Kashfa sekta ya Elimu: Kwa hili CHADEMA mmekurupuka

Mnahangaika kutafuta nani kasababisha hayo yote,jibu ni serikali hii ilimdharau sana mwalimu, akadharaulika, akadhalilika sana na watu wakaaminishwa kwamba ualimu ni kazi isiyo na heshima, isiyo na staha, isiyostahili malipo mazuri, ni kazi ya shida, ni kazi ya wachovu. Sasa nadhani kwa matokeo ya mwaka huu ambapo asilimia TANO tu! (5%) ndio waliopata div 1,2 na 3 na (95%) ni wale waliopata div 4 na 0 watu wenye akili wameelewa maana yake ni nini matokeo haya. Mwaka 2008 walimu walitaka kugoma serikali ikatishia walimu na kuwalazimisha kurudi kazini mara moja kwa lugha ya gadhabu kutoka kwa mkuu wa kaya huku wakionyenyewa nguvu ya dola na akaenda mbali kwamba akasema hata kura zao kama wafanyazi hahitaji. Walim wakatii amri wakarudi kazini ila HAKUNA KAZI BALI UHARIBIFU (mgomo baridi). Walimu hawakupenda malumbano sana safari hii kwa kuwa matatizo yao sio ya jana wala juzi ni miaka mingi na walikuwa wamevumilia kwa kuipenda nchi yao ladba siku moja mambo yakiwa mazuri tutaboreshewa maslahi yetu. Kumbe ni danganya toto wanajineemesha wenyewe na kumsahau mwalimu ambaye kwa kifupi ndiye aliye kazini tangu UHURU kujenga taifa la TANZANIA kwa bei ya jasho lake kwa kuwafundisha watanzania wa fani mbalimbali madaktari, marubani, maprofesa, mashee, mapandri, wataalamu wa kilimo na aina kila aina ili kujenga taifa kubwa lenye nguvu lenye utajiri mwingi wa mali na tamaduni na lenye kujitemea siku za usoni lakini imani ya kukumbukwa walimu ikafutwa wakapewa zawadi ya kudharauliwa.Bila shaka yoyote mwalimu katufikisha pabaya mno tupende tusipede ingawa matatizo mengine sio kwamba hayapo.Ushauri wangu serikali iwaombe radhi walimu na iboreshe maslahi yao. Watu wengine hawapendi kuambiwa ukweli ila hamna jinsi. kila siku ooh! vitabu, vyumba vya madasa ohh! maabara nani kawaloga nyiye viongozi wa taifa hili? huu si muda wa kutafuta mahali pa kujificha.
 
Kwa hili, CHADEMA mmekurupuka. Bora hata Lowassa aliyemwomba Rais kuunda Tume. Badala ya kuitisha maandamano, undeni tume huru ya pamoja, kati ya walimu, wazazi na wanafunzi. Kuwe na tume huru kila kata, wilaya na mkoa. Kisha tume hizo zifanye majumuisho ya vikao vitakavyoendeshwa. Mnataka kuwakomboa Watanzania? Wakomboeni kwa mazungumzo na maazimio. Maandamano ni hasira za mkizi, huishia ukingoni.
kWANI KIINI CHA TATIZO HAKIJULIKANI HADI LEO MIAKA 51 YA UHURU. UNAJENGA SHULE HAZINA WALIMU, VITABU, MAABARA ETC. UNATEGEMEA NINI. WALIMU HAO WACHACHE UNAWADHULUMU. HIYO TUME HAINA FAIDA YOYOTE KWAVILE KIINI CHA TATIZO KINAJULIKANA!!!!!
 
Kwa hili, CHADEMA mmekurupuka. Bora hata Lowassa aliyemwomba Rais kuunda Tume. Badala ya kuitisha maandamano, undeni tume huru ya pamoja, kati ya walimu, wazazi na wanafunzi. Kuwe na tume huru kila kata, wilaya na mkoa. Kisha tume hizo zifanye majumuisho ya vikao vitakavyoendeshwa. Mnataka kuwakomboa Watanzania? Wakomboeni kwa mazungumzo na maazimio. Maandamano ni hasira za mkizi, huishia ukingoni.

Tangia serikali hii ya awamu ya nne iingie madarakani ni tume ngapi zimeundwa na kudai ni huru pasipokurudi na majibu na kubaki kimya ama ajibu yasiyoeleweka ama mhusika kutowajibishwa? Then ukishajiuliza hilo jua lowasa ndo mkurupukaji ambae hajui kuunganisha mwenendo wa mambo tulikotoka
 
Kaka tatizo siyo waziri, kwa serikali ya ccm, hata kama waziri angelikuwa Dr Silaa, hakuna la maana ambalo lingelifanyika, tatioz ni mfumo mbovu wa elimu ambao umeasisiwa na sera mbovu za elimu zinazotungwa na serikali ya ccm. Kawambwa hana la kufanya zaidi ya kufuata ambayo yameandikwa kwenye ilani za ccm.

Kama nimekuelewa sawa sawa Ilani ya CCM ndiyo chanzo ya huu uzo wa zero above 60%?
 
Mwaka 2010 ndio majibu yalianza kuwa mabaya ingawa hayawezi kulingana kwa vyovyote vile na matokeo ya sasa. Kikaundwa kikosi kazi kikashirikisha pande zote muhimu kazi ikafanywa kwa ustadi mkubwa na mapendekezo yakatolewa na hela nyingi zilitumiwa kufanya hii kazi. Mapendekezo hayakufanyiwa kazi yako makabatini serikali inategemea miujiza, kwahio Tume haihitajiki hata kidogo kwasababu sababu za kufeli zinajulikana. Nashauri wafanye hima kufanyia kazi hayo mapendekezo. Bila hivyo tunafuga bomu litakalolipuka sio muda mrefu. Usiwashangae CHADEMA, shauri nini kifanyike.

hata akishauri serikali siyo sikivu na hakuna kitakachoendelea kama hata tume iliyotumia gharama kubwa wameshindwa kutekeleza majibu ya hiyo tume sidhani kama kuna atakae sikilizwa
 
kwani CHADEMA wanataka kuandamana tena au? kwA stail hiyo inabid nikikimbie hich chama kama ni hoja mwiten wazir wa elimu, walimu pamaoja na wadau wa elimu mjadili tatizo kuandamana tena sasa tutakuwa mazuzu,mabwabwa, au mbulula? kila kitu sisi ni waandamanaji tu!!!!!

Ww mburula hata ukiondoka huna faida kwa upeo wako mdogo wa uelewa.Maana ya accountability ni kwamba endapo kutatokea jambo baya kwenye wizara/idara unayoiongoza aidha kwa uzembe wako au wa walio chini yako unapaswa kuwajibika kwa kujiuzulu.Maandamano ya chadema ni kumshinikiza kawambwa kujizulu kisiasa kwani kagoma kuwajibika.
 
hakuna haja ya tume,tumeona tume nyingi zisizo na maana yoyote, sasa ni maandamano ndio mpango! chadema tunasubili amri yenu tuingie barabarani
 
Naona wewe una kabati la kutosha makabrasha ya tume.....naomba unipe hata report ya tume moja unayoijua na manufaa yake baada ya kutekelezwa.......
Kwa Tanzania yetu hizo reports ni kama gazeti la mwaka jana....likionekana mwaka huu ni kufungiwa mandazi tu.
 
Kwa hili, CHADEMA mmekurupuka. Bora hata Lowassa aliyemwomba Rais kuunda Tume. Badala ya kuitisha maandamano, undeni tume huru ya pamoja, kati ya walimu, wazazi na wanafunzi. Kuwe na tume huru kila kata, wilaya na mkoa. Kisha tume hizo zifanye majumuisho ya vikao vitakavyoendeshwa. Mnataka kuwakomboa Watanzania? Wakomboeni kwa mazungumzo na maazimio. Maandamano ni hasira za mkizi, huishia ukingoni.

Huo uzi hauna maana tume za nini?nani hajui ni kwa nini watoto wetu wamefeli ?labda wewe na Wazir mkuu mstaafu.Tume ili wapate ulaji?ni tume ngapi zimeundwa nchi hii?
 
Kwa hili, CHADEMA mmekurupuka. Bora hata Lowassa aliyemwomba Rais kuunda Tume. Badala ya kuitisha maandamano, undeni tume huru ya pamoja, kati ya walimu, wazazi na wanafunzi. Kuwe na tume huru kila kata, wilaya na mkoa. Kisha tume hizo zifanye majumuisho ya vikao vitakavyoendeshwa. Mnataka kuwakomboa Watanzania? Wakomboeni kwa mazungumzo na maazimio. Maandamano ni hasira za mkizi, huishia ukingoni.

Hivi wewe unaishi nchi gani?! Ni mtu gani usiyejua chanzo cha kufeli kwa wanafunzi hawa?!... Hata ukitoka nje ya geti na kuwauliza vijana watakuambia chanzo cha tatizo. KUUNDA TUME NI WIZI MTUPU!..
 
Kwa hili, CHADEMA mmekurupuka. Bora hata Lowassa aliyemwomba Rais kuunda Tume. Badala ya kuitisha maandamano, undeni tume huru ya pamoja, kati ya walimu, wazazi na wanafunszi. Kuwe na tume huru kila kata, wilaya na mkoa. Kisha tume hizo zifanye majumuisho ya vikao vitakavyoendeshwa. Mnataka kuwakomboa Watanzania? Wakomboeni kwa mazungumzo na maazimio. Maandamano ni hasira za mkizi, huishia ukingoni.
tume ya nini? Kwani. Ni kipi hakijulikani?nikiwa mtaalamu nafahamu fika wanasiasa wanaruhusiwa kuwa na ndoto. Lowassa na wenzake walipata ndoto nzuri ya elimu kwa kila Kata na hata kijiji. Tatizo sio wao waliopaswa kutafsiri ndoto. Walikurupuka vibaya sana ili waonekane walikuwa na ndoto nzuri. Wanajimu tupo tele DUCE Na UDSM,SAUT. HATUHITAJI TUME. CHADEMA WAENDELEE NA SIASA NA MAANDAMANO NA WAULIZE JE MPANGO MKAKATI WA KUFIKIA KILA KATA UPO?NA MALENGO MUDA MFUPI MPAKA MUDA MREFU NI YAPI? KINYUME WAZAZI WATOE SHUKRANI KWA CHECHEMEE KUANDAA KAMBI ZA KUKUZA WATOTO KUWAEPUSHA NA NGONO ZA UTOTONI.
 
Kwa hili, CHADEMA mmekurupuka. Bora hata Lowassa aliyemwomba Rais kuunda Tume. Badala ya kuitisha maandamano, undeni tume huru ya pamoja, kati ya walimu, wazazi na wanafunzi. Kuwe na tume huru kila kata, wilaya na mkoa. Kisha tume hizo zifanye majumuisho ya vikao vitakavyoendeshwa. Mnataka kuwakomboa Watanzania? Wakomboeni kwa mazungumzo na maazimio. Maandamano ni hasira za mkizi, huishia ukingoni.

Tume ya nini? Tatizo lipi kwenye elimu lisilojulikana linalohitaji tume? Kwa kutumia common sense tu unajua kuwa kuwa hayo mambo ya tume ni muendelezo tu wa usanii!
 
Kumbe watanzania wanapenda tume enh? Kwa hili lipo wazi kabisa tume ya nini?
 
tume ya nini?,maandamano ya nini? Vyote kwa Tanzania havijaleta tija,sipingi maandamano ila kama yataleta manufaa,lakini kwa hili la kufeli kuandamana sio suluu,kama kawambwa hataki kuwajibika nawashauri cdm waichukue km point ya kuishitaki serikali ya ccm kwa wananchi(ambao ndio wahanga wa matokeo)naamin itasaidia kuwaamsha wananchi hivyo kuiangusha ccm ktk kila chaguzi na hasa ule mkuu wa 2015.
 
tume ya nini?,maandamano ya nini? Vyote kwa Tanzania havijaleta tija,sipingi maandamano ila kama yataleta manufaa,lakini kwa hili la kufeli kuandamana sio suluu,kama kawambwa hataki kuwajibika nawashauri cdm waichukue km point ya kuishitaki serikali ya ccm kwa wananchi(ambao ndio wahanga wa matokeo)naamin itasaidia kuwaamsha wananchi hivyo kuiangusha ccm ktk kila chaguzi na hasa ule mkuu wa 2015.
 
Kwa hili, CHADEMA mmekurupuka. Bora hata Lowassa aliyemwomba Rais kuunda Tume. Badala ya kuitisha maandamano, undeni tume huru ya pamoja, kati ya walimu, wazazi na wanafunzi. Kuwe na tume huru kila kata, wilaya na mkoa. Kisha tume hizo zifanye majumuisho ya vikao vitakavyoendeshwa. Mnataka kuwakomboa Watanzania? Wakomboeni kwa mazungumzo na maazimio. Maandamano ni hasira za mkizi, huishia ukingoni.

dah!! nimeipenda sana idea yako. ndo maana mi naamini kuna watanzania wengi wenye uwezo mzuri wa kupembua mambo pengine kuliko hata hawa ccm wasiojifunza jipya. wamekalia ideas zao tuu ambazo kila kukicha zina-prove failure. hicho uichoki-suggest ni kizuri, lakini si kwa serikali mbovu kama hii isiyojali ushauri wa wengine. serikali kichwa ngumu kama hii breakfast yake ni maandamano, lunch yake nim kuing'oa madarkani tuu.
ndugu yangu MwanaHaki, hawa ccm na serikali yao hata ukiwapelekea ushauri wa dhahabu hawaufanyii kazi. kwani mangapi yameshafanywa na wataaamu wetu na bado yakaonekana upuuzi tu mbele ya ccm?? acha maandamano yawe ni moja ya nyenzo za kutufikisha huko tunakopataka.
 
Back
Top Bottom