KARLO MWILAPWA
JF-Expert Member
- Apr 10, 2019
- 2,590
- 4,603
Suala la uwekezaji wa bandari limeenda kinyume na matarajio ya wengi walioamini kupitia suala hili watapata uungwaji mkono na vyama vyao vitazidi kukubalika Zaidi lakini imekuwa ni tofauti, na suala hili linawatesa Zaidi waliolikuza kama "agenda" ya kisiasa.
Kuna baadhi ya wanachama wa CHADEMA wakiongozwa na Mdude Nyagali waliotaka kutumia suala hili kuitisha maandamano ambayo kimsingi ni utaratibu wa kufanya fujo kwenye mfumo wa kidemokrasia. Wengi wanatambua demokrasia ni mfumo unaopendelea mijadala zaidi kuliko maandamano lakini CHADEMA walitaka kuitisha maandamano. Hii ikawa ni kiki ya kwanza iliyobuma.
Kuzunguka nchi nzima kujaribu kupotosha habari za nchi kuuzwa na mambo mengine kupitia uwekezaji wa bandari. Baada ya CCM kuingilia kati na kuelimisha Umma na Umma ukaelewa elimu ya uwekezaji wa bandari walioyopewa na CCM kuliko upotoshaji wa CHADEMA. Hiyo ikawa ni kiki ya pili iliyobuma.
Kwa kiki hii kubuma ambayo naweza kusema "it was last kick of dying horse" ni ishara mbaya kwa CHADEMA hususani kipindi hiki ambacho kunatarajiwa kuwa na uchaguzi mdogo katika Jimbo na Mbarali na uchaguzi wa udiwani katika kata mbalimbali.
Je, tutarajie nini?
Tutarajie CHADEMA kugoma kushiriki uchaguzi huu kwa kisingizio hakuna tume huru?
Tutarajie kulaumiwa kwa CCM pale CHADEMA itakaposhindwa Kwa aibu kwenye uchaguzi huo?
Macho na masikio ya watanzania kwa sasa ni kwenye uchaguzi huu mdogo ili wafahamu, nani kaeleweka zaidi kwenye suala la uwekezaji wa bandari, ni CCM au CHADEMA?