Kanuni ya Umoja katika kuwezesha kutatua changamoto kubwa za maisha zinapokujia

Heaven Seeker

JF-Expert Member
May 12, 2017
478
1,047
Rejea mada tajwa hapo juu kwenye heading na ninaomba niende moja kwa moja kwenye mada husika.

UTANGULIZI

Kwanza kabisa unaweza kukubaliana nami kuwa changamoto kubwa zaidi za watu wa maisha ya kati ni kuhudumia matibabu, kupoteza ajira, kuunguliwa na nyumba, misiba na kupatwa na kadhia ya kesi mahakamani inayoweza kupelekea mhusika kufungwa.

Kuna njia kadhaa katika jamii yetu zimewekwa kutatua changamoto hizi ikiwemo mtu binafsi kufanya savings, kuwa na BIMA ya maisha, Afya, nyumba n.k.

Pamoja na kuwepo kwa njia hizo bado changamoto ni kubwa katika jamii yetu kutokana na sababu nyingi ikiwemo, pamoja na mambo mengine, kutokuwa na uwezo wa kufanya savings za kutosha kutatua changamoto husika, mlolongo mrefu na usumbufu mwingi wa kupatiwa stahiki zako katika shirika husika la BIMA, kutokuwa na uwezo wa kuwa na BIMA ama BIMA kubagua baadhi ya changamoto.

UMOJA NI NGUVU

Wahenga walisema Umoja ni nguvu na utengano ni udhaifu. Wakaendelea kusema Haba na Haba hujaza Kibaba. Wakasema pia kuwa kidole kimoja hakivunji chawa na wakaenda mbali wakasema penye wengi hapaharibiki jambo.

Ndio maana hata nchi na wadau mbalimbali wanajitahidi kutengeneza Umoja kama vile NATO, AU, ECOWAS, EU, G20, G9, WTO n.k. ili kutatua changamoto mbalimbali zinazowakabili kwa pamoja ambazo pengine isingekuwa rahisi kuzitatua individually.

Hivyo suala la kuwa na umoja ni jambo muhimu sana. Kwa kukazia zaidi, ndio maana utaona watu wa mashirika ya BIMA wanapambana kukusanya senti zetu ndongondogo ili kutatua matatizo ya mtu mmoja mmoja na ukweli ni kuwa bado wanabakiwa na faida ukichukua mapato wanayokusanya ukatoa gharama za kulipia hizo BIMA.

WATU GANI WAMELENGWA KATIKA JAMBO HILI ?

Si suala la ubaguzi ila nimejaribu kuzingatia mambo kadha wa kadha, ila kama kutakuwa na wadau wanaoweza kuboresha zaidi wazo hili itakuwa jambo jema. Kimsingi wazo hili linawahusu watu wenye ajira katika sekta rasmi na wawe na BIMA za AFYA.

Wanakuwa watu 100 watakaokuwa wanachangai Tsh. 50K kila mwezi. Maana yake kwa mwezi inakuwa ni Tsh 5M na kwa mwaka ni 60M. Mfumo huu unamtaka mwanzilishi mmoja wa kuanzisha wazo hili kisha anawahusisha rafiki zake wa karibu sana wenye sifa nilizosema hapo juu angalau wawe watano.

Kisha na hao watano watatafuta rafiki zao wa karibu wengine zaidi. Wataendelea kutafutana mpaka wafikie watu 100. Nina sisitiza, ni kwa ajili ya marafiki wa karibu tu na si muhimu wawe ndugu. Kwenye masuala ya ndugu ni migogoro chungu mzima na masimango mengi. Marafiki wa karibu wanafaa zaidi katika Umoja huu.

CHANGAMOTO HUSIKA ZINATATULIWAJE?

1. UGONJWA
: Kwakuwa kila mtu anakuwa na BIMA ya afya, basi msaada utahusu pale mtu anapopatwa na changamoto za matibabu ambayo hayapo kwenye hizi BIMA za kawaida. Michango italipia nusu ya gharama zote pale mtu anapopatwa na changamoto za kiafya.

Kikomo cha kumsaidia mtu itategemea na makubaliano ila lengo hasa ni kumsaidia mtu pale anapokuwa hawezi kuhudumiwa na BIMA ya AFYA ya kawaida. Michango itamhusu mhusika mwenyewe, mwenza wake ama watoto.

Vilevile, umoja huu utamchangai mhusika kiasi cha Tsh 1M pale mhusika, mtoto ama mwenza wake anapokuwa amepatwa ugonjwa unaoweza kupelekea kulazwa hospitali ila unatibika kwa BIMA ya afya, hii itakuwa kama sehemu ya kuchangia gharama nyinginezo.

2. MSIBA: Ikitokea mwanachama amefariki basi umoja huu utachangia angalau 5M kwa mwenza wake ama mzazi. Na ikitokea mwenza, mzazi ama mtoto wa mwanachama amefariki basi umoja huu utatoa mchango usiopungua 1M kwa mhusika.

3. KUUNGULIWA NYUMBA: Ikitokea mwanachama ameunguliwa nyumba basi umoja huu utalipia gharama za makazi ya muda (nyumba ya kupanga) yenye kiwango sawa na nyumba aliyokuwa anaishi member husika kwa kipindi kisichopungua miezi 6 mfululizo.

4. KESI MAHAKAMANI: Bila kujali aina ya kesi. Ikitokea mhusika amepatwa na changamoto inayopelekea mwanachama kufikishwa mahakamani basi umoja huu utamchangia nusu ya gharama atakazotumia kwa ajili ya Wakili wake.

Hapa vigezo na masharti vinaweza kuzingatiwa kulingana na makubaliano ya wanachama. Ila lengo haswa limejikita kwenye zile kesi za mfano kusingiziwa ama ambazo mwanachama hakuhusika moja kwa moja na kuna dalili za uonevu. Siyo kwa ajili ya uzembe wa makusudi.

5. KUPOTEZA AJIRA: Ikitokea member wa Umoja huu amepoteza ajira basi umoja huu utalipia nusu ya mshahara wake aliokuwa akiupata kwa kipindi kisichopungua miezi 6 tangu kupoteza ajira.

Wakuu, hili ndio wazo langu na karibuni kwa mawazo tofauti ya kupinga kwa kuonesha udhaifu wa wazo hili ama kuunga mokono kwa kufanya maboresho zaidi.

Hoja hujibiwa kwa hoja na siyo kwa kupigwa mawe. Lengo mahsusi la kuelimika ni kuwa na uwezo wa kutengeneza mawazo ya kutatua changamoto za maisha na ikiwezekana basi mwanadamu aishi kwa raha na furaha hapa Duniani.
 
Uonavyo mkuu hili suala haliwezekani kabisa. Bali ni ndoto tu za mchana au siyo?
ntakupa mfano mdogo tu

nafkr magrp ya whasapp unayajua


hayatofautiani na ulichosema.


umoja utaanza wenye nguvu

anaefaidika na kula hasara zaidi ni yule wa kwanza kuchangiwa


huyu atapata hela nyingi kwa watu wachache coz grp ndo limeanza na lina nguv


lkn vilevile huyuhuyu atapata hasara mara mbili ya faida aliyoipata wakat akichangiwa

ni pale tu atakapoanza kuchangia wengine kivipi

hapa atajikuta anachangia ata ambao hawakumchangia
atajikuta idadi inaongezeka ya member wapya halafu wana matukio kibao hana budi kuwachangia bado wale wenye matukio ya kujirudiarudia.



huo ni mfano tu
 
ntakupa mfano mdogo tu

nafkr magrp ya whasapp unayajua


hayatofautiani na ulichosema.


umoja utaanza wenye nguvu

anaefaidika na kula hasara zaidi ni yule wa kwanza kuchangiwa


huyu atapata hela nyingi kwa watu wachache coz grp ndo limeanza na lina nguv


lkn vilevile huyuhuyu atapata hasara mara mbili ya faida aliyoipata wakat akichangiwa

ni pale tu atakapoanza kuchangia wengine kivipi

hapa atajikuta anachangia ata ambao hawakumchangia
atajikuta idadi inaongezeka ya member wapya halafu wana matukio kibao hana budi kuwachangia bado wale wenye matukio ya kujirudiarudia.



huo ni mfano tu
Mkuu nimekusoma. Lakini hii issue siyo kuchangiana bali ni michango ambayo kila mtu anatoa kila mwezi. Na maximum naumber ya members inabidi kubakia 100 ili kupnguza matukio mengi sana.

Huu mfumo ni sawa na ule wa BIMA kwamba kila mwezi unachangia na hiyo BIMA itakusaidia endapo tu utapatwa na matatizo.

Utofauti wake na formal BIMA ni kuwa, huu mfumo unarahisisha zaidi member kupata pesa bila mlolongo maana wahusika wataweka utaratibu rahisi na wa uwazi zaidi.

Kingine ni kuwa hili ni kundi la watu marafiki zaidi na siyo kila mtu. Na wawe na ajira katika mfumo rasmi. Umepata kidogo point mkuu?
 
Back
Top Bottom