Changamoto ni sehemu ya maisha!

BOB LUSE

JF-Expert Member
Jan 25, 2014
3,584
2,898
Usitafute maisha yasiyo na changamoto, utafeli asubuhi, ukifanikiwa katika maisha utakuna na changamoto zake, ukifeli pia utakuna na changamoto.

Ukiwa na Elimu kubwa, ukikosa Elimu, ukiwa juu, ukiwa chini, ukisali na kuabudu, pia usiposali na kuabudu, changamoto zipo.

Changamoto zinaleta radha ya Maisha, kwakuwa changamoto ya Leo sio ya kesho, ushindi wa Leo ni tofauti na wa kesho! Usimlaumu mtu Kwa yanayokufika, usipokumbana na hayo, utakumbana na mengine.

Maisha ni kujifunza na kushindana Ili ushindei,Kila mtu ana kikombe chake anachokinywea! Usitamani dozi ya mwenzio.
 
Ili tuwe na chakufanya ndio maana binadamu alibuni karatasi akaita pesa , ikaingia kwenye mzunguko ikawa ni changamoto kuipata ili tupate thaman ya maisha .

Thamani ya maisha haiwezi kuwepo bila changamoto.
 
Back
Top Bottom