nusuhela
JF-Expert Member
- Jan 26, 2014
- 5,736
- 6,972
Swali la kujiuliza ni je, kweli wakati wa mchana watu hawaangalii runinga? Kama hawaangalii vile vipindi vinarushwa kwaajili ya nani?Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa amesema kuwa hata bunge la Uingereza halionyeshwi ''LIVE " kwa muda mrefu kama ilivyokuwa kwa bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ambalo lilikuwa likionyeshwa kuanzia saa 3 asubuhi hadi saa 7 mchana, na kuanzia saa 10 jioni hadi saa 2 usiku na kupelekea watu kutokufanya kazi na badala yake kuamka asubuhi kufuatilia bunge kwa muda wa miezi hadi mitatu.