Bome-e
JF-Expert Member
- Jan 3, 2014
- 17,104
- 26,070
"Katika hali ya kunishangaza, nilikuwa nabadilishana mawazo na mzungu mmoja raia
wa Ujerumani kwenye N.G.O yake. Katamka maneno yaliyonistaajabisha.
Tumeongea mambo mengi lakini baadae tukaanza kuongelea siasa. Akasema kuna
yule aliekuwa waziri mkuu anaitwa Lowasa, nimeona sasa mnampenda sana. Mimi
nikamjibu inaonekana kuna Watanzania wanampenda awe Rais. Yule Mzungu
akaniuliza, si yule aliejiuzuru kwa sababu ya Corruption?, nikamjibu ndie huyo.
Akasema, wakati ule alionekana amekula Rushwa, sasa anataka kuwa Rais na watu
wanamuunga mkono!, akaongezea kwa kusema how can you easily forget?, how can
you easily change your mind?, yaani mnawezaje kuwa wasahaulifu namna hii,
mnawezaje kubadili fikra zenu haraka hivi juu yake?, hapo mimi nikabaki na
kigugumizi. Akaongeza, au Lowasa amewahi kuwaelezea uhusika wake na hizo
corruption?, mimi nikamjibu hapana. Akasema tena, Or was he cleared by the court?
yaani, je Mahakama iliona hana hatia?, nikamjibu kesi haijawahi kwenda Mahakamani.
Akauliza, then which criteria do you use to support him? Nikamjibu kwakweli sijui wananchi wanatumia kigezo gani.
Yule mzungu akasema, anyway, you are such amazing country, with this style it may
take you so many years to change."
Sent as received.
Pamoja na kwamba ni kastori kakutunga lakini ndio ukweli,how can we easily forget?kama aliachia ngazi kuwalinda maswahiba zake au kulinda chama atashindwa vipi kuwalinda akiwa rais?
Hivi kuwajibika ndio huku?