Kati ya vyuo vikuu bora 400 duniani cha Afrika ni kimoja!

tatanyengo

JF-Expert Member
Mar 30, 2011
1,134
280
Imotolewa orodha ya vyuo vikuu 400 bora duniani (top 400 universities worldwide) lakini cha kusikitisha ni kwamba ni chuo kimoja tu kutoka Afrika kilichoingia katika orodha hiyo. Chuo pekee cha Afrika kati ya vyuo 400 bora ni University of Cape Town cha Afrika Kusini ambacho kimechukua nafasi ya 156. Shame on Africa!
 
Dah!udsm,mzumbe na mbwembwe zote walizo nazo wameangukia pua.bora hata sisi wasuaso hatunaga makuu.
 
Unaweza kutupa source yako? how does Sussex University (england) rank?
 
Wewe uliyeweka hii thread baada ya kugundua hivyo, umejifunza nini na unatoa ushauri gani? au ndo umeweka thread watu waanze kubishana?
 
Let's be honest,unadhani ni vigezo gani wanatumia ili kupata vyuo bora?
Kazi za vyuo vikuu zinatambulika. Ambazo ni Reseach,consultancy,na training/teaching.
Sasa wote tunatambua kuwa idadi ya vyuo vikuu duniani kwa sasa ni kubwa. Na ushindani nao ni mkubwa. Na vyuo vyetu vingi hapa TANZANIA kama si vyote vina matatizo yanayofanana au kukaribia kufanana. Kuna matatizo kama ya teaching facilities,uhaba wa walimu,theater na halls za kusomea. Hapo sijazungumzia accomodations.
Na natumai kama vitu hivyo vitakuwepo basi ndio tunaweza kuja na ushindani wa vyuo bora duniani.
Na hilo sio tu tatizo la Tz bali ni tatizo la Afrika.
 
mkuu hapo kwenye accomodation pananiuma sana sana,yani unakuta chuo kinajina na baadhi ya wahitimu wake wako vitengoni sasa ila ukiangalia huu mfumo wa kubebana yani unasikitisha sana.
 
Wewe uliyeweka hii thread baada ya kugundua hivyo, umejifunza nini na unatoa ushauri gani? au ndo umeweka thread watu waanze kubishana?

ajatumia huu mfumo wa kuliona tatizo,kuuliza kwanini imekua hivyo baada ya kupata majibu basi unayaghulikia.Huyu mtoa huu uzi lengo lake tuanze kubishana maana uzi wake una nyufa nyingi.
 
Dah!udsm,mzumbe na mbwembwe zote walizo nazo wameangukia pua.bora hata sisi wasuaso hatunaga makuu.

unasemaje wewe? Tz udsm ndio kipo juu, hata kama kiliporomoka kwenye rank ya dunia, but bado kipo juu kwa Tanzania ukilinganisha na vyuo vingine vya hapa..
 
unasemaje wewe? Tz udsm ndio kipo juu, hata kama kiliporomoka kwenye rank ya dunia, but bado kipo juu kwa Tanzania ukilinganisha na vyuo vingine vya hapa..

kwa kipi cha maana kilichopo hapo udsm?
 
Tunapenda kupata vyeti ndio maana elimu ya vyuo vyetu vikuu haina ubora.Wanaopata hii elimu ktk vyuo vyetu hawana mchango wowote ktk kuboresha mazingira ya jamii,siasa na uchumi wa nchi yetu.
#.Je,kama tatizo la vyuo vyetu ni vifaa vya kufundishia,walimu na malazi.Unadhani ni kiasi gani cha pesa kinaweza tatua haya matatizo?Bila uadilifu hata bajeti yote ya nchi ielekezwe kwenye elimu,hakuna mabadiliko chanya tutakayopata.
#.Mfumo wetu wa elimu umejaa ubabaishaji,kwani ni bora kukawa na elimu maalumu kabla ya kukimbilia degree.Mafano:tukaweka mkazo katika vyuo vinavyosimamia misingi ya ujuzi kwanza(Polytechnic Colleges) badala ya hivi vya nadharia(Vyuo vikuu)..Kule England walivibadili majina vyuo vya ujuzi lakini mising ya vyuo hivyo ikabak palepale.Chuo kikuu ni jina tu,ila maana yake itatimia kama,msomi m1 kutoka huko chuo kikuu ataweza badili rasilimali zilizomzunguka na kuwa tija kwa jamii yake.
CHAGIZO:Msomi yeyote yule anatakiwa awe nguzo muhimu ktk jamii yake(famili na nchi yake) kwanza,hapo ndipo faida ya usomi wake itakapojionyesha.
 
Vyuo vikuu kumi bora hivi hapa:

1. University of Cambridge (United Kingdom)

2. Harvard University (United States)
3. Massachusetts Institute of Technology (United States)
4. Yale University (United States)
5. University of Oxford (United Kingdom)
6. Imperial College London (United Kingdom)
7. UCL (University College London) (United Kingdom)
8. University of Chicago (United States)
9. University of Pennsylvania (United States)
10. Columbia University (United States)
 
Back
Top Bottom