Kasheshe la Mafuta: Dar kimeanza kuwaka, vituo kadhaa vyaanza kutoa mafuta!

Barking dogs never bite! Tanzania hakuna waandamanaji wa kuitoa CCM madarakani. Ni watu wanaoweza kutoa matusi mitandaoni na kupiga makelele meeengi bila utekelezaji. Labda mkodi waarabu wawasaidie.

Kumbe wewe siyo mtanzania ...... wewe sijui ni mpuuzi wa nchi gani
 
Nchi inayumba - CCM haina mwongozo na inasambaratika! Ilikuwa ni comedy ya CCM tu jana huko Bungeni Dodoma. Makamba Mbunge wa CCM na Mwenyekiti wa Kamati ya Nishati na Madini apendekeza hoja juu ya swala hili. Waziri Mkuu akaa kimya; Kamati ya Uongozi ya Bunge yakubaliana na wazo wa kujadili hoja; Wabunge wajadili hoja kwa jazba kubwa - mwishowe waziri Ngeleja [CCM] atoa tamko la Serikali. Jee kulikuwa na haja ya kwenda through usanii huu - Waziri Ngeleja anangojea mpaka hoja iletwe ndio atoe Tamko la Serikali kwa issue ya dharura kwa taifa kama hili? CCM haioni kama hii ni hali ya hatari kwa nchi? Serikali na CCM wameshindwa kuendesha nchi - Nafikiri kuna haja ya kuwa na Tahariri Squarev ya Tanzania!

usanii mtupu!
EWURA ni mamlaka halali na ilikwisha kutoa tamko lakini halikutekelezwa! leo anaibuka mtu mwingine bila kuchukua hatua anatoa tamko lingine la kutishia nyau!!!!depot zinatoa mafuta 24hrs ila vituo vya DAr bado havina mafuta, ina maana wamepuuza tena labda wanasubiri mkwara wa Mkuu wa kaya ili waupuuze nao.
 
Hv chadema wapo wapi muda kama huu?me sielewi kwann hawajaanda maandamano mpk saiv,zaidi ya siku 7??au wao maandamano wanaandaa kma wakiwa wanataka madaraka tu? Suala la jailo wapo kimya suala la mafuta wapo kimya,jaman mananiangusha chadema,andaeni maandamano jmn tuwashinikize hawa wahuni watoke madarakani,imefika muda tuwe kama watu wa london kwa kuchoma hivi vituo vya mafuta na mali za mafisdi pai
Tatizo letu watanzania ni kutaka kutayarishiwa kila kitu. Matatizo upate wewe na wananchi weznio, maandamano atayrishe Chadema. This mindset up is wrong. Sisi kama wananchi ni lazima tuonyeshe waya forward. Kitu kama hichi kikiandaliwa rasmi unageuk kuwa uasi na uhaini. Lakini wanachi wakifanya uprising wenyewe ni sawa kabisa. Acha kusubiri kufanyiwa kila kitu!!1
 
Kama serikali ni legelege pia bunge lenye 75% ya wabunge wa chama tawala nalo ni legelege, mbunge anasema jwtz wachukue vituo vya mafuta wawahudumie wananchi kweli ndio utatuzi wa tatizo?
 
Wauza mafuta (ambao hadi sasa wameonyesha wana nguvu zaidi ya serikali ya CCM) wa huku Tanga wameanza mgomo wao rasmi jana. Hadi jana jioni kulikuwa na vituo viwili tu vya mafuta hapa Tanga mjini. For curiosity, mikoa mingine vipi?

Najiuliza tunataka nini zaidi ili tuingie Tahrir Square?
 
Pigeni kelele tu. JK yuko na rais wa Somalia wanakula bata. Akitoka hapo anaishia zake Washington kula kuku. kelele zenu hazimnyimi usingizi. Poor TZ. Ngoja tuone kama Igunga hamtawapa tena hao hao wala nchi!!!!!!
 
Serikali inajitahidi iwezavyo kuleta maisha bora kwa wananchi wake. Tatizo ni dogo sana yaani watendaji wake kwahiyo susiilaumu sana, ila tuwalaumu watendaji wake.

Wakati mwingine tunapata shida kutoa tafsiri ya sahihi ya serikali ni nini?
 
Mnajua nini?
Mimi ninaside na hawa wafanyabiashara

In short Tanzania ni nchi ambayo ngumu sana kufanya biashara na sishangai sana kuhusu hizi charges na rushwa iliyokithiri

serikali inasema meli zinakaa siku 5 kule baharini...ukweli ni kuwa meli zinakaa mpaka siku 50 kule nje baharini kwenye foleni sasa hilo huhitaji kujua kuwa kuna incompetency sehemu na sishangai kuskia TRA na EWURA wana husika

Sasa huyu kaleta hoja na vielelezo na kasema kama kuna mtu anahitaji zaidi amtumie e-mail.

sisi tumezidi:

rushwa

urasimu

mazingira magumu kufanya biashara

Kodi zisizoeleweka kila kona badala ya kodi moja na ambayo inaeleza inafanya nini

local authorities kujaa staff ambao pia ni wala rushwa na wahuni



sasa tusitake kukaa hapa na na kutaka kuitakasa sana serikali na departments zake ili hali ukweli tunaujua lakini hatutaki kuuweka wazi. Naungana na wenye vituo hivi na nashauri its about time they come back and fight hizi slander wanaztumiwa kwa kuweka wazi jinsi wanavyonyonywa watu kama TRA,TBS,EWURA, LOCAL AUTHORITIES na kadhalika.

sitaki kuanzisha thread nyingine kwani siku hizi naona kabla hujaanzisha thread inabidi ipitie kwa GESTAPO wa JF kabla hajatundikwa so tutaendelea humu humu kuelezana

Lakini baada ya catalogs za uwongo toka serikalini mimi nikiambiwa nani nimwamini between serikali na wafanyabiashara hawa then nadhani mnajua nitakuwa upande upi
 
Ndugu wananchi, tatizo hili ni kubwa kuliko tunavyofikiri. Nawapa pole sana, Mungu yupo na kwa uweza wake atatuepushia maafa yanayochochewa kwa kasi na kadhia hii. Nawaomba sana wote tushikamane na tuwe kitu kimoja katika kukabiliana na hali hii. IGP Mwema aliwahi kusema huko nyuma kuwa mafisadi papa tukiwachokonoa cha moto nchi hii itakiona. Je, kuanguka kwa RA ni mwanzo tu wa kile alichokiona IGP wetu? Tushikamane pamoja, tukitengana hatutaweza.
 
Katika post zooooote zaidi ya 100 sijaona SULUHISHO zaidi ya malalamiko tuuuuu. Mtaendelea kulalamika hadi lini na mnamlalamikia nani?????????Humu jamvini kuna watu ni mahiri sana wa kuandika huku wamejificha maofisini wakila kiyoyozi.

Natoa suluhisho sasa nini tunatakiwa kufanya:
Wauza mafuta wakiendelea kugoma, basi kesho asubuhi na mapema tukutane pale ubungo mataa. Naamini hapo ni makutano ya maeneo mengi ya jiji. Hakuna haja ya mkakati mwingine, cha kufanya kitapatikana kesho hiyohiyo saa 12 asubuhi...Yapo mengi tu ya kufanya...!
Tuache maneno sasa tufanye vitendo kama wao wanavyotutenda.
Vinginevyo hatuna haja ya kulalamika tena, na tufunge madomo yetu milele.
 
Ninatokea kibamba kuelekea town. Vituo vyooote havijafunguliwa.

Hivi ule mkwara wa ngeleja ulikuwa geresha tuuuuuu? Aaaaagh!

Jamani mbona mnatusumbua sana. Serikali inamiliki 50% shares katika BP, hivyo mashangingi ya Serikali yanabeba mafuta kutoka Kurasini na kuyauza mitaani. Wenye taabu na mahangaiko ni nyinyi walala hoi tu
 
Ngeleja kwa nini haachii ngazi, hivi haoni kwamba watanganyika wanataabika kwa sababu yake, hivi ni lazima awe waziri? kwa nini hachukui maamuzi magumu, halafu tamko la Bunge ni lipi kuwapa 24hrs wasipo tii what next?, kweli serikali imewekwa mfukoni.

Mh Mnyika jana katamka anao ushahidi kwamba maofisa wa serikali wamehongwa na ndio chanzo cha tatizo na kiburi cha hawa wafanya biashara ya mafuta, Dr Hosea upo wapi?

Hivi ni nini kazi ya usalama wa taifa, kulinda maslahi ya nani? kwa nini wapo kimya mpaka sasa, kwa nini hawa wafanyabiashara bado wana lala nyumbani kwao badala ya keko au ukonga, jamani huu ni uhujumu uchumi wa taifa letu, Pinda uko wapi kwa nini usiige maamuzi kama ya Hayati Sokoine?, na sisi wananchi tupo wapi? tunafanya nini? mimi nafikiri hata kujadili hapa pia haisaidii inazidi kutuumiza vichwa vyetu.

Kwa hali ilivyo na kwa jambo hili na amini Wananchi wataingia mtaani nawaomba Polisi kwa jambo hili toeni ushirikiano na nyie mnaguswa na jambo hili, wewe polisi shika silaha yako lakini usipige raia yani mwajiri wako mwache aandamane kwa amani na apeleke ujumbe magogoni.
 
Ndugu wananchi, tatizo hili ni kubwa kuliko tunavyofikiri. Nawapa pole sana, Mungu yupo na kwa uweza wake atatuepushia maafa yanayochochewa kwa kasi na kadhia hii. Nawaomba sana wote tushikamane na tuwe kitu kimoja katika kukabiliana na hali hii. IGP Mwema aliwahi kusema huko nyuma kuwa mafisadi papa tukiwachokonoa cha moto nchi hii itakiona. Je, kuanguka kwa RA ni mwanzo tu wa kile alichokiona IGP wetu? Tushikamane pamoja, tukitengana hatutaweza.

Katika post zooooote zaidi ya 100 sijaona SULUHISHO zaidi ya malalamiko tuuuuu. Mtaendelea kulalamika hadi lini na mnamlalamikia nani?????????Humu jamvini kuna watu ni mahiri sana wa kuandika huku wamejificha maofisini wakila kiyoyozi.

Natoa suluhisho sasa nini tunatakiwa kufanya:
Wauza mafuta wakiendelea kugoma, basi kesho asubuhi na mapema tukutane pale ubungo mataa. Naamini hapo ni makutano ya maeneo mengi ya jiji. Hakuna haja ya mkakati mwingine, cha kufanya kitapatikana kesho hiyohiyo saa 12 asubuhi...Yapo mengi tu ya kufanya...!
Tuache maneno sasa tufanye vitendo kama wao wanavyotutenda.
Vinginevyo hatuna haja ya kulalamika tena, na tufunge madomo yetu milele.

Jamani mbona mnatusumbua sana. Serikali inamiliki 50% shares katika BP, hivyo mashangingi ya Serikali yanabeba mafuta kutoka Kurasini na kuyauza mitaani. Wenye taabu na mahangaiko ni nyinyi walala hoi tu


swali

btn serikali na wafanyabiashara mnaamini maneno ya nani?
 
Wakuuu tupeni updates ina maana bado wamrtunisha misuli, hapa bongo nasikia Bamaga na Big born sinza wanauza ila foleni sana taarifa tafadhali maana tunakaribia kupaki!
 
Naomba ukumbuke watendaji ndio serikali yenyewe kwani unataka kusema waziri au rais sio mtendaji. Nasema the all Government is corrupted and they are not performing at all
Serikali inajitahidi iwezavyo kuleta maisha bora kwa wananchi wake. Tatizo ni dogo sana yaani watendaji wake kwahiyo susiilaumu sana, ila tuwalaumu watendaji wake.
 
Tangu kuanza kwa hili sakata la mafuta nimefuatilia kwa ukaribu sana watu wanasema nini. Wengine wamethubutu kusema jeshi liingilie kati, wengine wakasema wachome vituo vya mafuta na maneno mengi sana. Lakini Watanzania ni lazima tufikiri kwa upana zaidi na tusiwaone kwamba wauza mafuta ni wabaya. Tujiulize ni kwa nini wakatae kupunguza bei ya mafuta hata baada ya vitisho vikali toka bungeni na mamlaka husika?

Kabla ya serikali kupunguza bei hadi Tsh 2004, bei ilikuwa imefikia Tsh 2200. Serikali ikasema inapunguza tozo zake ili yaweze kushukA BEI. Je ni kweli kwamba tozo ambazo serikali imepunguza zinafika Shs 196 ambazo serikali imepunguza? Je serikali ni kweli imepunguza kiasi hicho kwenye tozo zake? Serikali iwathibitishie Watanzania kwamba kiasi ambacho imepunguza kwenye tozo zake ni kipi ili tuweze kujua nani mbaya kati yake na wauza mafuta. Sio tu inawalazimisha kupunguza bei, hayo mafuta hawajayapata bure. Gharama zingine inaongeza serikali yenyewe. Kwa wastani meli huchukua wiki 3 hadi 5 kabla ya kupakua mzigo. Wamiliki wa meli hutozwa pesa kwa muda huo wote wanapokuwa wako baharini wakisubiri kuja kushusha mzigo na gharama hizi zote hujumlishwa kwenye bei ya mafuta. Baada ya hapo kuna inport duty, Ewura charges, TBS charges za kupima quality ya mafuta, TRA charge za kupima kiasi cha mafuta, na gharama nyingine lukuki. Kwa hiyo serikali itulie kwa umakini badala ya kukurupuka tu. Hawa Ewura (Haruna Masebu) wanaidanganya serikali halafu inachukua maamuzi ambayo yanaumiza wananchi na wafanyabiashara.

Kama serikali inataka kutatua tatizo hili kwa uwazi iwaeleze Watanzania gharama zote ambazo anatozwa mfanyabiashara anayeingiza mafuta nchini, nadhani tutawahurumia hawa watu, tozo ni nyingi mno. Hapo ndipo watu tutajua nani mbaya kati ya serikali na wafanya biashara.

Kumbuka kwamba hizo gharama zote tunabeba sisi wananchi. Yaani
1. Gharama ya kusafirisha toka huko Arabuni
2. Parking ya meli ikisubiri kupakua mzigo(demurage charges)
3. Quality inspection (TBS)
4. Quantity checking-TRA
5. Quantity checking-SGS
6. EWURA
7. Inport duty
8. Faida ya mfanyabiashara n.k
 
Back
Top Bottom