Kanisa la Wasabato Mnapaswa Mkosoe maovu ya serikali zaidi kuliko kukosoa wenzenu wa Roman Catholic

Robert Heriel Mtibeli

JF-Expert Member
Mar 24, 2018
21,340
51,900
KANISA LA WASABATO MNAPASWA MKOSOE MAOVU YA SERIKALI ZAIDI KULIKO KUKOSOA WENZENU WA ROMAN CATHOLIC.

Anàandika, Robert Heriel
Mtibeli.

Mimi nimezaliwa kwenye Usabato, nimekua na kulelewa kwenye Usabato. Kimsingi Mimi ni Msabato ingawaje ni Mtibeli kiasili. Yaani tuseme ni Mtibeli aliyezaliwa katika Dhehebu la kisabato. Sasa sisi Watibeli ni Watu wa kusema ukweli hata kama unatugusa wenyewe. Hatunaga ushabiki.

Licha ya Wasabato wengi kubobea katika Mafundisho ya biblia na dini yao lakini wanaupungufu mkubwa wa kuisema Kweli hasa linapokuja suala la siasa, utawala na serikali.

Ni ngumu sana kusikia Kanisa la Sabato likikemea maovu ya Serikali. Kwa upande wangu sijawahi kusikia. Ila wakati huohuo ni rahisi kusikia kanisa la Wasabato wakiipongeza serikali na kuiombea. Hapa ndipo Watibeli tunapoona kuna tatizo fulani la Unafiki.

Wasabato wamefundishwa kutojihusisha na siasa. Kanisa pia moja ya sera zake ni kutojihusisha na siasa.

lakini Wasabato ni mabingwa duniani wa kukosoa dini zingine hasahasa Ukatoliki ambao ndio Mama wa Ukristo. Hata biblia inayotumika ni Wakatoliki walioiratibu na kuipanga. Ukisema bila ukatoliki hakuna biblia utakuwa upo sahihi kwa sababu Biblia ilikusanywa na wakatoliki. Nisitoke nje ya mada, na wala Wakatoliki wasidhani nawatetea hapa.

Hakuna kanisa lolote au dini yoyote itakayokuwa ya haki na sahihi zaidi ya ile inayotetea haki na kuikosoa serikali. Hakuna dini wala dhehebu hilo.

Manabii wote, mitume wote, Makuhani wote, Waamuzi wote walijihusisha na siasa hasa pale mambo yanapoenda Mrama au viongozi wa kisiasa wanapogeuka wadhalimu au kutenda maovu.

Yesu mwenyewe ambaye ndio msingi wa ukristo aliikosoa serikali na vyombo vya Dola.

Sasa iweje Wasabato wanajitoa katika wajibu huo.

Utatakaje Haki bila kujiingiza kwenye siasa ? How?

Yaani uwaambie waumini wako waache dhambi wakati msingi wa dhambi unabebwa na siasa.

Waumini watashikaje amri za Mungu bila kukemea viongozi wao wa kisiasa? how?

Amri kama ya kufanya kazi ambayo ni moja ya amri za Mungu, Muumini anafanya kazi kwenye serikali yenye mazingira ya mengi ya rushwa, wizi, ufisadi, dhulma alafu muda huohuo Kanisa halikemei serikali ikiwa na baadhi ya viongozi madhalimu, hivi kweli inakuja Akilini?

Unasema lengo la kanisa ni uinjilishaji,haya utafanyaje uinjilishaji kwa Watu na jamii inayodhulumiwa?
Badala ya kusaidiana na jamii kukabiliana na baadhi ya viongozi madhalimu ninyi mnawatia moyo wakijinga kuwa ati tumaini lipo wakifika Mbinguni kwani duniani kuna dhiki.

Wasabato tumekuwa kama Wamishenari walioungana na makoloni kututawala na kulainisha mioyo yetu kwa aya za kuokoteza.

Tumekuwa Machawa wa Watawala.

Haya mnahubiri neno la kweli, lakini kweli gani yenye mipaka? Kweli inayohusu Watu duni, dhalili, Waumini wasio na Mamlaka ndio kweli?

Kweli inayowaogopa Watawala na serikali? Hiyo ni kweli gani hiyo?

Tumekalia Sabato
Alama ya mnyama!
Sijui Papa!

Kama mnashindwa kuikosoa serikali mnayoiona mtawezana na Mambo ya Mnyama au huyo Papa kweli?

Tuacheni kuwa Machawa wa serikali!

Mbona Wakatoliki na Walutheri mabaraza yao kila mara hutoa matamko ya kukosa serikali pale wanapoona unakosea?

Dini ya kweli ni ile inayopigania Haki. Na huwezi pigania haki bila kuigusa siasa na serikali kwa sababu hao ndio wanahusika na mambo ya kutoa Haki.

Tusiwapotoshe waumini kuwa ati ufalme wa duniani hatuhusiani nao ilhali ibiblia iko wazi kuwa sisi ni Watu wa duniani na asilimia mia moja tunautawala huku duniani. Huko mbinguni sio kwetu na hata biblia yenyewe inakiri hilo. Ndio maana hata tukienda huko kama biblia isemavyo hatutakaa milele isipokuwa miaka elfu tuu.

Acha nipumzike sasa!

Robert Heriel
Taikon wa Fasihi
Kwa sasa Dar es salaam
 
SDA wako busy kuuza vitabu vyao vya matunda🤣🤣 kwenye maofisi na stend,ndo kazi yao,kitabu Cha elfu 7,watakuuzia elfu 50,na wanajua kudai hatari,kama mikopo kausha damu🤔

Halafu Hawa jamaa,si ndo waliganda airport kipawa,JK Nyerere Airport,kipawa,daslam,wakiwa na mabegi yaliyochoka na hawakuwa na nauli,wakasema wanamsubiri Yesu,awasafirishe kimiujiza👁️
 
Kanisa haliipongezi serikali, sijawahi kusikia wakikaa vikao vya kuipongeza serikali. Ila lina wajibu wa kuiombea serikali na kukemea dhambk na nadhani wanafanya hivyo.

Wabaki hivyo hivyo, kukosoa ni kazi za vyama pinzani, sio kazi ya kanisa.

Nisichopenda na huwa sifurahi ni kujilinganisha na wengine, kuona kanisa lipo sawa kulinganisha na wengine, kuponda wengine. Mengine yote naamini wapo sawa.
 
Inamana mpaka leo haujajua kipimo cha kanisa halisi na la kweli la Mungu.

Mungu aliweka vipimo na mizani.

Ili wanawake waliweke kila kanisa na kulipima.

Kama halitoshelezi basi Mungu hayuml ndani yake.

Wengi wanadhani wapo na Mungu kumbe ni zamani walishamuacha.

Mariamu na yusufu walizani hvyo pia kumbe walimuacha hekaluni.

Kanisa ni mwiko kujihusisha na siasa.

Kudai haki , ama kampeni zozote zile.

Kazi ambayo kanisa limeachiwa ni kuhubiri injili kwa kila kiumbe, kazo ambayo makanisa hawaitaki kabisa kwa sasa

Wapo bize na mashule,mahospitali, vyuo na mambo mengine ya kidunia.

Hayo ni mazuri ila sio kazi ya kanisa halisi.

Biblia inasema katoliki ni kahaba mkuu na mama wa makahaba, amezaa binti makahaba wanafanana nae

Na kila kanisa litalotoka kwa roman mwisho wa siku hurudi tena kwenye mifumo ile ile waliyotoka
Kkkt, anglican, pentecost na mengine yote.

Katoliki ni adui kuu wa dunia hii, ushoga upo nyuma ya vatican,marekan ni mdomo wake tu.

Uchafu wote wa makanisa asili ni roman.
 
Ni sawa na nzii kwenye mgongo wa nyati.
Mungu alishaliona ilo ndomana akaandika haya. Lenyewe linadhan linanguvu na haliitaji kitu.


Ufunuo wa Yohana 3:15-18
[15]Nayajua matendo yako, ya kuwa hu baridi wala hu moto; ingekuwa heri kama ungekuwa baridi au moto.

[16]Basi, kwa sababu una uvuguvugu, wala hu baridi wala moto, nitakutapika utoke katika kinywa changu.

[17]Kwa kuwa wasema, Mimi ni tajiri, nimejitajirisha, wala sina haja ya kitu; nawe hujui ya kuwa wewe u mnyonge, na mwenye mashaka, na maskini, na kipofu, na uchi.

[18]Nakupa shauri, ununue kwangu dhahabu iliyosafishwa kwa moto, upate kuwa tajiri, na mavazi meupe upate kuvaa, aibu ya uchi wako isionekane, na dawa ya macho ya kujipaka macho yako, upate kuona.
 
Mungu alishaliona ilo ndomana akaandika haya. Lenyewe linadhan linanguvu na haliitaji kitu.


Ufunuo wa Yohana 3:15-18
[15]Nayajua matendo yako, ya kuwa hu baridi wala hu moto; ingekuwa heri kama ungekuwa baridi au moto....
Kanisa Katoliki limetajwa wapi hapo?
 
Back
Top Bottom