analysti
JF-Expert Member
- Aug 24, 2009
- 729
- 612
Bila kejeli,hivi tunalalamika kuanzishwa kwa COPEC?
AS in,we don't want COPEC or it's been long overdue?
What is the message here?? Sijakuelewa mkubwa!!
Bila kejeli,hivi tunalalamika kuanzishwa kwa COPEC?
AS in,we don't want COPEC or it's been long overdue?
Kazi kwelikweli jamani sijui mwisho wake itakuwaje
Naamini pamoja na kauli hii umegundua kuwa HALI SI NZURI na hata kuwashawishi watu wakuelewe ni ngumu sana.
Hapa ndo inapokuwa ngumu mtu kuitetea serikali, yawezekana wana vitu vya kuufanya umma uiamini lakini wamevikalia wao, wanabaki kudai 'kazi ya wananchi ni kulalamika tu' sijui wakitarajia tukavunje makabati yao kujua nini kipo kwenye files?
Pole mkuu, inachosha kuwatetea hawa jamaa.
Post imechakachuliwa,nilitaka kuuliza hili swali kwenye thread ya Ngeleja bungeni.So sorry.What is the message here?? Sijakuelewa mkubwa!!
Serikali ya ccm haiwezi kuwagusa wafadhiri wa chama chao lasivyo makubwa zaidi yatafumuka na watakuwa uchi wa mnyama. Kama wangekuwa watu wakawaida, mbona tamko la EWURA lilikuwa linatosha? kULIKUWA NA HAJA GANI WAZIRI KUTOA TAMKO LA PILI WAKATI TAASISI ILIYO CHINI YAKE ILISHATOA TAMKO KAMA HILO NA HALIKUTEKELEZWA?
Nadhani pia kwa mjibu wa ngereja, solution yao ni kuwapa lesseni sijui COPEC wafanye biashara hiyo wakati walikuwa wamekalia maamuzi haya kwa miaka minne sasa. Hii inaonyesha wafanyabiashara hawa wana nguvu na ndiyo wenye maamuzi ya nani apewe leseni ya biashara ya mafuta. Kama ndivyo inategemea COPeC watapata wapi hela ya harakaharaka ya kuleta mafuta wakati watoaji wa hiyo hela ni viongozi walewale ambao ndiyo wenye makampuni yaliyogoma?
Hapa kuna sinema fulani tusubiri kwa kuwa sisi ni wapole na wanyenyekevu wa moyo mapaka itakapoisha.
Inawezekana kabisa<br />
<br />
nina wasiwasi viongozi wetu wanatoa mikwara halafu wanaenda kuomba msamaha.
Eee Mungu Baba, sikia kilio changu, hali hii ieendelee hivi hata miezi sita, watanzania wengi wamekuwa wagumu kutambua kuwa CCM imeshindwa, wanahitaji kujinza kwa vitendo zaidi hivyo hali hii itasaidia watanzania kutambua ukweli.
Natamani kuchangia lakini najizuia nisije nikaongea bila busara.kwakuwa siwezi kusema yaliyoko moyoni naomba mgomo wa wauza mafuta uendelee mpaka kieleweke.Labda kwa njia hii watanzania watapata akili za ziada na kufanya maamuzi magumu.
Ninatokea kibamba kuelekea town. Vituo vyooote havijafunguliwa.
Hivi ule mkwara wa ngeleja ulikuwa geresha tuuuuuu? Aaaaagh!
Hv chadema wapo wapi muda kama huu?me sielewi kwann hawajaanda maandamano mpk saiv,zaidi ya siku 7??au wao maandamano wanaandaa kma wakiwa wanataka madaraka tu? Suala la jailo wapo kimya suala la mafuta wapo kimya,jaman mananiangusha chadema,andaeni maandamano jmn tuwashinikize hawa wahuni watoke madarakani,imefika muda tuwe kama watu wa london kwa kuchoma hivi vituo vya mafuta na mali za mafisdi pai
Ahaa kumbe mafanikio ya CCM! Nilidhani mafanikio ya watanzania chini ya CCMTusiyabeze mafanikio ya CCM jamani!
Nashukuru kwa comment hii - Maana tangia saa 11 alfajiri nipo hapa Africana kwenye "foleni ya mafuta"!
Tumedhubutu - Tumeweza - Tunasonga Mbele!
Mi nadhani ushauri wa zitto uzingatiwe jeshi litumike vituo na maghala yafunguliwe na mafuta yatolewe bure. La sivyo wananchi tuandamane tuvamie vituo hivyo na kujichotea mafuta kwa nguvu.