Kanisa laahirisha ndoa baada ya watarajiwa kukiri kuzini

NostradamusEstrademe

JF-Expert Member
Jul 1, 2017
3,032
4,028
''Asiye na dhambi awe wa kwanza kuokota mawe na kuwapiga hawa watuhumiwa''.........mwisho wa kunukuu sasa endelea na story

======
1684907658791.png
Bibi na Bwana harusi watarajiwa wamejikuta wakishindwa kufunga pingu za maisha baada ya Kanisa kukataa kuwafungisha ndoa kutokana na kile kinachodaiwa walishiriki tendo kabla ya kufunga ndoa kitu ambacho ni kinyume na taratibu za dini.

Watarajiwa hao kutoka Kaunti ya Tana River nchini Kenya walikiri kuwa walikuwa wakifanya mapenzi kabla ya ndoa sababu ambayo ililifanya kanisa kuwafukuza na kutaka wakatubu.

Inaelezwa kwamba wakati wa kikao cha ushauri na maungamo kwa wanandoa hao watarajiwa, bwana harusi alikiri lakini bibi harusi mtarajiwa alikana kuwahi kushiriki tendo hali ambayo ilimfanya Mchungaji kuwaita ofisini na baadae kukiri.

Hatua hiyo ilimfanya Mchungaji Eli Mwakisha, kukasirika na kutishia kuwalaani wawili hao. Mwakisha aliwafukuza ofisini kwake na kuita timu ya maombezi kwa ajili ya sakata hilo.

Baada ya saa mbili za maombi mazito, aliwaita tena ofisini na kuwaambia watengane na kusimamisha mipango ya harusi kwa muda wa miezi 12 huku akisema hayo yalikuwa ni maagizo ya Mungu.

Kiongozi wa maombi katika kanisa hilo Helida Kase, amesema wawili hao waliagizwa kutumia muda huo kutubu na kuomba, lakini pia wahakikishe wanahudhuria ushauri wa wanandoa kila Jumatano, Ijumaa na Jumapili.

Wanandoa hao watarajiwa walikataa kuzungumzia suala hilo huku baadhi ya waumini wa kanisa wakiona kuwa hio haitakuwa harusi ya kwanza kusimamishwa au kufutwa, kama ilivyo kawaida wakati watarajiwa walio katika uchumba wakigundulika wamefanya mapenzi kabla ya ndoa.

Source: Mwananchi
 
Hhaaahahaaa labda sio mimi. Wakihairisha naenda kutafuta kanisa jingine nafunga.na nahamia huko hata kanisa la maombezi.kwani sh ngapi?

Hakuna dhambi kubwa wala ndogo,dhambi ni dhambi tu.alietukana na aliezini wote ni sawa tu!

Neema ya bwana Yesu kristo aliyonipa nkipiga goti dakika moja kwa kumaanisha nkatubu nkimaanisha mi na mchumba yameisha tunaingia ndani ya ndoa tukiwa safi.

Sasaa miezi 12 hadi vikao vya sherehe visimamishwe..

Wakenya bakini na makanisa yenu hukohuko kwenu!
 
Huyo pastor hakutenda haki, siku hizi wachumba wanaonja mpiko kabla ya kufunga pingu za maisha. Tena kuna wengine wanafunga ndoa tayari kitu na box kimo. Mambo yamebadilika sana kijana anaweza kuwa na wachumba wengi na wote anawatembezea mjegeje bila haya, mwisho wa siku anawatosa na kuibuka na mmoja.

Mapasta wengine hufutilia siku ya mimba kutungwa tangu ndoa ifungwe, mimba ikionekana mapema hesabu ya siku inapigwa, ikibainika mimba iko nje na muda tangu ndoa ifungwe wanandoa wanatengwa ushirika mpaka watubu au wanafukuzwa kanisani kwa dhambi ya uasherati.
 
Kuna vijana na mabinti wakitaka kuoana na wanaona kuna mlolongo wa mambo mengi ya harusi wanabebana hivyohivyo bila kufunga ndoa. Adhabu wanayopewa na wachungaji ni kutengwa kushiriki ibada mpaka watubu kuoana bila kufunga ndoa,
 
Siku hizi kuna changamoto kubwa kusubiri uje uzindue albamu siku ya ndoa, wakati we umejikaza huli, wenzako wanakula, inabidi na we ule tu kabla ya ndoa japo si utaratibu kula vituz kabla ya ndoa. Uhuni umezidi sana
 
''Asiye na dhambi awe wa kwanza kuokota mawe na kuwapiga hawa watuhumiwa''.........mwisho wa kunukuu sasa endelea na story

Bibi na Bwana harusi watarajiwa wamejikuta wakishindwa kufunga pingu za maisha baada ya Kanisa kukataa kuwafungisha ndoa kutokana na kile kinachodaiwa walishiriki tendo kabla ya kufunga ndoa kitu ambacho ni kinyume na taratibu za dini.

Watarajiwa hao kutoka Kaunti ya Tana River nchini Kenya walikiri kuwa walikuwa wakifanya mapenzi kabla ya ndoa sababu ambayo ililifanya kanisa kuwafukuza na kutaka wakatubu.

Inaelezwa kwamba wakati wa kikao cha ushauri na maungamo kwa wanandoa hao watarajiwa, bwana harusi alikiri lakini bibi harusi mtarajiwa alikana kuwahi kushiriki tendo hali ambayo ilimfanya Mchungaji kuwaita ofisini na baadae kukiri.

Hatua hiyo ilimfanya Mchungaji Eli Mwakisha, kukasirika na kutishia kuwalaani wawili hao. Mwakisha aliwafukuza ofisini kwake na kuita timu ya maombezi kwa ajili ya sakata hilo.

Baada ya saa mbili za maombi mazito, aliwaita tena ofisini na kuwaambia watengane na kusimamisha mipango ya harusi kwa muda wa miezi 12 huku akisema hayo yalikuwa ni maagizo ya Mungu.

Kiongozi wa maombi katika kanisa hilo Helida Kase, amesema wawili hao waliagizwa kutumia muda huo kutubu na kuomba, lakini pia wahakikishe wanahudhuria ushauri wa wanandoa kila Jumatano, Ijumaa na Jumapili.

Wanandoa hao watarajiwa walikataa kuzungumzia suala hilo huku baadhi ya waumini wa kanisa wakiona kuwa hio haitakuwa harusi ya kwanza kusimamishwa au kufutwa, kama ilivyo kawaida wakati watarajiwa walio katika uchumba wakigundulika wamefanya mapenzi kabla ya ndoa.
Source Mwananchi
Hiyo miezi 12 ndio kabisa mpaka mimba
 
Back
Top Bottom