Kanisa laahirisha ndoa baada ya watarajiwa kukiri kuzini

''Asiye na dhambi awe wa kwanza kuokota mawe na kuwapiga hawa watuhumiwa''.........mwisho wa kunukuu sasa endelea na story

Bibi na Bwana harusi watarajiwa wamejikuta wakishindwa kufunga pingu za maisha baada ya Kanisa kukataa kuwafungisha ndoa kutokana na kile kinachodaiwa walishiriki tendo kabla ya kufunga ndoa kitu ambacho ni kinyume na taratibu za dini.


Watarajiwa hao kutoka Kaunti ya Tana River nchini Kenya walikiri kuwa walikuwa wakifanya mapenzi kabla ya ndoa sababu ambayo ililifanya kanisa kuwafukuza na kutaka wakatubu.

Inaelezwa kwamba wakati wa kikao cha ushauri na maungamo kwa wanandoa hao watarajiwa, bwana harusi alikiri lakini bibi harusi mtarajiwa alikana kuwahi kushiriki tendo hali ambayo ilimfanya Mchungaji kuwaita ofisini na baadae kukiri.

Hatua hiyo ilimfanya Mchungaji Eli Mwakisha, kukasirika na kutishia kuwalaani wawili hao. Mwakisha aliwafukuza ofisini kwake na kuita timu ya maombezi kwa ajili ya sakata hilo.

Baada ya saa mbili za maombi mazito, aliwaita tena ofisini na kuwaambia watengane na kusimamisha mipango ya harusi kwa muda wa miezi 12 huku akisema hayo yalikuwa ni maagizo ya Mungu.



Kiongozi wa maombi katika kanisa hilo Helida Kase, amesema wawili hao waliagizwa kutumia muda huo kutubu na kuomba, lakini pia wahakikishe wanahudhuria ushauri wa wanandoa kila Jumatano, Ijumaa na Jumapili.

Wanandoa hao watarajiwa walikataa kuzungumzia suala hilo huku baadhi ya waumini wa kanisa wakiona kuwa hio haitakuwa harusi ya kwanza kusimamishwa au kufutwa, kama ilivyo kawaida wakati watarajiwa walio katika uchumba wakigundulika wamefanya mapenzi kabla ya ndoa.
Source Mwananchi
Mchungaji anataka waendelee kuzini??
Huyo mch may be ni kibubu chake!; wivu ndio uliosukuma maamuzi yake!
 
Hhaaahahaaa labda sio mimi. Wakihairisha naenda kutafuta kanisa jingine nafunga.na nahamia huko hata kanisa la maombezi.kwani sh ngapi?

Hakuna dhambi kubwa wala ndogo,dhambi ni dhambi tu.alietukana na aliezini wote ni sawa tu!

Neema ya bwana Yesu kristo aliyonipa nkipiga goti dakika moja kwa kumaanisha nkatubu nkimaanisha mi na mchumba yameisha tunaingia ndani ya ndoa tukiwa safi.

Sasaa miezi 12 hadi vikao vya sherehe visimamishwe..

Wakenya bakini na makanisa yenu hukohuko kwenu!
Si ndo hao wana Yesu wao na wanafunga hadi kufa..!! Kweli wabaki nayo makanisa yao
 
Ni shida Sana mungu atusaidie ni ngumu sana kujizuia eti mpaka tufunge ndoa na ni vizur ujue mwenzio ana utamu gani wa sukar au wa limao ili ufanye maamuzi sahihi

Sent from my Infinix X657 using JamiiForums mobile app
 
Wangekuwa kama mimi hapa wangeishi kwa amani ktk uhuru wao...ona sasa uhuru unavyoingiliwa kupitia imani..ona wale wengine wa shakahola walivyobaki mafuvu kupitia imani.
Wazungu nyie na waarabu mlichotuletea huku Africa(dini)tumekuwa watumwa tena.Tunauwana kwa mlango wa imani ya dini huku nyie huko ulaya mnabuni jinsi ya kuboresha picha za porno na uchafu mwingineo.
Haya bana Mungu amesema subirini miezi 12..endeleeni kusubiri.
Mie tunda langu nililila kabla hata ya ndoa, na hakuna mtu aliyenihukumu, tuna mwaka wa 18 ktk ndoa sasa.waliowekewa sheria kutokulana tunda, wengi walishaachana ktk muda huo.,Uhuru, uhuru.
 
Back
Top Bottom