na kwa mujibu wa Ibara ya 37(6)(b) ya Katiba hiyo hiyo, ili Rais ahesabike kuwa yuko nje ya nchi, lazima awe nje ya nchi kwa muda unaozidi saa ishirini na nne.

Ingawa Ofisi ya Rais wa JMT yaweza kuwa mahali popote ndani ya mipaka ya JMT, katu haiwezi kuwa mahali popote tu duniani, kama Chifu Hangaya anavyotaka kuifanya. Ni lazima iwe ndani ya mipaka ya nchi yetu.

Vilevile, nchi haiwezi kuwa na Rais zaidi ya mmoja kwa wakati mmoja. Rais awapo nje ya nchi kwa muda unaozidi saa ishirini na nne, Makamu wa Rais (au Waziri Mkuu, endapo Makamu wa Rais naye hayupo) ndiye Rais wa nchi kwa kipindi hicho (Kaimu Rais)! Period. Why is she so insecure?

Hivi, Katiba ya Tanzania ipo ili itusaidie, kama kila uchao inasiginwa na wale walioapa kuilinda?

View attachment 2188837
Hiyo nafasi ya makamu ni kivuli tu. Umuhimu wake unaonekana pale anapofariki raisi kwamba tusiwe na uchaguzi. Raisi akiwa hai makamu wake ni kama hayupo tu. Huoni kila baya la awamu ya 5 anatajwa JPM na sio samia.
 
Acha kudanganya watu ujinga wako na hutaji ibara yoyote inayoseea unayosema. kinyume chake ibara ya 47(1)(c) inasema wazi kwamba Rais akiwa hayupo Makamu wa Rais anafanya kazi zote za Urais na ninainukuaa hapa chini,

"Kutakuwa na Makamu wa Rais ambaye atakuwa ndiye Msaidizi Mkuu wa Rais kuhusu mambo yote ya Jamhuri ya Muungano kwa jumla, na atafanya kazi zote za Rais kama Rais hayuko kazini au yuko nje ya nchi."

Hivyo hakuna kazi hata moja Makamu wa Rais hatakiwi kufanya sasa hivi. Vita ikitokea dakika nne zinazokuja Philip Mpango ataamuru majeshi yamchape adui.

Basi makamu wa rais apande Ndege akafanye kazi za rais huko nje maana Samia anakutana na Kamala Harris huko kama rais wa JMT.

Iko hivi kikatiba Kuna mambo makamu wa rais hawezi kufanya hata kama anakaimu urais, kwa mfano hawezi kutengua teuzi za rais na wala hawezi teua yeyote.
Hawezi vunja bunge, wala kuvunja Baraza la mawaziri au kufukuza mkuu wa majeshi etc
 
Ibara ya 47(1)(c) inasema wazi kwamba Rais akiwa hayupo Makamu wa Rais anafanya kazi zote za Urais na ninainukuaa hapa chini,

"Kutakuwa na Makamu wa Rais ambaye atakuwa ndiye Msaidizi Mkuu wa Rais kuhusu mambo yote ya Jamhuri ya Muungano kwa jumla, na atafanya kazi zote za Rais kama Rais hayuko kazini au yuko nje ya nchi."

Hivyo hakuna kazi hata moja Makamu wa Rais hatakiwi kufanya sasa hivi.

Vita ikitokea dakika nne zinazokuja Philip Mpango ataamuru majeshi yamchape adui.

Nakumbuka wakati Mkapa akiwa Rais aliwahi kuugua na kutibiwa uswis kwa miezi kama mitatu,na itakumbukwa Mkapa alijiwekea utaratibu wa kuhutubia taifa kila mwisho wa mwezi. Ninakumbuka vizuri pamoja na Rais Mkapa kutokuwepo kwa sababu ya matibabu bado aliendelea kutoa hotubs hi yeye akiwa uswis wakati makamu wa Dr Dr.Shein yupo. Kwa hiyo bila shaka ni kawaida.
 
..Tunatakiwa tujiulize maswali haya:-

1. Je, Raisi hayuko kazini?

2. Je, Raisi yuko nje ya nchi?

..Kwa maoni yangu, Makamu wa Raisi anapokaimu atatekeleza mambo ambayo utekelezaji wake unahitaji uwepo wa Raisi "PHYSICALLY."

..Kwa mfano, tendo la kuapisha Wateuliwa linaweza kufanywa na Makamu wa Raisi as Acting President. Lakini sidhani kama Acting President anaweza kuteua.

..Makamu wa Raisi ambaye ni Acting President anaweza kusaini mswada kuwa sheria, lakini sidhani kama anaweza kusaini mswada ambao Raisi mwenyewe hajiuridhia.

..Tukirudi kwenye teuzi za Raisi, suala hilo huwa ni mchakato, na tangazo linapotoka mara nyingi ni kuwa Rais alishiriki ktk hatua mbalimbali na alishatoa uamuzi.

..Mwisho, Ssh yuko ktk ziara nchini Marekani. Yuko nje kwa zaidi ya MASAA 24, je ina maanisha Ssh huko aliko amekuwa sio Raisi wa Tanzania?

..Nadhani mtoa mada alitakiwa kusoma vifungu vya katiba zaidi ya hivi alivyovileta, na zaidi kudurusu waandishi wa katiba yetu walilenga nini walipoandika kifungu kinachohusiana na Kukaimisha nafasi ya Raisi.

Cc Nguruvi3, Pascal Mayalla, Petro E. Mselewa , Pulchra Animo
Mkuu JokaKuu, uko very right kwenye mengi.
  1. Rais anahesabika yuko nje ya nchi, anapokuwa nje ya mipaka ya JMT, na nchi inakuwa chini ya Makamo wa Rais ambaye anakuwa ni kaimu rais.
  2. Rais wa Tanzania ni executive president, yaani rais Mtendaji, Kwa mujibu wa katiba yetu ya JMT ya Mwaka 1977, rais wa JMT anaweza kushauriwa lakini kwenye kufikia maamuzi, yeye kama yeye, halazimiki kufuata ushauri wa yeyote.
  3. Hivyo hata wakati Rais wa JMT yuko nje ya nchi na nchi inakuwa chini ya Makamo wa Rais au Kaimu rais, Kaimu huyo ni just ceremonial only hawezi kufanya uamuzi wowote, au kusaini document yoyote inayohitaji presidential seal. Hivyo Kaimu rais hawezi kuteua mtu yoyote au kusaini document yoyote inayohitaji saini ya Rais.
  4. Enzi za Nyerere, tulikuwa na sheria ya presidential preventive detention order iliyokuwa inasainiwa na Rais wa JMT kumhifadhi kizuizini indefinately mtu yoyote hatari Kwa usalama wa taifa bila kuelezwa sababu wala kufikishwa mahakamani.
  5. Ikatokea Nyerere yuko nje ya nchi, nchi ikawa chini ya Makamo wa Rais, enzi hizo, Abdul Kumbe, kuna mhuni mmoja akasumbua, Usalama wakamdaka na kumsweka kizuizini, Jumbe akaisaini Ile presidential preventive detention order.
  6. Ndugu wa mhusika wakazuiliwa kumuona, hawajui kosa lake, hajafikishwa mahakamani. Mke wa mhusika akapeleka kilio chake kwenye Kamati ya Msaada wa Kisheria, iliyokuwa chini ya Kitivo cha Sheria, FoL, cha Chuo Kikuu cha Dar es Salaam, UDSM.
  7. Prof. Issa Gulam Hussein Shivji, Kwa kushirikisha na Prof. Gamaliel Mgongo Fimbo, na Prof. Chris Peter Mains, wakaishika hii kesi.
  8. Wakafungua shauri la court review kuomba prerogative order ya habeas corpus, kuomba mtuhumiwa kama anakosa, afikishwe mahakamani.
  9. Wanajenga hoja kuwa Ile ni kazi ya rais, Makamo wa Rais hawezi kusaini hati yoyote kwaniaba ya rais. Na mtu yoyote akikamatwa Kwa sababu yoyote, lazima aelezwe kosa lake.
  10. Kina Shivji walishinda, rais awepo au asiwepo, hakuna mtu mwingine yoyote anaweza kutumia presidential seal.
  11. Rais anaweza kufanya chochote popote as long as kiko ndani ya mamlaka yake. Uteuzi ni mamlaka yake anaweza kuteua akiwa popote.
  12. Kwa mujibu wa mkataba wa kimataifa wa Vienna convention, ofisi za ubalozi za nchi zozote zinahesabika ni ndani ya nchi husika. Zile press release za uteuzi kutokea Marekani, zina anuani ya ubalozi wetu wa Marekani, hivyo rais yuko sahihi, kumteua yoyote, akiwa popote.
  13. Hata Ikulu yetu ni mahali popote rais wetu anapoweza kufanyia kazi ya urais.
  14. Kiswahili cha Kisiasa Kwa Watanzania: Ikulu sio Eneo Specific, ni Makazi ya Rais, Tuna Ikulu ya Magogoni, Chamwino, Sasa Hadi Ikulu ya Chato!
  15. Hivyo Kwa hizi 2 weeks ambazo Rais Samia atakuwa Marekani, pia atakuwa anaendelea na kutimiza majukumu yake ya urais akiwa Ikulu ndogo ya ziarani Marekani.
P.
 
Back
Top Bottom