Kashfa kubwa CCM Kilimanjaro

STINGER

Member
Oct 18, 2011
41
11
Kashfa kubwa yaikumba CCM Kilimanjaro



Uongozi wa chama cha mapinduzi ccm mkoa wa Kilimanjaro umeingia katika kashfa kubwa baada ya kusemekana ya kuwa imefungua akaunti ya siri isiyo rasmi ambayo inatumika kukusanyia michango ambayo inadaiwa kuingia mifukoni mwa baadhi ya viongozi wa chama hicho.

Taarifa kutoka ndani ya uongozi wa chama hicho ngazi za wilaya na mkoa ikiwemo kutoka baadhi ya viongozi wa chama hicho wakiwemo wale wapya, ni kuwa wamepata taarifa ya kuwa kuna akaunti ambayo inatumiwa na baadhi ya viongozi wa ccm mkoa kukusanya fedha kutoka kwa wadau mbali mbali wengi wao wakiwa ni wafanyabiashara mashuhuri wa mkoa wa Kilimanjaro.

Mmoja wa viongozi hao wa ngazi ya wilaya amesema kuwa katika kufuatilia wamegundua akaunti iliyofunguliwa crdb yenye namba 0061102000043 ambayo katibu wa mkoa jonathan mabiya amaitumia kukusanya michango mbalimbali akidai ni kwa ajili ya ccm jambo ambalo baadhi ya viongozi wansema hawana habari na kaunti hiyo.

Kiongozi mwingine wa ccm ngazi ya mkoa amekiri kupokea taarifa kuhusiana na akaunti hiyo na pia amepata malalamiko kutoka kwa baadhi ya wafanyabiashara wakisema ya kuwa wametumiwa ujumbe na mabiya ya kuwataka wachangie uchaguzi wa mkoa

Kiongozi huyo amesema ya kuwa mfanyabiashara huyo mashuhuri wa mjini oshi ametumiwa ujumbe na katibu huyo akimtaka achangie uchaguzi mkuu kwa kuweka mchango wake kwenye akaunti hiyo iliyoko crdb.



Kiongozi huyo amesema anashangazwa na hatua ya kuombwa mchango huo wakati chama kilitangza kupitia katibu mwenezi shaka ya kuwa chama kiko tayari kwa chaguzi zake zote kuanzia ngazi ya kitongoji, mitaa, kata, wilaya, mkoa hadi taifa

Msururu wa tuhuma kwa

Kiongozi huyo wa mkoa amesema tuhuma hizo ni mwendeleo wa tuhuma nyingi ambazo ccm mkoa haswa katibu wa mkoa wamekuwa wakitajwa kuhusika nazo na nyingi zinahusiana na maswala ya fedha.

Amesema kuwa ziara ya makamu mwenyekiti kinana, mabiya alichangisha wafanyabiashara na baadhi ya viongzoi wa taasisi za serikali fedha akisema ni kwa ajili ya kuandaa futari kwa kinana na wenzake, ajabu ni kwamba taarifa zilizotoka ni kuwa futari hiyo aliandaa kinana yeye kama yeye na sic cm mkao hata redio zote za hapa mkoani zilitangaza hivyo, sasa fedha milioni 8 alizochangisha mabiya kama inavyosemekana zilipatikana kiasi hicho zilikwenda wapi, zilitumika vipi?

Wamasai wa siha

Kashfa nyingine ni ile inayowahusu wamasai kutoka siha ambao inasemekana mabiya aliwafuata na kuwaambia ya kuwa katibu mkuu chongolo anakuja Kilimanjaro hivyo atawaunganisha waonane naye wampongeze kwa kumpata mkuu wa mkoa mpya badala ya kigaigai ambaye wanadai aliwanyanyasa wakati wa sakata la wamasai na wakulima hivi karibuni

Kiongozi huyo anasema kuwa mmoja wa wamasai hao alikwenda kulalamika kwa baadhi ya viongozi ya kuwa mabiya na baadhi ya viongozi walikwedna kuwatembelea huko siha kimya kimya na kuwajulisha ya kuwa ccm iliskia malalamiko yao n arc kigaigai ameondolewa. Msema ji huyo wa wamasai aliendela kusema kuwa kwenye kikao hicho cha siha, mabiya aliwashauri ya kuwa katibu mkuu pamoja na rc mpya watakuwa pamoja katika ziara ya katibu chongolo Kilimanjaro hivyo ni vyema wakapata nafasi ya kuonana nao na kuwapa salamu zao.

Anasema mmasai huyo aliendelea kulalamika ya kuwa aliwashauri watafute zwadi ya kuwapa chongolo n arc mpya ambapo alisema ni vyema zikawa ni fedha ndipo walipochangishana na kupata shilingi milioni 8. Walikubaliana milioni 5 iwe ni zawadi kwa katibu mkuu na milioni 3 iwe ni zawadi kw arc mpya.

Mmasai huyo anasema siku ya kwenda kumuona katibu mkuu ilifika na wakondoka mapema kwenda moshi huku wakijua ya kuwa milioni 8 ambazo waliziwakilisha kwa mabiya tayari zimewafikia walengwa. Mmasai huyo anasema walifika moshi na kwenda moja kwa moja mpaka ofisi ya ccm mkoa na kukuta wanaccm wengi wakiwa tayari kumpokea katibu mkuu.

Anasema walipelekwa moja kwa moja ukumbi mkubwa wa ccm mkoa na kuambiwa katibu mkuu alikuwa hotelini na atakuja kuwaslimaina nao muda si mrefu halafu katibu mabiya akatoweka. Anasema muda si mrefu mabiya alirudi na kusema kuwa katibu mkuu n arc mpya walikuwa na mazungumzo na wageni na kwamba wakimaliza ziara ya kwenda rombo itaanzia huko huko hotelini hivyo katibu n arc hawataweza kuonana nao na wasiwe na wasiwasi zawadi zao zitafika na salamu zao pia zitafika kwa katibu mkuu n arc.

Sasa wale wamasai wanauliza hata kama hawakuonana na wahusika mbona hata salamu za shukrani kuwa wamepata zawadi zao hawajazisikia? Kiongozi huyo wa mkoa anasema kuwa malalamiko hayo yalimfikia hata mwenyekiti wa mkoa boisafi lakini akamezea maana alishaambiwa akimfuatafuata mabiya kama anavyofanya uenyekiti hataupata hivyo boisafi alimezea ili asikose uenyekiti

Kukigawa chama

Kashafa nyingine inayomkabilia mabiya ni kuwa aliund akundi ambalo amekuwa akilitumia kutekeleza kile kinachitwa umafia ndani ay ccm mkoa. Makao makuu ya kundi hilo yako kwenye mgawaha ulioko ccm wilaya ambapo umebandikwa jina Lumumba ndogo au byoro di chenji.

Imedaiwa mabiya na kundi lake wanawalazimisha viongozi wa ngazi mbalimbali wakiwemo wabunge kuopitia hapo hata kama hawan shughuli jambo amalo wengi wamekubaliana nalo kwa shingo upande. Inasemekana wengi wakifika pale hwua wanalazimika kuingia garama za manunuzi ikiwemo ya pombe ili kumnufaisha mabiya ambae anamiliki mgahawa huo kupitia kivuli cha kwa mwanachama aitwae asumani na amabe alimzawadia uenezi wa ccm manispaa.

Kiongozi huyo anasema viongozi wengi wakiwemo wabunge wanalazimika kupitia hapo bila kupenda maana mabiya anawatisha kwa kuwaambia ya kuwa bila yeye na timu yake ubunge watausikia kwenye magazeti.



Hili ndilo lilimpata mwanachama Ibrahim shayo ambaye aligoma kabisa kuhudhuria vikao Lumumba ya moshi kwa kile alichodai ni kama alikuwa anakwazika. Kiongozi huyo anasema shayo alikuwa anapata shid akupitia pale nyakati za usiku ambazo ndiyo mara nyingi wanaojipendekeza wasipoteze nafasi zao hufika. Shayo anasema kukwazika huko kulikuwa kunatokana nay eye angelazimika kupitia hapo akishatoka kuswali Isha halafu apitie mahali ambapo analazimika kununua raundi ya bia au watu wanakunywa bia. Kukataa kwake kulimponza kiasi cha kwamba hata alipogombea ujumbe wa kata yake kweney uchaguzi wa ccm mwaka huu jina lilikatwa.

Kinachompa kiburi mabiya

Baadhi ya wana ccm wanasema kinachompa kiburi mabiya ni vitu viwili;

  • Kauli aliyotoa katibu mkuu chongolo katika wilaya ya mwanga wakati alipokuwa kwenye ziara yake Kilimanjaro pale aliposema kuna wanaomnafikia mabiya ambapo alisema haondoki Kilimanjaro hadi uchaguzi mkuu 2025 uishe
  • Mabiya anatamba waziwazi ya kuwa chama kinamuamini mpaka ngazi ya kamati kuu baada ya kugundua ya kuwa uongozi wa kamati kuu ulifanya makosa kurudisha jina la juma raibu meya wa zamani halafu akapatikana na kashfa. Mabiya anatamba kuwa kuna baadhi ya viongozi wa kamati kuu walisema wanajuta kutokufuata ushauri wake na viongozi wa mkoa wa Kilimanjaro mpaka chama kikaingia kwenye kashfa ya kumpoteza meya kupitai chama hicho
 
Back
Top Bottom