babukijana
JF-Expert Member
- Jul 21, 2009
- 13,113
- 16,021
mkuu acha kuhatarisha usalama wako huko rudi nyumbani hao wenzetu washapagawa,acha walipuane tulipokua tunauliza hapa kwanini wananunua masilaha kibao kina smatta walikuja juu kwamba lazima waweke ulinzi ili nchi kama sisi tukiwachokoza watuchape sasa naona wanaanza kulipuana wenyewe kwa wenyewe,smatta na mwenzio nyalego kikiwaka karibuni bongo mtalala kwenye korridor na vibaraza vipo kwaajili yenu.Jamani hapa Nairobi hakutoshi tena manake ni hivi punde kuna bomu moja limegunduliwa Mombasa road si mbali sana kutoka njia panda ya Nyayo stadium kabla ya kulipuka. Ni mbele tu ya Garage ya Sea motors na limepatikana chini ya daraja. So kwa sasa barabara hii kuu imefungwa na wanausalama wanaendelea na uchunguzi. Mwenzenu huku ndani hakukaliki natamani nimalize chuo nirudi nyumbani bongo. Lile la jumapili lilinikosakosa ingawa sikuwa kwenye mkutano huo wa kisiasa na hili la leo nilipita hapo darajani kama saa nne hivi. Najiuliza ni ahadi za Al Shabab zinatimia au ni haya mambo ya YES and No? Kazi tunayo!