KERO Karatu umeme unakatika zaidi ya mara tano (5) kwa siku

Hii ni kero ambayo mwananchi ameiwasilisha JF akitaka wahusika kuchukua hatua
A

Anonymous

Guest
Umeme katika line ya KARATU maeneo ya
NMC, Mangafi, Gibbs, Endoro, Marera, Ayalabe, Rhotia, kilima tembo, Mbulumbulu, Manyara kinaoni, Chemchem, Mto wa Mbu, Selela, unakatika sana, yani mara kwa mara kiasi cha wananchi kuwa na hofu ya kuunguliwa na vifaa vyetu vinavyotumia umeme.

Manager wa TANESCO Mkoa wa Arusha na Meneja wa TANESCO wilaya Karatu mnalijua hili? Hii ni tofauti kabisa na Karatu mjini ambako umeme haukatiki hovyo hata kipindi cha mgao hii ni kero kubwa kiasi kwamba wananchi wanalia kubadilishiwa line , hii line imekua sio ya kutabirika maana hakuna siku umeme utatulia siku nzima bila kukatikakatika .

Tunaomba kero hii iwafikie wahusika na hatua zichukuliwe haraka kuepusha madhara
 
Kama Karatu iko Tanzania Hilo halina Tatizo kabisa..
Ila kama Iko nchi ya Kenya Ni tatzo kubwa sana kwa usalama wa Nchi na wananchi
 
Back
Top Bottom