Kanisa lakataa msaada wa mbunge aliyelikashifu

The Khoisan

JF-Expert Member
Jun 5, 2007
15,396
12,979
Kanisa Katoliki lakataa msaada wa mbunge

Thursday, 03 March 2011
Mussa Mwangoka, Sumbawanga

KANISA Katoliki katika Jimbo la Mpanda mkoani Katavi, limeagiza kurudishwa kwa msaada uliotolewa na Mbunge wa Mpanda Vijijini (CCM), Moshi Kakoso kwa ajili ya kusaidia vigango vya Parokia ya Karema.

Agizo hilo linatokana na kile kilichoelezwa kuwa ni kanisa kukerwa na hatua ya uongozi wa CCM wilayani Mpanda, kulikashifu.

Habari zilisema agizo hilo lilitolewa juzi na Makamu Askofu wa Jimbo hilo, Padri Patrick Kasomo, ambaye pia ni Paroko wa Karema, kufuatia maneno ya kejeli na kashfa yanayodaiwa kuwa yalitolewa na Katibu wa CCM wa Wilaya ya Mpanda.

Padri Kasomo alidai kuwa Katibu huyo wa CCM alitoa kashfa hizo alipokuwa akihutubia mkutano wa hadhara, ulioitishwa na mbunge huyo kwa lengo la kuwashukuru wananchi kwa kumchagua.

Hata hivyo alipoulizwa kuhusu madai hayo, Katibu huyo Jacob Nkomola, alisema hakusema maneno hayo dhidi ya kiongozi huyo wa kanisa na kwamba kilichopo ni mgogoro baina ya wananchi na kanisa baada ya Padri Kasomo kupora sehemu kubwa ya ardhi ya kijiji, yakiwemo maeneo ya wazi.

Alidai kuwa maeneo hayo ni pamoja la uwanja wa kuchezea mpira, ambao alipitisha trekta na kuubadilisha kwa ajili ya shughuli za kilimo.

"Nilichozungumza kwenye mkutano wa hadhara ni kwamba kiongozi wa dini anayevaa msalaba na kanzu anatakiwa kuwa mkweli, sasa huyu padri anaingiza ushabiki wa kisiasa, yeye tangu wakati wa uchaguzi alikuwa akipigia kampeni Chadema na anafanya hivi huku akipora maeneo ya wazi ili kumkwamisha diwani wa CCM aliyeshinda katika Kata ya Karema," alidai katibu huyo katika mazungumzo ya njia ya simu.

Msaada uliokataliwa ni wa Sh300,000 zilizotolewa kwa nyakati tofauti katika vigango vya Kaparamsenga, Ikola, na Karema.

Kila kigango kilipewa kilipata Sh 100,000 ikiwa ni msaada kutoka kwa mwanasiasa huyo.

Padri Kasomo alidai kuwa katika mkutano huo, Katibu wa CCM wa Wilaya ya Mpanda, alimkashifu yeye na imani ya kanisa.

Alisema kuwa mtendaji huyo wa CCM aliwasalimia wananchi kwa salamu inayotumiwa na Kanisa hilo Katoliki inayosema ‘Kristu' na kujibiwa tumaini letu lakini mtendaji huyo alisema tumaini liwe kwenu tu si kwa padri wenu Kasomo,fisadi ambaye hastahili kuwa kiongozi wa kiroho .

Padri huyo alidai kuwa kejeli na kashfa hizo zilizotolewa mbele ya waumini wake.

Alidai katibu huyo aliwataka waumini wa kanisa kuandamana kwenda parokiani kumvua kanzu ya upadri

Mkuu wa Wilaya ya Mpanda Dk Rajab Rutengwe alipohojiwa kwa njia ya simu alikiri kupokea malalamiko hayo kutoka kwa Makamu wa Askofu Kasomo.

Source: Mwananchi
 
Huyo Mbunge naye anachemka. Yaani TShs. 100,000 anaita msaada; hiyo angempa mwanae akaweke kwenye sanduku la sadaka kwani ni mchango mdogo sana siyo lazima ijulikane nani katoa.
 
Hiyo misaada apeleke Gongolamboto kamwe haiwezi kulinunua kanisa.
Huyo mbunge angekuwa Muislam basi wajinga wangeanza kudai udini huu ila wakristo kwa wakristo washikishane adabu kama vipi mtimue huyo mbunge awe anasali akiwa Dodoma na si huko Rukwa

KANISA HALINUNULIKI KWA PESA yeyote ile
 
mh twendeni mbele na kurudi nyuma hv kupora eneo la wazi nayo imekaaje kwa matumizi binafsi.si ndo mambo yanayopigiwa kelele kila siku kudhulumu wananchi?
 
Hiyo misaada apeleke Gongolamboto kamwe haiwezi kulinunua kanisa.
Huyo mbunge angekuwa Muislam basi wajinga wangeanza kudai udini huu ila wakristo kwa wakristo washikishane adabu kama vipi mtimue huyo mbunge awe anasali akiwa Dodoma na si huko Rukwa

KANISA HALINUNULIKI KWA PESA yeyote ile

Sasa apo Uislamu unaingiaje?? Nilitegemea ungejibu madai ya ufisadi wa uyo Padre anayepora ardhi ya wanakijiji unakimbia mada. Wakatoliki alwyz wabinafsi sana na wanatamaa utafikiri wataenda na mali makaburini wakifa. Aache upuuzi wake arudishe ardhi ya wanakijiji asilete mambo ya kizamani uyo mvaa kofia ndefu km kishada. Fisadi yeyote lzm alaaniwe awe Padre au yeyote. Usitetee upupu soma vzr madai juu na usiende nje ya mada. Hahahhaha eti Padre mporaji kwa wanakijij maskin duh hii kali. Tutaskia mengi na hizi siasa+dini. Wakatolik wanazid kujianika ktk kujihusisha kwao na siasa kwa chama cha........simoooo
 
I'm sure huchakutana na Wakatoliki wote kukuonesha hiyo tamaa. Unaposema 'Wakatoliki always' unamaanisha 'all Catholics always' na hii sweeping statement ni fallacy.
 
Habari kutoka mkoa mpya wa KATAVI ni kwamba Askofu wa jimbo la Mpanda ameagiza kurudishwa kwa msaada uliotolewa na mbunge wa jimbo la mpanda vijijini kupitia CCM kwavile mbunge huyo alikuwa amelikashifu kanisa katoliki katika mikutano yake ya hadhara wakati alipokuwa akishukuru wananchi wa jimbo kwa kumchagua kuwa mwakilishi wao! habri hii pia inapatikana katika gazeti la mwananchi la leo(ijumaa 4-02-2011)
 
Alitaka kujitafutia umaarufu kuwa katoa msaada kanisani wakati hiyo hela ni sawa na sadaka ya misa ya jioni ya jumanne tena ya watoto!
 
Alitaka kujitafutia umaarufu kuwa katoa msaada kanisani wakati hiyo hela ni sawa na sadaka ya misa ya jioni ya jumanne tena ya watoto!

Kwani sadaka ina kima? Au ndio mambo ya kanisa, mstari wa mbele kwa wenye nacho?
 
Habari kutoka mkoa mpya wa KATAVI ni kwamba Askofu wa jimbo la Mpanda ameagiza kurudishwa kwa msaada uliotolewa na mbunge wa jimbo la mpanda vijijini kupitia CCM kwavile mbunge huyo alikuwa amelikashifu kanisa katoliki katika mikutano yake ya hadhara wakati alipokuwa akishukuru wananchi wa jimbo kwa kumchagua kuwa mwakilishi wao! habri hii pia inapatikana katika gazeti la mwananchi la leo(ijumaa 4-02-2011)

saaaaaaaaafi sana, CCM wakamape RA akatumie na AL Adawi na mafisadi wengine........ :)
CCM ni mkusanyiko wa waovu, wachochezi na waliofilisika...ukiwapokea nawe unakuwa kama wao....
 
Back
Top Bottom