Bando la wiki
JF-Expert Member
- May 23, 2023
- 314
- 877
Naona ni muda muafaka kanisa katoliki Tanzania kujitoa kwenye makucha ya Papa chini ya mfumo wake wa Roman Catholic.
Haingii akilini, makanisa tumejenga sisi waumini, magari tuwanunulie mapadri na maaskofu halafu hatokee mtu from nowhere kisa ni papa abadilishe asili ya mwanadamu kwa kutaka mashoga kubalikiwa ndani ya kanisa takatifu la Yesu kristo.
Kanisani wanaingia wazinzi, waasherati, wachawi, walevi, wezi, majambazi, waongo, na kila aina ya watenda maovu. Wanapoingia kanisani kuomba TOBA huwa ni jambo la siri baina yake na padri, wakisha pata toba wanarudi kwenye mstari kimya kimya pasipo kuwa exposed kwa waumini wengine.
Hakuna uspesho wowote walionao mashoga kiasi kwamba kanisa lishugulike nao kuwabaliki badala ya kuingia kanisani kama watu wanaopinga ushoga na watu wanaotaka msaada ili waache tabia yao hiyo chafu ya ushoga.
Sasa kanisa kumbukeni mambo huanza mdogo mdogo namna hii ya kuwabaliki mashoga na mwisho kabisa ni kuanza kuwafungisha ndoa wanaume wawili ndani ya kanisa takatifu la kristo.
Waumini hatutakubaliana na jambo hilo, ni bora nitafute kanisa lingine la kikristo nikamuabudu Yesu huko kuliko kufungamana na ninyi kwa kuruhusu dhambi hii ya ushoga kanisani.
Viongozi wa dini nadhani mnakumbukumbi namna dhambi ya ushoga ilivyo uangamiza miji ya Sodoma na Gomola. Mungu ni yule yule aliye uangamiza miji hiyo kwa kuchukizwa na agenda ya mashoga kuondoa mpango wa Mungu duniani wa mwanaume na mwanamke kuungana pamoja katika ndoa takatifu ili wawe kiwanda cha kuujaza ulimwengu.
Sasa ni muda kwa baraza la maaskofu Tanzania (TEC) kumwandikia barua/ waraka Papa kupingana na hoja yake ya kubaliki mashoga kanisani. Kama ambavyo Tec mlithubutu kuiandikia serikali waraka kupinga uwekezaji wa kimagumashi wa DP World nadhani pia ni muda sahihi kufanya jambo hilo hilo kwa kupinga wazi wazi uamuzi wa papa ili sisi waumini tusiwaone ninyi ni manafiki ambayo bwana Yesu aliwataadhalisha kwenye:
"Mathayo 23:15
[15]Ole wenu waandishi na Mafarisayo, wanafiki! Kwa kuwa mnazunguka katika bahari na nchi kavu ili kumfanya mtu mmoja kuwa mwongofu; na akiisha kufanyika, mnamfanya kuwa mwana wa jehanum mara mbili zaidi kuliko ninyi wenyewe."
Mkashamwandikia hiyo barua ya kupinga hoja yake mmwambie hasipokubaliana nanyi ni bora kujitenga nae kuanzisha kanisa la Kristo litakalojulikana kama Tanzanian Catholic litakolodumisha ibada sahihi za bwana wetu Yesu kristo.
Baraza la maaskofu mkishindwa kufanya hivyo kubalini matokeo ya waumini wenu (mimi miongoni mwao) kuwakimbia na kumtafuta Yesu katika madhehebu mengine ya kikristo. Uzuri ni kwamba bwana wetu Yesu kristo hana mipaka kwamba anapatikana tu katika kanisa la RC popote pale unaweza kumuomba na akajibu.
Tumsifu Yesu kristo....