ChoiceVariable
JF-Expert Member
- May 23, 2017
- 44,736
- 51,589
Fuatilia yanayojiri kwenye Bunge la 12, Mkutano wa 12, Kikao cha 8, leo Septemba 7, 2023.
Ratiba:
Waziri Mkuu Kassim Majaliwa: Namuagiza Naibu Waziri Mkuu kushughulikia suala la ukosefu wa mafuta nchini.
Hati za kuwasilishwa Mezani Maswali kwa Waziri Mkuu Maswali ya kawaida
Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Kassim Majaliwa amekiri uwepo wa changamoto ya uhaba wa mafuta nchini wakati akijibu swali la Rashid Shangazi, Mbunge wa mlalo (CCM) aliyetaka kufahamu mipango ya Serikali katika kukabiliana na changamoto kubwa ya uhaba wa mafuta nchini.
"Kwanza nikiri kwamba tunazo changamoto za upatikanaji wa mafuta nchini kwa sababu baadhi ya vituo kwenye maeneo mbalimbali vimekuwa vikikosa mafuta na watanzania wanaohitaji huduma hii maeneo kadhaa tumeona wakiwa wanalalamika kukosekana kwa mafuta" amesema.
Waziri Majaliwa amesema zipo jitihada kadhaa zinazofanywa na Serikali kuondoa tatizo la uhaba wa upatikanaji wa mafuta na amemuagiza Naibu Waziri Mkuu kushughulikia suala hili, muhimu zaidi nishati yenyewe ipatikane nchini.
Hivi shida kubwa kutoka Kwa wadau wa mafuta wanasema ni nini? Maana Kwa maelezo ya Waziri mkuu Kuna uhaba wa mafuta lakini ewura wanasema mafuta yapo,Je Ewura wanadanganya?